Napenda kufahamu juu ya hawa mbuzi

Bora kuwafungia safari tu kama unaweza
 
Hii itakuwa nzuri zaidi, ni bora uende mwenyewe hata kama ni south Africa kufuata kuliko kuuziwa copy mkuu
Matapeli wengi sana siku hizi
Bora kwenda ni unatalii pia na kupanua fikra zingine za biashara huko
Kenya ni jirani zaidi na unaweza kupata hata trucks zinazokuja kwa urahisi
Ila hakikisha unapata vibali vyote original wasije wakawachoma moto
 
mkuu kenya ni wafugaji wazuri wa mbuzi wa maziwa hata mbuzi wa nyama pia wenyewe wanabord ya ubora na wanyama wanasajiliwa kulingana na breed zao na ukitaka kununua breed pure unapata kupitia kwao, pia fanya kupilia page yao ya fb inaitwa MKULIMA YOUNG natumai utakutanan na wafugaji wengi na ndo itakuwa mwanzo wako kupata utakacho
 
Kama utawahitaji Hao Mbuzi wapo chuo cha kilimo sua na Tengeru, au tembelea morogoro kuna wafugaji wengi, Nilikuwa nao tulianza kuwafuga tangu mwaka 1998, Tuliwatoa Sua waliletwa kwa majaribio kutoka Norway na Tuliuza sana kwenye miradi ya Worldvision vijijini bei huwa ni kuanzia 100,000 hadi 200,000 hutegemea na Umri na Mara nyingi Huuzwa wakifikia umri wa miezi 3 kwa sasa sina kwasababu tulisitisha uzalishaji kwa muda. Changamoto ni Magonjwa Mfano ndigana, mafua, kwahiyo unahitaji upate darasa kwanza la sivyo utapata hasara kwasababu wanapata matibabu na chanjo mara kwa mara, Kwa ufupi uandae banda la juu kwasababu hawalali chini kama mbuzi wa kienyeji ili kuepuka magonjwa ya kifua, mafua, kuoza kwatwo, ugonjwa wa ngozi (Hawapatani na majimaji). Angalizo Hakikisha unanua mbegu ya mapacha kweli usije ukanunua sio na wenye rangi nyeupe ni kwaajiri ya maziwa na wekundu ni wa nyama
 
hawa nimewahi waona mbeya CRDB kwa nyuma kuna bar moja maarufu sana wanachoma mbuzi wa aina hii
 
150 kg jamani sio mchezo INA maana ukiuza nyama kwa bei ya 5000 unapata 750,000 kwa mbuzi huyo?
 
Kuna mzee anao ila uzito huo sijui kama wanafika

Wanaridhika na hali na wanazaa mapacha,
Aliniambia mtoto aliyemaliza kunyonya ana muuza 80,000
Nikamwambia ngoja nikafikirie, nikasahau leo ndo naona hapa nakumbuka
USINISAHAHU KWENYE UMALKIA WAKO!
 
thanks mkuu
 
hv kwann tanzania hatupo kama hawa wenzetu wakenya?..........


sisi tuna shida sana jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…