Napenda kukitetea Chuo changu cha Mlimani (UDSM)

kukumdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2011
Posts
2,871
Reaction score
2,762
Kumekuwa na Taarifa kuwa UDSM kinazalisha vilaza. Napenda kuwahasa wananchi waendelee kusoma pale maana ndio chuo pekee kinachotoa elimu bora kuliko vyote Tanzania. Matatizo ni machacha sana kwenye kitengo cha uchumi, kitengo hiki hakina walimu ndio maana wanaomaliza uchumi pale bila kupata elimu ya ziada nje ya nchi unakuwa useless katika taifa. Walimu wote wa uchumi wa UDSM ndio hovyo paka kupelekea wahitimu kutotoa mchango wowote katika nchi hii! Hivyo naomba mjue vitengo vingine viko sawa kabisa ila kitengo cha uchumi ni chakukiangaliza zaidi ikiwezekana kifutwe ili chuo kisiendelee kuchafuka.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Chuo ni kizuri ila kuna wahuni wachache waliosoma pale kama akina Mwigulu Nchemba na Juliana Shonza wanakuwa kama "vilaza" hawajielewi mfano Mwigulu anapotoa upuzi wake kisha lundo la wafuasi wake mfano wa Juliana Shonza wakamuona shujaa na kuongezea maneno mengine ya hovyo kabisa.Hawajawahi kujenga hoja ndani ya CCM hata siku moja..Hawa wamepata elimu yao ndani ya chuo bora kabisa nchini 'UDSM'..Kweli sisi wengine alumni wa pale tunaonekana wa hovyo kabisa.
 
Itabidi tuwawajibishe

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Wanatumika wapate mradi wao. Inaanza kulipa. habari za kuaminika J.Shonza amezawadiwa Ofisi na Gari, Nini zaidi kwa mtu ambae anatumikia tumbo?
 

Mada inahusu udsm sio Mwigulu. Wakati weka siasa pembeni ujadili mambo ya msng.
 
'kinachotoa elimu bora kuliko vyote Tanzania'...kweli? Hata kwa medical-related courses? How about agricultural course? Ama ni bora kwa kozi uliyosoma wewe? unatushawishije kua kinatoa elimu bora kuliko vyote wakati unaponda Economics ya pale na pengine kuna vyuo vingine vizuri vya kozi hiyo?

tragedy of the commons
 
Viongozi wengi wa juu hapa nchini wamepita UDSM, na tunaona utendaji wao ulivyo mmbovu kiasi kwamba kuifikisha hii nchi hapa ilipo, na hata unapo wauliza maswali ya msingi hujibu utumbo kama Mwigulu na hata kauli zao ni tata, mfano Rais, anaulizwa why tanganyika ni maskini.. nae anajibu hajui. Waziri mkubwa.. anasema wakikaidi Piga tu.. unaona tu kabisa hicho chuo kinazalisha vimeo.
 

Inaonyesha ni jinsi gani usivyo ujua ukilaza wa UDSM. Na hata hujui unacho kitetea pia. Wewe mwenyewe kwa jinsi ulivyo andika tayari usha-thibitisha kwamba umejaa ukilaza. Halafu unakuja kutetea ukilaza wa UDSM wakati wewe ni zao la UDSM na umejaa ukilaza.

Heri ungekaa kimya huenda tungejua walio leta hiyo mada walitudanganya. Lakini kwa uzi wako huu, tumesha jiaminisha kwamba UDSM inazalisha vilaza na mmoja wapo ni wewe. Pitia uzi wako ili ujiridhishe jinsi ulivyo kilaza.

Tafadhali usiendelee kujadili mada hii maana utaendelea kutuonyesha ukilaza wako zaidi.
 

Kuna mbwa wa jiran yetu hapa mtaani ni mvivu sana mpk akiskia wengine wanabweka yy anajibu 'me too'
 
Mada inahusu udsm sio Mwigulu. Wakati weka siasa pembeni ujadili mambo ya msng.

Wewe ni mfano wa wale tunaowaita 'wabovu wa akili' taswira ya taasisi yoyote inawakilishwa na nini?? bila shaka ni wadau wake..Mwigulu Nchemba na Juliana Shonza wanawakilisha taswira ya jamii yao,CCM Mahali walipopata elimu e.t.c..mbona hapa unatumia Logic ndogo tu kuelewa?? mbona wewe ni mzito sana?? jibu ni kuwa unasukumwa na ushabiki..toa mawazo ya kujenga uheshimiwe!
 
Jamani mijadala ya ubora wa vyuo inatugawa watz. Ubora wa graduate unategemeana na credibility na uwezo wa mhitimu mwenyewe.
 



Nakipenda sn hiki chuo kwanz wanafunzi wake wanajitambua ndio waliopigania wanafunz kutoka vyuo vingne kuongezewa means test ya mkopo kwa kila mwanafunz japo kuna wanafunz mpaka leo wanabuzana mahakaman na serikali na hv sasa kinashka nafasi ya sita ktk vyuo bora africa ndo kabisa unatoka na GPA tatu lkn elimu ulovuna ni ya kila nyanza bora
 
Mada inahusu udsm sio Mwigulu. Wakati weka siasa pembeni ujadili mambo ya msng.

Bila Mwigulu hii mada isingekuwepo hivyo hapaswi kutenganishwa.Atakayeitetea UDSM na atuambie sababu kwanini maana Mwigulu ni model ya Wasomi wa daraja la juu kutoka pale Chuoni na chochote anachofanya anatoa taaswira ya Chuo husika kilivyo na aina ya wasomi inayowatengeneza,Ni kweli anakiaibisha.Kama alivyosema Dr Slaa logic thinking ya Bw Mwigulu ni duni kweli kwa maana hajui haya anayoyafanya siku moja atapanda Mahakamani sio kwa hiyari bali kwa nguvu akatoe huo ushahidi juu ya hizo tuhuma nzito kabisa,Kingine kinachoonyesha kuwa elimu ya huyu bwana ni utata ni kutokujuwa kwake kuwa tuhuma za namna hiyo licha ya kuingilia kazi za Usalama wa Taifa lakini pia anaivua nguo Usalama wa Taifa na Serikali kwa ujumla kwa namna ilivyoshindwa kuwagundua hao anaowaita watu hatari kwa usalama wa taifa hivyo basi anamaanisha Serikali na Usalama wa Taifa wote dhaifu.Mwigulu is a gift CHADEMA could never have
 

Kaka kumbuka vyuo karibia vyote vimetokana na UDSM mfano sua, muhimbili, ardhi na vingine! Ndio maana nikasema kitengo kimoja ndio kiboreshwe kwasababu kweli hatuna wachumi! Ila kutokana na coz niliyosoma na mafanikio niliyonayo na mchango katika taifa nimkubwa kuliko ukoo wenu ulivyowai kuchangia.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Lazma tukubali kuwa hakuna kinachoushi milele, mm nilisoma UD lkn kwa sasa wahitimu wake hawana ubora, wanazidiwa na vyuo vingine.
Nadhani uliyeanzisha huu mjadala unaonyesha fika ukilaza wa wahitimu wa UD kwa sasa, maana kama msomi unapaswa kutumia usomi wako kuzungumza vitu vya kujenga hasa ktk eneo ulilosomea, nchi yenyewe ndo hii tuionayo jamani, tuwe siriaz na usomi wetu.
Hukwenda chuo ili uwe promoter wa UD, wakitaka wanafunzi watapeleka tangazo kwenye TV, h
 
Wanatumika wapate mradi wao. Inaanza kulipa. habari za kuaminika J.Shonza amezawadiwa Ofisi na Gari, Nini zaidi kwa mtu ambae anatumikia tumbo?

Amepewa yeye kama nani kwenye chama na ni nani kamapa? Mbona wengine ambao ni bora zaidi sana na ni waaminifu wala hawajafukuzwa kwenye vyama vingine hawajapewa?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Tukubali tukatae ukweli ni kwamba wengi bado mnakiadmire chuo kikuu cha Taifa(udsm) sema tuu hamkupata nafasi ya kusoma pale na wengi mnajilaumu na wengine ambao hamjasoma masters hakuna chuo mnachofikiri kwenda kusoma zaid ya udsm unless GPA zenu haziwaruhusu kuingia pale mana kama umesoma chuo kingine ikiwa ili uwe admitted pale kwny GPA yako toa 0.7 ndo utakuwa ufaulu wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…