Napendekeza mikopo yote inayokopwa na serikali itumike kulipa madeni, na makusanyo yote ya Kodi yatumike kwenye bajeti

Napendekeza mikopo yote inayokopwa na serikali itumike kulipa madeni, na makusanyo yote ya Kodi yatumike kwenye bajeti

I have many ideas mkuu tatizo ni hela ndio changamoto and no body believe in us when we have nothing that's problem mkuu we have to prove ourselves
yah mkuu, mkuu itabid tuwe washikaji contacts zihusike , naona tuko uelekeo mmoja mkuu🙏
 
Namna pekee itayoweza kutuamsha kama nchi toka usingizini ni kujiuliza maswali kadhaa…

1.) Tanganyika inakopa jumla ya Trillion ngapi kwa mwaka?

2.) Tanganyika inalipa madeni Trillion ngapi kwa mwaka?

3.) Tanganyika inakusanya mapato ya ndani Trillion ngapi kwa mwaka?

Majibu

1.) Tangu 2021 hadi 2024 tunaambiwa deni limepanda toka Trillion 70 enzi za Ndugai hadi Trillion 100 katika kipindi hiki cha Chura kiziwi, ukigawanya unapata tunakopa wastani wa Trillion 10 kwa mwaka.

2.) Ulipaji wetu wa madeni ya nje, kwa taarifa tunazopewa huko bungeni, ni kwamba tunalipa Trillion 12 kama marejesho ya madeni na Riba kila mwaka.

3.) Makusanyo tunayoambiwa ya TRA pamoja na wengine ni wastani wa Trillion 2 kwa mwezi, Hivyo ni kama Trillion 24 kwa mwaka. Hivyo nusu ya makusanyo yanenda kulipa madeni.

Sasa najiuliza, au tuseme napendekeza. Kwakuwa tunacholipa kwa mwaka ni zaidi ya tunachokopa, ni kwanini basi Trillion zote 10 tunazokopa kwa mwaka zisibakie tu huko huko, zisije kwetu, halafu tuwe tunalipa tu Trillion 2 kwa mwaka kama riba ya madeni ambayo tulishachukuwa?

Maana ubaya wa kuendelea kutupa hiyo mikopo mipya mikononi mwetu, halafu ndio tuwarudishie kama malipo ya mikopo ya nyuma, ni wizi mkubwa wa watendaji wa serikali, ambapo hiyo mikopo kwa asilimia kubwa inaishia kwenye mifuko ya mafisadi serikalini, na kusababisha deni kupaa wakati hatujanufaika chochote na hiyo mikopo, na mwishowe tunakamuliwa kodi kuilipa, hivyo isipitie mikononi mwetu, wabaki nazo tu huko huko tuwe ndio kama tumelipa

Hivyo basi, waache kutukopesha, maana makusanyo yetu pekee yanatosha endapo tusingekuwa tunalipa mikopo. Kwahiyo basi Tanganyika isipewe mikopo, bali hiyo mikopo wabaki nayo moja kwa moja, na sisi tutalipa Trillion 2 tu kila mwaka kama riba, hadi deni litakapoisha.

IKUMBUKWE, NI RAHISI KUIBA MKOPO KULIKO KUIBA MAKUSANYO. MKOPO UNAWEZA KUSAINI NA HATA KULETWA USILETWE, LAKINI KWENYE BAJETI TUKAANZA KUKATWA PESA KULIPA MKOPO HEWA!

Inshort Tanganyika, kama ilivyo nchi nyingi za Afrika, tumegeuzwa ng’ombe wa maziwa, tunalishwa debe moja la pumba ambayo inauzwa alfu 3, halafu tunakamulishwa maziwa ndoo 2 zenye thamani ya elfu 30, kisha tunashukuru aliyetupa msaada wa pumba. Mwingulu hebu fanya hivi utukwamue kwenye huu mtego, kuweni wazalendo, kuweni na huruma na binadamu wenzenu, mnashirikiana na mabeoari kutukamua kikatili, tutakamuliwa hivi hadi lini?!
Kwa tafsiri yako unamaanisha wasikope kabisa?

Au wakope sehemu nyingine ili walipe madeni yaliyopo, yaani wahamishe madeni?
Kwakuwa wanatukopesha ni wale wale, IFM, World Bank.., basi hizo pesa wabaki nazo maana wakitupatia immediately tunawarudishia, sasa badala ya kutupa wabaki nazo, wawe wametukopesha ila bila kutupatia hizo pesa, kazi yetu sisi ni kulipa riba tu. Maana wakitupa tia zinaaemda matumboni mwa watu na deni linazidi kuongezeka badala ya kupungua..
Shida ni kwamba tunazungusha madeni.

Bila kuchukua hizo pesa hutoona barabara, madaraja, hospitali, Wala mradi mkubwa wowote
 
Sasa kuliko ukope Ili kulipa mkopo uliopita, Si Bora usikope kabisa!!

Mkopo unatakiwa itumike kuzalisha faida kuongeza mtaji,Kisha utumie faida kulipa mkopo.

Mbeleni lazima Mwigu atakwama Kwa sera hizi.

Tusubiri!!
 
Sasa kuliko ukope Ili kulipa mkopo uliopita, Si Bora usikope kabisa!!

Mkopo unatakiwa itumike kuzalisha faida kuongeza mtaji,Kisha utumie faida kulipa mkopo.

Mbeleni lazima Mwigu atakwama Kwa sera hizi.

Tusubiri!!
Kinachofanyika sasa ni kwamba tunakopa ili kulipa madeni, maana tunakopa Trillion 10 kwa mwaka, na tunalioa Trillion 12 kwa mwaka, tafsiri yake ni hiyo, tunakopa kulipa madeni. Hivyo ni bora hiyi mikopo ibaki huko huko ijilipe yenyewe, sisi tulioe riba tu.., maana wakitupatia zinaishia mifukoni mwa watu tu na kupaisha deni..
 
Tunakopa Trillion 10 kwa mwaka na kulipa Trillion 12 papo hapo. Akili zetu zipo makalioni?
 
 
Back
Top Bottom