cold water
JF-Expert Member
- Oct 6, 2021
- 238
- 954
Mimi ni ke mwenye umri wa miaka 25 ,ni mrefu wastani,maji ya kunde/chocolate colour mwembamba wastani ,napenda kuvaa jamani,lakini nikinunua nguo nikianza tu kuivaa sikawii kuichoka,nguo zangu ni za mtumba najua nikienda mtumbani na elfu 50 narudi na nguo nyingi kwa sh 4000_6000 lakini dukani narudi na magauni mawili tu ya sh 25000,je wewe mwanamke mwenzangu au ata mwanaume maana kuna wanaume wako vizuri kwenye fashion wanaweza nishauri pia, je unapenda kununua nguo dukani/mtumbani na vipi utaratibu wako wa kununua nguo upoje? Nguo gani unapenda ziwe nyingi zaidi kati ya skirt,t shirt,na suruali? Wewe unapendelea kuvaa rangi gani zaidi kwaajili ya kupendeza na kuwavutia wengine,na unanunua nguo baada ya mda gani? Karibuni kucomment nipo kusoma comment zenu wapendwa wa jf......