Napenda kuwa Mchambuzi wa masuala ya kisiasa

Napenda kuwa Mchambuzi wa masuala ya kisiasa

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
643
Reaction score
845
Habari Zenu wakuu,

Kuna kipindi nilikuwa sipendi kabisa habari za siasa but kutokana na maisha yanavyozidi kwenda nimekuwa nikivutiwa sana na Siasa.

Nimekuwa mfuatiliaji sana wa mambo mbali mbali za kisiasa Tanzania na Nje ya Tanzania.

Napenda kuona jinsi wachambuzi wanavyodadavua mada mbali mbali kwa umakini wa hali ya juu na ustadi mkubwa.

Sasa basi naombeni mnishauri nianzie wapi,na je kuwa mchambuzi wa maswala ya kisiasa yanahitaji elimu kubuwa sana,nifanye nini ili nisibase upande mmoja na niwe nabalance mambo katika uchambuzi wa siasa.

Natanguliza Shukurani zangu za dhati na natarajia majibu yenye mantiki ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwangu.

[HASHTAG]#mckonjetv[/HASHTAG]
 
Ili u-excel kwenye siasa za Bongo, criteria ni 3 tu:

-Uwe mbayuwayu (wazee wa mujini wanaita 'kuusoma upepo')
-Uwe mchumia tumbo (follow the money)
-Uwe muongo muongo.

That's it kwa siasa za kibongo. Otherwise lime light yako itazima asubuhi tu. Bongo mufilisi !

The bottom line is... SIASA ni biashara kama biashara zingine.

-Kaveli-
 
Nilikuwa napenda siasa ila kwa jinsi siasa za bongo zinavo enda sizipendi zaidi.

Lakini kuwa mchambuzi mzuri kwanza si lazima usomee(japo ni vema ungekuwa una elimu ya Political Science)

Pili lazima usiegemee upande wowote, (ushabiki wa kivyama au baadhi ya viongozu acha)

Tatu lazima uchunguze mambo, usipayuke tuu kwa kuwa unahisi ndio mawazo yako sahihi

Nne soma vitabu , soma historia , wasome wana siasa manguli wa zamani, elewa kuwa Historia ndiyo maabara ya uchambuzi wa siasa

*sikiliza wachambuzi wazuri na sikiliza hata wenye bias kwa pande zote za kitu unacho taka kuchambua.

*elewa siasa za bongo nyingi ni ushabiki , ukishangiliwa sana siyo ndo uko sahihi.
 
nenda kasomee course inaitwa Political Science huko kuna mambo mengi utafundishwa kama Political Comparative ambapo utaweza kujifunza siasa za nchi mbalimbali na utajifunza masuala ya politics na government in perspective...
mimi ni political analyst nimesomea political Science..
 
Niliambiwa niwe na pesa kwanzaa, siasa itakupendaa tu.
Vinginevyo ushikwee mkonoo, tena baada ya mapambano mengi, hii yaweza hatarisha maisha yako.
Anyway hiyo avater ni yako? upo verified lkn umekaa kihuni afu unataka kuwa mchambuzi!!!
 
Uchambuzi wa siasa za JF bila kujali unachambua nini jiandae usiwe na nyongo manake unaweza kuitapika yote mpaka upate vichomi
Jukwaa hili wanasiasa wa kubwa wamekimbiaa lkn ukiingia kwenye acc zao unaambiwa last seen a minute ago
Wanachungulia tu.
 
Pili lazima usiegemee uoande wowote, (ushabiki wa kivyama au baadhi ya viongozu acha)

Uchambuzi wa siasa una matawi mengi.Unaweza kuwa mchambuzi wa eneo moja tu mfano Marekani unaweza kutana na mchambuzi wa siasa aliyebobea wa siasa za Republican tu.Anakijua chama ndani nje.Si lazima mchambuzi wa siasa asiegemee kokote anachotakiwa ni kujua kwa undani hicho anachokichambua.Na mara nyingi si rahisi kuwakuta wachambuzi wasioegemea upande wowote sio rahisi kuwapata popote duniani.

Wachambuzi wasioengemea upande wowote mara nyingi huwa ni walimu au maprofesa ambao hufundisha masomo ya political science darasani sio kwenye public.Ukifundisha darasani huwi BIASED lazima usiwe na upande sababu watu wa itikadi zote za kisiasa unakuwa nao darasani.Ni kama kanisani au msikitini ukichambua kitabu cha dini hutakiwi kuegemea upande wa chama chochote cha siasa.

Cha msingi kijue vizuri hicho unachotaka kukichambua kisiasa
 
Chambua soka hata la bongo tafuta uwe msemaji wa Timu huko kwenye siasa utamfata Ken salu wiwa...
 
Anza kwa kumchambua mwanasiasa Mange Kimambi , utapata exposure kubwa sana
 
Nadhani unapaswa kwanza kuwa msomaji wa vitabu mbalimbali vya siasa na historia, pili uwe mfatiliaji wa habari za kitaifa na kimataifa. Zungumzà na wasomi. Epuka uchochezi, Kubali kukosolewa, usiongee kitu bila kutafiti.
 
Niliambiwa niwe na pesa kwanzaa, siasa itakupendaa tu.
Vinginevyo ushikwee mkonoo, tena baada ya mapambano mengi, hii yaweza hatarisha maisha yako.
Anyway hiyo avater ni yako? upo verified lkn umekaa kihuni afu unataka kuwa mchambuzi!!!
Mchambuzi anatakiwa Avae suti Muda wote.? Hiyo Avater ni yangu niliweka 5years ago wakati najiunga Jf. Kuwa verified maana yake me sio Fake na situmii fake names. Asante kwa maoni
 
Nadhani unapaswa kwanza kuwa msomaji wa vitabu mbalimbali vya siasa na historia, pili uwe mfatiliaji wa habari za kitaifa na kimataifa. Zungumzà na wasomi. Epuka uchochezi, Kubali kukosolewa, usiongee kitu bila kutafiti.
Ila nionavyo mimi wale wachambuzi waropokaji ndio wanapendwa zaidi
 
Uchambuzi wa siasa za JF bila kujali unachambua nini jiandae usiwe na nyongo manake unaweza kuitapika yote mpaka upate vichomi
Huwa naona kwenye thread zako bro. kama una roho nyepesi unaweza ukakiuka vigezo na masharti vya jf
 
Habari Zenu wakuu.
Kuna kipindi nilikuwa sipendi kabisa habari za siasa but kutokana na maisha yanavyozidi kwenda nimekuwa nikivutiwa sana na Siasa. Nimekuwa mfuatiliaji sana wa mambo mbali mbali za kisiasa Tanzania na Nje ya Tanzania. Napenda kuona jinsi wachambuzi wanavyodadavua mada mbali mbali kwa umakini wa hali ya juu na ustadi mkubwa.
Sasa basi naombeni mnishauri nianzie wapi,na je kuwa mchambuzi wa maswala ya kisiasa yanahitaji elimu kubuwa sana,nifanye nini ili nisibase upande mmoja na niwe nabalance mambo katika uchambuzi wa siasa.
Natanguliza Shukurani zangu za dhati na natarajia majibu yenye mantiki ambayo yatakuwa msaada mkubwa kwangu.
[HASHTAG]#mckonjetv[/HASHTAG]
Karibu tukufundishe.
 
Back
Top Bottom