Napenda kufahamu juu ya hawa mbuzi

Napenda kufahamu juu ya hawa mbuzi

Shida iko kwenye kuwaleta. nilijaribu kuwasiliana na baadhi ya wauzaji wa huko lakini nilipatwa na mashaka na response zao.
niliweka mawasiliano yangu kwenye si moja , hivyo nimekuwa nikipokea quotation kadhaa ambazo nahisi asilimi kubwa ni wapigaji.

Hivi juzi kati kuna mtu moja alinitumia mesejei kwenye simu akidati yeye ni mfanyabiashara ya kule ta hao mbuzi ila yuko Kenya.
Bora kuwafungia safari tu kama unaweza
 
Hii itakuwa nzuri zaidi, ni bora uende mwenyewe hata kama ni south Africa kufuata kuliko kuuziwa copy mkuu
Matapeli wengi sana siku hizi
Bora kwenda ni unatalii pia na kupanua fikra zingine za biashara huko
Kenya ni jirani zaidi na unaweza kupata hata trucks zinazokuja kwa urahisi
Ila hakikisha unapata vibali vyote original wasije wakawachoma moto
 
mkuu kenya ni wafugaji wazuri wa mbuzi wa maziwa hata mbuzi wa nyama pia wenyewe wanabord ya ubora na wanyama wanasajiliwa kulingana na breed zao na ukitaka kununua breed pure unapata kupitia kwao, pia fanya kupilia page yao ya fb inaitwa MKULIMA YOUNG natumai utakutanan na wafugaji wengi na ndo itakuwa mwanzo wako kupata utakacho
 
Kama utawahitaji Hao Mbuzi wapo chuo cha kilimo sua na Tengeru, au tembelea morogoro kuna wafugaji wengi, Nilikuwa nao tulianza kuwafuga tangu mwaka 1998, Tuliwatoa Sua waliletwa kwa majaribio kutoka Norway na Tuliuza sana kwenye miradi ya Worldvision vijijini bei huwa ni kuanzia 100,000 hadi 200,000 hutegemea na Umri na Mara nyingi Huuzwa wakifikia umri wa miezi 3 kwa sasa sina kwasababu tulisitisha uzalishaji kwa muda. Changamoto ni Magonjwa Mfano ndigana, mafua, kwahiyo unahitaji upate darasa kwanza la sivyo utapata hasara kwasababu wanapata matibabu na chanjo mara kwa mara, Kwa ufupi uandae banda la juu kwasababu hawalali chini kama mbuzi wa kienyeji ili kuepuka magonjwa ya kifua, mafua, kuoza kwatwo, ugonjwa wa ngozi (Hawapatani na majimaji). Angalizo Hakikisha unanua mbegu ya mapacha kweli usije ukanunua sio na wenye rangi nyeupe ni kwaajiri ya maziwa na wekundu ni wa nyama
 
Habari wakuu.

Katika harakati za kupata maarifa mapya mtandaoni nilikutana na hawa mbuzi (picha chini) maelezo niliyosoma kuwahusu ni kuwa;

hawa ni mbizi wa nyama wanao uwezo mkubwa wa kupata uzito hadi kufikia kg 150 kwa dume. Pia jike lake hufika hadi kg 120 na huzaa mapacha.

Maelezo yanasema kuwa hawa mbuzi licha ya kuwa na miili mikubwa na pembe ni wapole. Na ni mbuzi wanaofaa sana kwa ufigaji wa mbuzi wa nyama.

Kwa bahati mbaya niliposoma habari ya kuwahusu mbuzi hawa hapakuwa na taarifa nilizoitaji kuzifahamu kuwahusu, sasa naleta kwenu wandugu kwa anayewafahamu anijuze haya yafuatayo:-

1. Wanapatikana wapi kwa hapa Tz

2. Wanachukua muda gani kuwakuza

3. Gharama za matunzo yao kwa wastani wa mbuzi 3. (Dume 1, jike 2)

4. Changamoto na ufugaji wake kwa jumla

Nimeambatanisha na picha zao
View attachment 933263
View attachment 933265

Natanguliza shukrani wakuu.
hawa nimewahi waona mbeya CRDB kwa nyuma kuna bar moja maarufu sana wanachoma mbuzi wa aina hii
 
150 kg jamani sio mchezo INA maana ukiuza nyama kwa bei ya 5000 unapata 750,000 kwa mbuzi huyo?
 
Kuna mzee anao ila uzito huo sijui kama wanafika

Wanaridhika na hali na wanazaa mapacha,
Aliniambia mtoto aliyemaliza kunyonya ana muuza 80,000
Nikamwambia ngoja nikafikirie, nikasahau leo ndo naona hapa nakumbuka
USINISAHAHU KWENYE UMALKIA WAKO!
 
Nimeattach picha moja hapo ina mawasiliano nyingine zilifutika. Ukipata muda nenda meru, siha, karatu wapo mpk vijijini ila wengi ni uzito wa 70-100kg asili yao ni Switzerland. Au ulizia makanisa ya kkkt kaskazini (wenye project) watakulink na wafugaji .

hudhuria maonesho ya 8-8 Arusha mwakani utawakuta kwa wingi na utanunua hapo hapo kwa bei tajwa.

Ufugaji wake ni wa ndani wanakatiwa nyasi hawatoki nje
thanks mkuu
 
mkuu kenya ni wafugaji wazuri wa mbuzi wa maziwa hata mbuzi wa nyama pia wenyewe wanabord ya ubora na wanyama wanasajiliwa kulingana na breed zao na ukitaka kununua breed pure unapata kupitia kwao, pia fanya kupilia page yao ya fb inaitwa MKULIMA YOUNG natumai utakutanan na wafugaji wengi na ndo itakuwa mwanzo wako kupata utakacho
hv kwann tanzania hatupo kama hawa wenzetu wakenya?..........


sisi tuna shida sana jamani
 
Back
Top Bottom