Napenda kuwashukuru wote kwa mawazo yenu

Napenda kuwashukuru wote kwa mawazo yenu

Nilikuja hapa kuomba ushauri mwaka jana mkanipa ushauri mzuri sana nikaufanyia kazi mwanzo wa mwaka nikaja kuomba tena ushauri na shukuru sana kwa kunipa tena ushauri napenda kuwashukuru wote kwa ushauri wenu ila shukurani za pekee ziende kwa huyu aliyetoa huu ushauriView attachment 728587kwasababu kupitia huu ushauri niliamua kuufanyia kazi kwanza nilienda maeneo aliyoniambia nilikuta wanaofanya hiyo biashara ni wengi sana na ni kazi sana kupata wateja ikanibidi niende nje ya mji kuangalia vipi hali huko niliona unafuu huko ikabidi mimi nibadili niuze mazima ili niepushe garama kwasababu mtaji wangu ulikuwa mdogo ikabidi nikanunua mbao na misumari nikatengeneza nikanunu mwamvuli nikaelekea pale kirumba sokoni nikanunua matunda mbalimbali na kupeleka kwenye kijiwe chagu nimemuweka hapo dada ananiuzia kwa kweli yanalipa kwakuwa kwa siku sikosi faida ya 10000 paka 20000 nazikusanya ili nitanuwe biashara yangu au nifunguwe kitu kingine nashukuru sana kwa ushauri wenu nimeona siyo mbaya niwaeleze nilipo fika paka sana
Hongera,endelea na moyo huo huo utafika mbali sana...
 
Asante kwa kuleta mrejesho, na hii ndio faida ya JF ingawaje kuna watu hawataki kuiona ikiwa hai. Cha muhimu ni kuwa na nidhamu ya matumizi maana tayari una nidhamu ya mapato.
 
Asante kwa kuleta mrejesho, na hii ndio faida ya JF ingawaje kuna watu hawataki kuiona ikiwa hai. Cha muhimu ni kuwa na nidhamu ya matumizi maana tayari una nidhamu ya mapato.
Mkuu nidhamu ipo ya hali ya juu sana
 
Back
Top Bottom