Napenda kufahamu kazi ya matunda ya tende kwa mwanaume

Napenda kufahamu kazi ya matunda ya tende kwa mwanaume

pastor muyamba

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2016
Posts
252
Reaction score
135
Wakuu matunda aina ya tende yana kazi gani ?na kwa siku ngapi yana fanya kazi ,na je mazuri kuliwa yakiwa mabichi su makavu ya supermarket?

Juisi ya tende je iko vizuri ?
 
Kwanini ule usivyovijua kula Maembe, ndizi,nanasi, Matikiti acha kula matunda usiyoyajua
 
Wakuu matunda aina ya tende yana kazi gani ?na kwa siku ngapi yana fanya kazi ,na je mazuri kuliwa yakiwa mabichi su makavu ya supermarket?juisi ya tende je iko vizuri ?
Tunda la tende linaongeza nguvu za kiume. Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo lako. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja na yakae usiku kucha.

Asubuhi, zisage tende hizo kwenye maziwa hayo hadi zichangayike, kisha weka asali kiasi cha vijiko vitatu au vinne vikubwa pamoja na unga wa hiriki, kiasi cha nusu kijiko kidogo. Kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.
FAIDA 10 ZA TENDE.jpg
 
Ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji chakula tumboni, hivyo utaondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia.

Pia ndani ya tende kuna virutubisho vya ‘amino acids’ ambavyo ni muhimu mwilini
 
Kuwa makini, tende zinazotajwa kuwa na manufaa kiafya sio hizi tunazopimiwa Kariakoo! Hizi kula tu uufurahushe ulimi!
Aisee wacha bwana!! Sikulijua hilo...

Enhhe.. hizo zenye manufaa zinapatikana wapi na zikoje mkuu
 
Wakuu matunda aina ya tende yana kazi gani ?na kwa siku ngapi yana fanya kazi ,na je mazuri kuliwa yakiwa mabichi su makavu ya supermarket?juisi ya tende je iko vizuri ?
Ninasikia ni matunda yalio na uwezo wa kuongeza vichocheo vya kuwa na hamu ya mapenzi kwa wote(me/ke)
 
Aisee wacha bwana!! Sikulijua hilo... Enhhe.. hizo zenye manufaa zinapatikana wapi na zikoje mkuu

Kaka hizi tunazoletewa akina sie huku, zimeshafanyiwa processing viwandani na kuongezwa vikorombwezo ikiwemo sukari! Tende zinazozungumziwa kiafya, zenye nutrients halisi ni zile unprocessed ambazo huku hakuna!
 
Attachments

  • Tende.jpg
    Tende.jpg
    110 KB · Views: 370
Kaka hizi tunazoletewa akina sie huku, zimeshafanyiwa processing viwandani na kuongezwa vikorombwezo ikiwemo sukari! Tende zinazozungumziwa kiafya, zenye nutrients halisi ni zile unprocessed ambazo huku hakuna!
Japo mimi sio mlaji saaana wa tende. Tupambane Na hali zetu... shilole countries
 
Kaka hizi tunazoletewa akina sie huku, zimeshafanyiwa processing viwandani na kuongezwa vikorombwezo ikiwemo sukari! Tende zinazozungumziwa kiafya, zenye nutrients halisi ni zile unprocessed ambazo huku hakuna!
Dodoma hizo hapo pichani zipo kibao
 
Back
Top Bottom