Napenda sana Utangazaji wa Habari wa Mtangazaji Harris Kapiga wa Clouds tv

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
  1. Anatangaza huku anatabasamu na sometime anacheka cheka
  2. Anatangaza huku kila mara akiwa anachezea chezea Kalamu yake
  3. Anatangaza huku kila mara akiwa ' anachomekea ' maneno yasiyoendana na Habari husika
  4. Anatangaza huku sometimes akiwa ' anatuhubiria ' pengine akijua wengi wetu ' tunaomkodolea ' tuna dhambi za ' Kutukuka '.
  5. Anatangaza huku mara zingine akitupa ushauri nasaha
  6. Anatangaza huku mara zingine ' anatubinyia ' macho ' Watazamaji ' wake hali ambayo kiukweli hutuvitia sana hasa sisi ' Watazamaji ' wake wa Kiume.
  7. Anatangaza huku mara nyingi akiwasifu mno wale waliopo ' Madarakani ' wa Lumumba street na kuwaponda wale wa ' Biafra ' street.
Hongera sana Mtangazaji Harris Kapiga na ' Binafsi ' huwa unanivutia sana na endelea hivyo hivyo Mtu wangu kwani unapatia na upo vizuri kuliko Watangazaji wote ninaowajua ' duniani '. Pia pongezi kubwa ziende kwa Uongozi mzima wa CMG ( Clouds Media Group ) kwa kuwa ' Wabunifu ' na kutuletea huyu ' Mtangazi ' ambaye naamini mpaka sasa lazima tu atakuwa amewavutia wengi kutazama taarifa zenu za Habari.

Niwaombe tu ' Watangazaji ' wengine wote wa ' Luninga ' nchini Tanzania muweze ' Kumuiga ' huyu ' Mtangazaji ' mwenzenu Harris Kapiga.

Nawasilisha.
 
Umesahau sifa moja,kila kitu anakijua yeye
 
Ananiachaga hoi tu anapoanza kutupa mikono hewani,halafu anasoma kwa kukatakata Sana maandishi, hadi habari inakosa mvuto, klauzi wanatufanyia makisudi tu, mbona kuna wale madada wanaflow vizur tu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…