Napenda kuvaa

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
238
Reaction score
954
Mimi ni ke mwenye umri wa miaka 25 ,ni mrefu wastani,maji ya kunde/chocolate colour mwembamba wastani ,napenda kuvaa jamani,lakini nikinunua nguo nikianza tu kuivaa sikawii kuichoka,nguo zangu ni za mtumba najua nikienda mtumbani na elfu 50 narudi na nguo nyingi kwa sh 4000_6000 lakini dukani narudi na magauni mawili tu ya sh 25000,je wewe mwanamke mwenzangu au ata mwanaume maana kuna wanaume wako vizuri kwenye fashion wanaweza nishauri pia, je unapenda kununua nguo dukani/mtumbani na vipi utaratibu wako wa kununua nguo upoje? Nguo gani unapenda ziwe nyingi zaidi kati ya skirt,t shirt,na suruali? Wewe unapendelea kuvaa rangi gani zaidi kwaajili ya kupendeza na kuwavutia wengine,na unanunua nguo baada ya mda gani? Karibuni kucomment nipo kusoma comment zenu wapendwa wa jf......
 

Ombeni sana vijana kabla hamjaoa
 
Mimi mashati,t-shirt na viatu ndo huwa naenda mtumbani lakin suruali lazima nichukue special maana za mtumba ni chache ambazo huwa zinanikaa poa,ni Arusha pekee ndo nilkuwa napata suruali za mtumba zilizokuwa zinanikaa poa,nina matege ya kubonyea kwa ndani ila sio sana maana mademu wangu huwa hawayaoni mpaka akinikasirikia ndo anagundua kuwa huwa nina matege
 
Mkuu

Umejitutumua sana!

Hongera
 
Mtumba kwa Ke ni sawa....ila sishauri Me uvae mamtumba..
Nguo inatakiwa iwe inang' aa flan ivi ndo huwezi kuichoka mapema.
Bora ununue special nyingi hata za laki3 halafu unaanza kuwa unavaa kwa kubadilisha zisijirudie rudie.
Kwahyo mpaka zije zichakae inachukua muda...zikichakaa unaenda tena na laki3 dukani
 
Nipo chuga nipe oda ya sarawili hizo mzee
 
Tupia picha moja humu ukiwa umependeza mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…