Napenda kujua hatua za kulitoa gari bandarini

deal na registraton year ndo mwaka gari ilikua imeingia road.
Mkuu hii nimeitoa beforward.Hivi hapa vitu vilivyopo kwenye gari ni hivyo vyenye rangi ya orange au ni hivyo vyenye white iliyofifia?Yaani kwa mfano gari hii ina CD player au haina?
 
Nenda showroom ya Janinternational wana offer ya Toyota passo kwa M6.5
 
Nafikiri changamoto yangu ni kwenye kujaza model.Kwenye website ya beforward hizi model ninazipata sehemu gani?
Model number unayoitaka mfano kwenye hii Subaru ni hiyo GH2. Kila model ya gari ina namba zake, angalia hapo utaziona, na pia utaziona zikifanana na za kwenye site ya TRA.
 
Wakala wa forodha si lazima. Serikali ilibadili sheria ya wakala wa forodha na kuruhusu watu binafsi kuchukua mzigo bandarini bila ulazima wa wakala wa forodha. Kutumia wakala ni hiyari yako na sio lazima.
 
Kutumia wakala wa forodha sio lazima. Serikali ilibadili sheria na kuondoa ulazima wa mtu kutumia clearing and forwarding agent. Sio lazima ukitaka unatoa gari yako mwenyewe.
 
Asante kwa nyongeza na masahihisho. I agree with you...
 
Kutumia wakala wa forodha sio lazima. Serikali ilibadili sheria na kuondoa ulazima wa mtu kutumia clearing and forwarding agent. Sio lazima ukitaka unatoa gari yako mwenyewe.
Exactly...

Ndiyo maana serikali imeweka utaratibu mzuri Wa kiasi ambacho mtu anaweza kununua gari kwa kutumia viganja vya mikono yake tu kwa sababu gharama zote za bei ya Gari, ushuru Wa bandari, kodi za TRA nk nk mpaka gari kufika mkononi mwa mtu ziko wazi online 24hrs..

Kwa maana kuwa, mtu anaweza kulipia kila kitu i.e gari yenyewe, gharama za kulisafirisha, tozo za serikali zote na za bandari kwa kutumia simu au PC yake comfortably while seated home bila kumtumia mtu Wa tatu (wakala)...

Hii haina maana kuwa mawakala hawana maana au umuhimu. Hawa ni wazuri, wazoefu, wanazijua fitna za bandarini na za sekta hii kwa ujumla na hivyo wanasaidia sana especially kwa wateja au watu wasio wajuzi na wazoefu Wa kuagiza Magari toka nje ya nchi...
 
Mkuu una maelezo mazuri sana[emoji122][emoji122]

Kwa kuongezea, SBT na Befoward wana branch zao hapa Dar es salaam so hata ukiwatumia wale hakuna kinachoharibika, kuliko mtu kuhangaika na huna ufahamu wa hivi vitu
 
Mkuu hii nimeitoa beforward.Hivi hapa vitu vilivyopo kwenye gari ni hivyo vyenye rangi ya orange au ni hivyo vyenye white iliyofifia?Yaani kwa mfano gari hii ina CD player au haina?
View attachment 1716308
Vyenye orange ndizo accessories zilizoko kwenye gari yako, hizo fainted ni kuwa hamna japo saa ingine inaweza kuonekana hivo while zingine zinafanya kazi

Kazi kwako churaaa[emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
Habari wakuu naombeni kuuliza je kwa mfano nikawa nimeagiza gari yangu toka nje na imefika bandali ya Dar. Vipi kuhusu ghalama na process zakulitoa gari zinakuaje?
Process ni vema ukatutafuta sisi mawakala(clearing agent) ambao makampuni yetu yamesajiliwa na TRA pamoja na TPA. Inachukua siku 2 mpaka 3 kukamilisha process za kugomboa gari bandarini.
Gharama ziko kwenye makundi matatu (4) kama ifuatavyo;
A. Ushuru wa TRA: hapa ushuru utategemea na taarifa za gari husika.
B. Gharama za Bandari (Port Charges)
1. Handling: ambayo hutozwa $7 jumlisha VAT kwa CBM moja (Urefu x Upanax Kimo).
2. Wharfage charges: hutozwa 1.6% jumlisha VAT ya thamani ya gari (CIF value).
3.Corridor Levy: hutozwa $0.3 jumlisha VAT kwa CBM moja.
C. Gharama za Uwakala wa Meli (TASAC Fee): hutozwa $2.5 kwa CBM moja.
D. Gharama za Ukaguzi wa TBS (Destination Inspection charges): hutozwa $150 kama Inspection fee na TZS30,000 ikiwa ni service fee.
Mwisho mkuu ni ada uwakala, karibu katika yangu itakutoza Laki Mbili Tu (200,000). Napatikana kwa aniani ifuatayo;
Ruaha Freight Ltd,
Samora Avenue,
NHC building (between Samora House & Exim Bank),
Dar es Salaam.
Mob: 0718 866 651 (Whatsap or Call)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…