Napendekeza namba moja ya wakala kwa mitandao yote ya simu

Naona watu wanaiba innovation hapa 😂😂, natania bhana
4D8DD390-A31A-40F2-A56F-EB4A832F1332.jpeg
 
Yaani badala ya wakala kubandika namba za kutolea pesa za mitandao tofauti tofauti, aweke namba moja tu ya wakala na wateja wenye line za mitandao yote waweze kutoa pesa kwa kutumia namba hiyo hiyo moja, halafu wenye mitandao watagawana wenyewe pesa huko kwa kutumia automatic system watakayojiwekea.

Inakera sana unataka kutoa pesa Tigo halafu wakala anakwambia labda utoa Voda, Tigo sina float. Au unataka kuwe pesa Airtel halafu wakala anakwambia labda weka Tigo, Airtel sina float, inakera sana.

Ni kama mabenki yalivyofanya kwa kutumia ATM za UMOJA ambapo mteja wa benki yeyote ile iliyounganishwa na UMOJA ATMs anaweza kwenda kutoa pesa kwenye ATM hizo halafu wao wanapigiana hesabu wao kwa wao automatically na kusettle accounts, hii imesaidia sana maana ingebidi kila benki iweke ATM yake kila kona ya nchi kitu ambacho kingekuwa ni ghali sana.

Hivi nimeeleweka kweli?
================================
Update: 19/06/2020
View attachment 1483235
Hiyo line utakuwa ya kampuni gani?? Au ya serikali?!
 
Unazifahamu ATM za umoja ambazo zinatumika na wateja wa bank nyingi tofauti kama DCB, Twiga nk; zinamilikiwa na nani? Au ATM zilizounganishwa na Mastercard na Visa ambapo wateja wa benki yeyote kutoka nchi yeyote wantumia ATM hiyo hiyo kutoa pesa, zinamilikiwa na nani?
 
Update: 26/10/2022
Tigo na Zantel wameanza kutumia namba moja ya uwakala, mitandao mingine ya simu kujiunga hivi punde.
 
Yaani badala ya wakala kubandika namba za kutolea pesa za mitandao tofauti tofauti, aweke namba moja tu ya wakala na wateja wenye line za mitandao yote waweze kutoa pesa kwa kutumia namba hiyo hiyo moja, halafu wenye mitandao watagawana wenyewe pesa huko kwa kutumia automatic system watakayojiwekea.

Inakera sana unataka kutoa pesa Tigo halafu wakala anakwambia labda utoa Voda, Tigo sina float. Au unataka kuwe pesa Airtel halafu wakala anakwambia labda weka Tigo, Airtel sina float, inakera sana.

Ni kama mabenki yalivyofanya kwa kutumia ATM za UMOJA ambapo mteja wa benki yeyote ile iliyounganishwa na UMOJA ATMs anaweza kwenda kutoa pesa kwenye ATM hizo halafu wao wanapigiana hesabu wao kwa wao automatically na kusettle accounts, hii imesaidia sana maana ingebidi kila benki iweke ATM yake kila kona ya nchi kitu ambacho kingekuwa ni ghali sana.

Hivi nimeeleweka kweli?
================================
Update: 19/06/2020
View attachment 1483235

==========================
Update: 26/10/2022
Tigo na Zantel wameanza kutumia namba moja ya uwakala, mitandao mingine ya simu kujiunga hivi punde.
Hili ni jepesi kama ambavyo umejaribu kulishauri unafikiri?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Tigo na Zantel wameshaanza kwa mafanikio makubwa sana, wanatumia namba moja ya uwakala kwa wateja wao wa Tigo na Zantel. Wateja wa Zantel wamenufaika zaidi, maana sasa wanatoa pesa hata kwa mawakala wa Tigo pesa.
 
Kilichotokea kwa Zantel na tigo sio hiki unachokiongelea, Zantel imenunuliwa jumla na tigo ,so kwa kifupi sahv hakuna zantel tena,

Watu wanachanganya mambo, Zantel haijaungana na tigo, Zantel imeuzwa kwa tigo
 
Haijalishi mbinu iliyotokea, ila wateja wa Zantel wamenufaika
 
Back
Top Bottom