Tatizo wanawake huwa mmeshindwa kutafsiri uhalisia,ulefu au ufupi haulei au kumjari Mke.
Tabia njema ndiyo nguzo ya mume bora.
Wengi huwa mnaendelea kuzeeka bila kuolewa kwa kusubiri wanaume walefu,weupe ukishtuka una umri wa miaka 35 alafu hujampata mwanamume mlefu,mweupe.
Baada ya umri kupita mnaanza kujaza makanisa kwa wachungaji eti mnatafuta mume wa kuwaoa,wakati huo sasa wanaume wanakukimbia.Kwani mwanaume huwa anajiuliza miaka yote uliyonayo hadi karibu unazeeka hujaolewa lazima utakuwa na matatizo tu,kumbe wewe ulikuwa unatafuta mwanamume mlefu,maji ya kunde,ana mwili umejaa jaa kidogo,anasauti nzuri.Imeshakura kwako huwa mnaishia kuzalishwa tu kisha mnaendelea kulea watoto wasio na baba.