Napenda kuifahamu Tanganyika Law Society(TLS)


Na Mimi labda nikuulize tu Mkuu hivi kuna faida gani ya kuwa na Police Tanzania ambayo huwa inakurupuka kuwakamata Watu hovyo hovyo halafu wanaumbuka mbele ya safari?

Na swali langu la nyongeza Kwako hivi kuna faida gani Tanzania tunaipata hasa baada ya Mteule kupewa ushahidi wote juu ya mmoja wa Watumishi wake kudanganya Jina lake na anashirikiana na drugs barons kadhaa nchini lakini bado ametuwekea nta masikioni Watanzania?

Nitashukuru ukinijibu Mkuu na nayasubiri kwa hamu sana majibu ya hayo maswali mawili Kuntu niliyoyauliza hapo juu.
 
TlS ifutwe haina faida kwa Taifa
we ndio mshamba kweli. hivi unajua kesi zote mahakama kuu hasa hizo za murder etc ili ziendelee mahakama kuu lazima ziwe na wakili wa kujitegemea? bila wakili wa kujitegemea kesi inasimama palepale haiendelei, na ni serikali inalazimika kuwalipa hawa mawakili wa kujitegemea ili kuendesha kesi? ulishawahi kufika mahakamani wewe? ulishawahi kufikishwa polisi au mahakamani? siku ukifikishwa mbele ya pilato utakuja kuitapika hii kauli yako hakika. utawakumbuka wanasheria, na watakapokusaidia ushinde kesi ambayo pengine ni umebambikwa tu (kwasaababu ya chuki za kibiashara au za kisiasa)...utawashukuru. unaongea haujui ili yakikukuta utakuja kuelewa. hao wanasaheria wanao uwezo kugoma kabisa wasiendeshe kesi mahakama kuu, na serikali itapiga goti kuwaomba.

kwasababu kwa kawaida huwa wanajitolea tu kuisaidia serikali kesi ziende, wasipoenda huwezi kuwafanya kitu kwasababu kwanza wamesoma na wanalipa kodi kwenye lawfirm zao na huwezi kuwalazimisha wafanye kitu wasichokitaka, ni biashara kama biashara zingien tu.
 
Kipi wamewahi kufanyaaa Ikaonesha wao ndio Stop engine
 
Nguvu kubwa iliyotumika kutaka kumzuia Tundu Lisu inaonyesha umuhimu wa TLS katika kuipiga break serikali inayokanyaga sheria za nchi.
Utashi wa mtu mmoja hata akiwa ni Rais hauwezi kuwa mbadala wa sheria za nchi.
 
Kwanza Hayo siyo Maswali Kuntu! Tukianza na swali lako la Kwanza! Kazi ya Polisi ni kulinda amani na usalama wala Raia wake! Kumbuka Polisi sio mahakama wala sio majaji! Kazi ya polisi ni kuwafikisha watuhumiwa kule wanakotakiwa Mambo ya Ana haki au hana haki huja baadae hii ni kwa nchi zote dunianiii!! Ndio maana kukawa na Mahakama Sidhani kama wewe Ukimkuta Mwizi nyumbani kwako polisi wakija utataka waanze kuhukumu Kesi kama kaiba kweli au hajaiba....watakacho fanya ni kumfikisha Katika vyombo vya sheria vinavyo takiwaaa!!!

Swali lako la pili.....Serikali haiongozwi na instagram Tuhuma zote mnazo zitoa hazina Ushahidi hata kidogoooooooooo......Kama mnatuma ambazo zina ushahidi si dhani kama Instagram na Kanisani ni mahali sahihi pakuoneshaaa tuhuma zenu na kusubiri majibu!! Leteni ushahidi tuanze na wewe ushahidi uliona nao ni upii toa ushahidi! Mfano ukisema fulani ana Vyeti feki toa ushahidiii ni simplee tuuu Haiana haja ya kubishana mfano Kuna mtu alisema ana Vyeti vyake ni kwanini asiviweke kuonesha huo ushahidi? Kwanini msiendee mahakamani?

Nilishawahi kuandika hapaa kuhusu hilo na ninashukuru meya wa Dar alinisikiliza na Amesema J4 anaenda mahakamani means huyo ana Ushahidiiii na huyo ndio msomi tunae mtaka kama Akishindwa kesii na Akiambiwa amlipe Fidia mtuhumiwa Msisite kumsaidia!

Lakini kuendelea kulia kwenye Insta sio solution?

Tuendelee na mjadala wetu Nipe Faida za TLS
 
mpe darasa huyo mwana kwetu
 
Nguvu kubwa iliyotumika kutaka kumzuia Tundu Lisu inaonyesha umuhimu wa TLS katika kuipiga break serikali inayokanyaga sheria za nchi.
Utashi wa mtu mmoja hata akiwa ni Rais hauwezi kuwa mbadala wa sheria za nchi.
Sheria gani Iliyo Vunjwaa? Na wakati inavunjwaa TLS haikuwepooo?
 
Hongera Lissu kwa ushindi mnono, I wish TLS ingekua na uwezo wa kufanya mabadiliko kwenye katiba ya TZ.
mtaalamu aliye pata atafanya kweli,uwe mpole tu,Nchi ina hitaji watu kama Lisu wengi ili kutoka katika giza nene hili
 
Ilikuwa ikiongozwa na makada wa CCM wakawa hawawezi kufanya kazi.
 

Majibu yako yamenifanya nisipoteze tena muda wangu kuendelea kujibizana nawe kwani umeonyesha Kiwango chako duni kabisa cha Kufikiri.
 
hizi ndo faida chache tu kwa kukusaida

1.wakili yeyote akiwa kazini hutetewa na hiki chombo pindi sinzonje akikurupuka
2.kinatoa msaada wa kisheria katika nchi pale unapoitajika
3.ndio kitovu cha sheria tanzania
4.kipaza sauti cha wanasheria tanzania
5.mwarobaini pindi bunge linapojichanganya kisheria
6.huwakilisha tanzania kisheria katika mikutano ya kisheria nje ya tanzania
7.kinakosoa serikali na mihimili mingine pindi wanapokosea kufafanua sheria husika
 
Huko ndio kushindwaa kaa pembeni

Kamwambie Bosi wako sasa kuwa mwisho wake wa kuwaonea Wadanganyika umefika kikomo kwani Mwanamume Tundu Antipas Lissu amekalia Kiti na sasa tutaheshimiana tu Kisheria. Narudia tena kukuambia na hadi nakuhakikishia kuwa 75% ya Wanasheria na Mawakili waliompigia Kura za kutosha Lissu wanatoka Chama Tawala cha CCM je umeshajua ni kwanini na wao wamechoka na leo wakaamua kufanya maauzi magumu ila mazuri na yenye maslahi kwa Watanzania wengi wanyonge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…