Napenda/navutiwa kusikiliza vipindi vya michezo pindi timu yangu inaposhinda

Napenda/navutiwa kusikiliza vipindi vya michezo pindi timu yangu inaposhinda

Clark boots

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
6,770
Reaction score
6,202
Yaan kiukweli, napenda na kivutiwa sana kusikiliza vipindi vya michezo pindi timu yangu inaposhinda..
Hii hutokana na furaha ninayokuwa nayo baada ya kushinda, mfano Leo Yanga yangu imeshinda huwa nashauku sana ya kusikiliza vipindi vya michezo kwenye radio mbalimbali wakati huu wa usiku..

Ila siku mambo yakiwa ovyo, kama ile majuzi tulivyofungwa na Mikia Sc, yaan nilizila vipindi vyote vya michezo radion siku ile maana naona huwa vinanikumbusha machungu tu..
Vipi kiupande wao ww mdau(chama lolote lile)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakweli atakei kupinga basi analo jambo
Hongera DAR YOUNG AFRICAN nimefurahi sana leo.

[emoji375][emoji375]
Tangu Al Ahly afungwe hapa bongo Simba imewakosesha raha sana.
Pole ndio mpira.
Nilikuwa CCM Kirumba leo kwakweli mashabiki wa Yanga wamefurahi sana mbali na kushinda ni kwamba hamjawahi kushinda mbele ya Mbao hapa Mwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni kawaida, mfano Jumamosi tulivyowakalisha Yanga, nilisikia EFM saa 1, saa 2 Magic FM, saa 3 Clouds, kesho yake saa 12 asubuhi BBC, saa 7 mchana Jumapili Clouds, yaani ilikuwa burdani sana.
 
Back
Top Bottom