Napendekeza idara ya TRA ingekuwa inatoa nishani kwa wafanyabiashara ambao wamefanikiwa kukua kwa viwango ambavyo wataviweka wao. Iwe wafanyabiashara wakubwa, wakati na wadogo. Wahojiwe waweze kueleza mbinu walizotumia kukua ili kuhamasisha kwanza ulipaji kodi pili kuhamasisha wafanyabiashara wengine kujifunza mbinu za wenzao pamoja na kuleta ushindani. Ikiwezekana raisi ndio atoe nushani hizo.