Habari wakuu naombeni kuuliza je kwa mfano nikawa nimeagiza gari yangu toka nje na imefika bandali ya Dar. Vipi kuhusu ghalama na process zakulitoa gari zinakuaje?
Here is the process;
1. Chagua gari yako unayotaka kununua toka kampuni yoyote online. Usione soni kushirikisha rafiki, jamaa au ndugu mzoefu anayejua kufanya haya mambo. Don't pretend you know kumbe you don't or you know just a little...
Kuna jamaa yangu mwaka 2012 alijifanya anajua. Akanunua gari toka Japani aina ya Honda CR -V kwa dola 4,000 sawa na Tshs 8,000,000 wakati huo. Gari ikafika nchini vizuri kabisa bandarini DSM. Akashindwa kuikomboa bandarini kwa sababu alidhani ndiyo amemaliza. Hakujua kuwa kuna kodi na tozo za TRA karibu au zaidi ya Tshs. 9,000,000 tens...!
Unajua kulitokea nini? Ilimlazimu kuuza gari hilo hapo hapo bandarini chini ya Tshs. 5,000,000 kwa wajanja....!!
2. Watakupatia kitu kinaitwa "QUOTATION OF PRICE FORM & PROFORMA INVOICE" ikionesha gharama ya gari lenyewe (FOB) na gharama za usafirishaji + insurance (CARGO IN FREIGHT a.k.a CIF). CIF ni gharama ya gari lenyewe + transportation from the original country to the destination country ktk bandari uliyochagua wewe kupokelea gari yako..
3. Ukishapokea hiyo fomu ya bei ya gari (quotation form & proforma invoice), fanya utaratibu wa kwenda kulipia gari yako aidha kupitia benki au njia zingine zozote za kufanya malipo kwa kadiri utakavyoelekezwa na kampuni inayokuuzia gari yako...
4. Ukishakamilisha kulipia gari yako huko, utaratibu wa kusafirishiwa gari yako mpaka bandari utakayoipokelea gari yako hufanyika mara moja. Kwa Tanzania mara nyingi ukiagiza gari popote iwe Marekani au Ulaya au Asia hususani Japan, Korea au Uchina, huchukua muda wa Sikh kati ya 45 na 90 kufika bandari ya Dar...
5. Mpaka hatua hiyo, unakuwa umeshanunua gari tayari. Lakini haiwezi kuruhusiwa kuwa barabarani hata itakapokuwa imefika bandarini mpaka uhakikishe umelipia kodi na tozo zingine zote za serikali ndipo utaruhusiwa kuondoka na gari yako. Kwa hiyo hatua ya tano ni hii...
5. Chukua hati ulizonunulia gari yako, nenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Waoneshe nyaraka za ununuzi wa gari yako, kisha watakukokotelea kodi na tozo zingine zote za gari yako ikiwemo gharama ya usajili (Registration) ya gari yako hapa nchini Tanzania...
Ukishapewa gharama hizo, nenda benki lipia na tunza nyaraka hizo zote ulizofanyia malipo ya gari + TRA...
6. Subiri gari yako ifike. Ikifika bandarini, pokea gari yako. Ikatie Bima na Stika ya usalama barabarani. Kisha start enjoying driving...
MUHIMU na ZINGATIA HILI:
å Kama siyo mzoefu au hujawahi kuagiza gari mwenyewe moja kwa moja toka nje ya nchi, usije ukajiingiza kichwa kichwa kujifanya unaelewa bila kupitia kwa mtu mzoefu na unayemwamini....
Kuna matapeli wabobezi wa kimataifa wako kwenye sekta hii na huwaliza watu wengi sana kila siku. Be careful & intelligent before you go...
å Kwa usalama wa fedha zako na kuwa na uhakika wa kupata gari yako, ni vyema sana ukatumia fedha zaidi kidogo kwa kuwapa na ukawawatumia mawakala wabobezi na wazoefu wa kuagiza magari toka nje wafanye kazi hiyo kwa niaba yako. They are so good kiasi ambacho watakuletea gari yako mpaka nyumbani kwako ukitaka...
However, napo pia kuwa makini. Maana ziko kampuni zingine za uwakala wa uagizaji magari hapa hapa nchini zina watu wasio waaminifu ambayo wanaweza kukutapeli vilevile...
Shirikisha watu wazoefu watakuongoza..
ASANTE..