Pole sana dada yangu kwa yote uliyokutana nayo, muhimu tu kuwa mjasiri sana tena sana.
Unajua mwanamke unapoolewa unapaswa kuwa na msimamo, bila hivyo utanyanyasika sana dada yangu, na ninaomba ujifunze kuwa na msimamo mbele ya mwanaume sio huyo tu hata kesho na keshokutwa utakapokuwa umeolewa kwingine,
nakupa good example, Mie nimeolewa na ni mama wa watoto wawili, mume wangu anafanya kazi nani nafanya kazi, kabla hatujafunga ndoa alinikuta nina kila kitu mpaka mashuka ya kulalia hajanunua mpaka leo tunatumia niliyonunua mimi, Ok nilimpenda sana hivyo mali sikuona kama ni kigezo cha yeye kutonioa, akaenda kwa wazazi akatoa mahari tukafunga ndoa, baada ya mwaka mmoja na nusu akaja mdogo wangu akiitaji msaada wa karo, nami nikamuahidi kumsaidia pindi tu nitakapopokea mshahara, Mume wangu akaja juu akaupangia majukumu mshahara wote hata kabla sijaupokea, na kuniambia kuwa ukimpa mdogo wako karo nakupa talaka, inabidi unisikilize mie na sio wazazi wako tena na ndugu zako, zogo likawa zogo ndani ya nyumba, siku tatu hakuna maelewano, nikaona sasa huu ni utumwa, nikamwita na kumweka chini nikamwambia wewe una nafasi yako kama mume wangu, na mdogo wangu ana nafasi yake kama mdogo wangu naomba talaka yangu leo tuachane na pesa hii hapa namtumia sasa hivi karo huku pesa nikiwa nimeshika mkononi,m mwanaume hakujibu nikatuma hile pesa hapo hapo nikajiandaa kwa hiyo talaka, kwa sababu nilijua mwisho wa hili ndio mwanzo wa hilo, Mwanaume hakusema chochote kwa muda wa siku mbili, siku ya tatu akachangamka na kunijali kama vile sio yeye aliyeleta upuuzi mwanzoni na maisha yakasonga.
Nimekupa mfano huo wewe kama mwanamke naomba ujiamini, usijidharau, usilie sana, waswahili wanasema kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa ..................!! Chonde chonde simama imara mama, mpaka mnafikishana police mapenzi hamna tena omba talaka yako, nenda kwenye vyombo vya sheria dai haki yako, tena ndio mkimbizi wala asikubabaishe hata kidogo, kama hauna kazi hata biashara halali utafanya mama utanunza watoto wako na watakusaidia mbeleni. Nimeandika kwa uchungu sana na hilo jina hapo badilisha kama ulivyoambiwa na waungwana, nakutakia kila rakheri Muhimu kuwa na msimamo.