<br /><font size="4"><i>Wanawake ambao wanafikiria zaidi mambo ya kisheria kuolewa kwao kulivutwa na "material things" na hivyo anataka kugawia utajiri wa mumewe. Mimi nilifikiri kama kweli ulipenda kuolewa bila kusukumwa na kitu chochote linapotokea tatizo kwenye ndoa shauri litapelekwa kwa msimamizi wa ndoa, baadaye kwa wazazi. Huwezi kufikiria maswala ya kisheria wakati bado mnaishi nyumba moja. </i></font>
Pole sana Unlucky ila pls allow me nikuite Lucky,sababu umeshajua adui unayepambana naye anatumia silaha za namna gani,kama unapenda uendelee na ndoa yako liko tumaini nipm nikupe mistari na shuhuda za kwenye bible haitakuacha,na mumeo hajui ni kiasi gani anataka kujiharibia future yake kwa kwenda kuoa mtu mwingine Neno la Mungu linasema USIMTENDEE KWA HIYANA MKE WA UJANA WAKO,PIA - NINYI WAUME WAPENDENI WAKE ZENU MSIWE NA UCHUNGU NAO.Stay blessed
asanteni na hili jina nilijipa mda sana wakati yote yalinitokea nimevumilia mengi mpaka malaya zake wamnitukana lakini bado nimestahamili yote mpaka leo hii sina chochote kaniweka ndani tu ananipa hizo hela kidogo tu za mimi kununua vitu vyangu kama sabuni n.k pamoja na pampers za watoto mpaka leo hii sina akiba yoyote naomba mniambie hiyo talwa iko sehemu gani na je watanisaidia siyo kunizungusha ne je hawatataka pesa,huyu bwana ana pesa sana je nikifight nae na akaja kuwapa rushwa hao watu si watanigeuzia kibao ? Halafu huyu bwana ni foregner anaishi kwa permit hapa je nikienda imgration office itakuwa sawa?na talaka nataka nipate je niende wapi?
Wewe hiyo miezi ya maandalizi sijui ya kumsubiri mwanao akue ndo ifanyie kazi, kama unajua hati ya nyumba ilipo (kama mna nyumba) ichukue kafiche kokote unakijua, na jipange hata siku akitoka kazini akute ushaleta fuso na kumwachia nyumba nyeupe. Kaanze upya for the sake of your kids..wala usiogope. Ni maamuzi magumu lakini inabidi kuyafanya ili kutunza utu wako kama mwanamke na pia kwa ajili ya watoto wako, yeye hana cha kupoteza. pm for more information kama uko tayari kufanya maamuzi magumu. Its time wanawake tuache kulalamika na kujisimamia maana hapo ndoa yako ilipofikia haina cha kuomba Mungu wala kuvumilia, You need to live for your kids maana atakuja kukuua na wanao wakabaki hawana mzazi maana yeye akishaoa tena ndo kwisha habari yao. pole.
jamani hata hizo nguo nimeshaambiwa nikikutoa hapa unaacha kila kitu mpaka chupi coz yote kabuy yeye siyo changu niondoke mtupu,hata mimi naona nisonge mbele wala nisihangaike uko kote ya nini yote mungu atanilipia mie nafikiria watoto niwachukue kimya niondoke coz mtu kama huyu ukishindana nae nita taabika sana dah
habari zenu wapendwa nadhani mlisoma story yangu yote na mume wangu haya sasa imefikia siku tena huyu bwana kanitafutia sababu eti hawezi kuishi na mimi kisa alinipiga wakati na mimba miezi nane nikaenda polisi lakini hakutiwa mbaroni leo ananitolea sababu hiyo kama umenivunja moyo sina mapenzi tena na wewe kisa hiyo sababu ya kwenda polisi watoto anataka kuwachukua anasubiri mtoto wangu wa miezi minne awe miezi 10 ndo anipe hiyo talaka,sasa jana binamu yake kaniambia kama huyu bwana anataka kuoa ndo mana wewe anakutafutia sababu dah roho inaniuma sana nimeteseka miaka sita hamna mapenzi nimechuma nae alikuwa maskini leo katajirika sasa anaenda kumuoa malaya anaedance clubs jamani naomba mnishauri niende wapi serekalini anipe jasho langu na hawa watoto pia nipate mimi na pia nataka huyu mtu atolewe kabisa hapa dar asiishi tena yani nimkomoe haswa kanitesa sana nimehangaika sana nae mpaka leo ana uwezo naomba mnisaidie dada judith upo
<br /><font size="4"><i>Mwanamke mwenye uwezo wa kuingia huku JF na kuchangia michango kupewa talaka si kuonewa lazima utakuwa umeshindikana. Wa kuonewa huruma ni wale wamama wa nyumbani wasiojua hili wala lile zaidi ya kuhudumia familia yake siku 365 bila kuchoka</i></font>
<br />
<br />
sasa akionewa asitafte msaada wa sheria kisa atasemwa. haiwezekani mtu ageuke mtumwa kisa mfume dume.
Mwanamke mwenye uwezo wa kuingia huku JF na kuchangia michango kupewa talaka si kuonewa lazima utakuwa umeshindikana. Wa kuonewa huruma ni wale wamama wa nyumbani wasiojua hili wala lile zaidi ya kuhudumia familia yake siku 365 bila kuchoka
Mimi haya mambo ya sheria nilikuwa siyaelewi, nahisi umepewa ushauri mzuri.pole kwa matatizo yote yaliyojitokeza na hongera kwa kuweza kuvumilia
suala la talaka kabla ya kufika mahakamani inatakiwa ipitie sehemu 2 hadi 3 na sehemu zote hizo kuwepo na maandishi na mwafaka au kutokuwa na mwafakakatika ufunguzi wa kesi hakikisha unaorodhesha asset mlizochuma kwa ajili ya mgao na kama kuna vitu vya kutoa kopi toa na hata picha ya vitu mbali mbali
- anzia serikali za mitaa (si lazima sana )
- ustawi wa jamii baada ya hapa wataipeleka
- baraza la usuluhishi wa ndoa then
- mahakamani (ni vyema ukatumia mahakama ya wilaya ili uweze kuweka wakili wa kukusimamia sheria)
Mkuu, unataka kusema mwanamume ana haki ya kumpiga mke wake? Hivi tunaishi katika karne gani?Ndachuwa.
Tangu mwanzo niliposoma post ya kwanza hadi ya tano nimegundua huyu Unlucky ndiye mwenye matatizo tena makubwa kuliko tunavyofikiri yamkini tunampa pole kwasababu hatujapata story upande wa pili.
Unlucky anadai alipigwa alipokuwa na mimba ya miezi minne lakini hajatuambia sababu za kupigwa zaidi ya kujitetea Bwana hakutiwa ndani na polisi hataki kutuambia kwanini polisi walikataa kumweka ndani mumewe.Napata hisia polisi waliona Unlucky ni mkorofi,mjinga kashindwa kumtii mumewe na nk.