Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Sijui heading ipo sawa au laa ila ninachokusudia ni zile process za kuvutia umeme majumbani. Huwa sipendi kubahatisha nikauliza mtu wa TANESCO kuhusu umeme nikaambiwa cha kwanza piga wiring ndipo ujaze fomu. Nimejaza fomu online napiga simu TANESCO huduma kwa wateja nijue hatua inayofuata naambiwa nitafute contractor afanye hatua inayofuata nikiuliza nampata wapi kwanini nisisaidiwe kumpata najibiwa eti TANESCO haina mamlaka hayo nilichoka.
Mungu mkubwa nikasema siulizi mtu nikakorokocha kwenye limfumo lao mpaka nikaona sehemu kumbe wameorodheshwa makontractor wote kwa kila mji na namba zao za simu (nikawaza moyoni hivi walishindwa hata kuniambia kwamba hawa watu wanapatikana huku?). Nikachukua namba nikamcheki mshikaji yuko very humble akakamilisha kila kitu. Eti akikamilisha TANESCO tena wanatuma surveyor kwa ajili ya kuja kuhakiki ili aidhinishe upate control namba ya kulipia mita
Sasa mzunguko wote huo wa nini, kwanini kusiwe na gharama tu fulani mtu atoe ofisini kisha mambo yote mmalize TANESCO? Maana hao makontractor, mafundi wa wiring kila mmoja anakuwa na taratibu zake hivyo unakuta kuna wanaoumia zaidi katika wateja wenu. Yaani ilivyo sasa ni kwamba hakuna gharama maalumu kwenye wiring wala kwa contractor bali itategemea maongezi ya mteja, hii siyo sahihi
Umeme ni swala nyeti mno inabidi lisimamiwe ipasavyo siyo hivi ilivyo sasa hitilafu imetokea eti TANESCO haihusiki nikamtafute fundi aliyepiga wiring mara mtu kajaza fomu eti akatafute mkandarasi yeye mwenyewe sasa anaanzia wapi? Ndiyo maana wafanyakazi wa TANESCO wametugeuza ni fursa/dili watu wa vijijini tukitaka kuvutia umeme wanafanya kunyang'anyana wateja. Halafu kuna kitu nikahisi labda ndiyo sababu ya mimi kupata usumbufu vile
Kitu chenyewe ni hiki... huyo surveyor alipokuja aliidhinisha lakini muingiza umeme alisema hafungi waya eti maana nyumba fupi mno inabidi mpaka nitafute chuma kuongeza urefu, basi nikainama kama sekunde kadhaa haraka haraka nikaibuka na wazo mujarabu kabisa; nilimwambia tuvute waya mpaka pale juu kwenye sambusa ya nyumba (juu kwenye msonge) kisha uunganishie kule na uzuri fundi mpiga wiring tulikuwa naye muda huo. Jamaa akasema hilo halina shida linawezekana lakini akatamka "YAANI WALIMU WAJUAJI HATARI, KILA NYUMBA YA MWALIMU TULIYOFANYA KAZI LAZIMA TUKUTANE NA UJUAJI MWINGI" kisha sote tukabaki kucheka
Kwahiyo hapo unaona shida hiyo na ajabu ni kwamba kila anayekuja lazima akosoe hatua ya nyuma yake sasa kwa nini ofisi isiweke utaratibu wa kusimamia kila kitu ili ijikosoe yenyewe?