wengi jamaa wananiambia wanipeleke kwa mganga arogwe niokoe ndoa yangu mie siamini vitu hivi hapa dar hamna mganga na kama yupo mbona tunataabika
Mkuu, unataka kusema mwanamume ana haki ya kumpiga mke wake? Hivi tunaishi katika karne gani?
Hata kama Unlucky ana makosa na ukorofi, mume hana haki ya kumpiga, hana haki.
hawezi kukunyangnya mali zote pigania haki yako waone TAWLA watakusaidia sana tena inwezekana huyu mmeo akabaki hana kitu kabisa.pigana mama usikate tamaa.
jamani hizi ndoa lol pole mpendwa wangu ,yaani huyu mmeo anakutafutia visababu visivyo na kichwa wala miguu mradi tu muachane,umejaribu kuwashilikisha wazazi wake? umejaribu kuomba msaada kwa washauri wa ndoa yenu na je umejaribu kuomba msaada wa kikanisa ?
wapendwa mie mbona sikumpeleka polisi nilimshtaki tu halafu na kesi nimerudisha na siwezi kusahau na miezi minane mimba kanipiga teke la nyuma mpaka mkojo ulitoka alinipiga mangumi mateke mdomo ulitutumka kama umetiwa hamira mpaka leo hii sowezi kukaa sana kama kanitia ubovu je angemuua huyu mtoto au mimi je?na hapa hana ndugu yeyote wala mzazi wote wako huko kwao ndo mana yuko huru
Wewe hiyo miezi ya maandalizi sijui ya kumsubiri mwanao akue ndo ifanyie kazi, kama unajua hati ya nyumba ilipo (kama mna nyumba) ichukue kafiche kokote unakijua, na jipange hata siku akitoka kazini akute ushaleta fuso na kumwachia nyumba nyeupe. Kaanze upya for the sake of your kids..wala usiogope. Ni maamuzi magumu lakini inabidi kuyafanya ili kutunza utu wako kama mwanamke na pia kwa ajili ya watoto wako, yeye hana cha kupoteza. pm for more information kama uko tayari kufanya maamuzi magumu. Its time wanawake tuache kulalamika na kujisimamia maana hapo ndoa yako ilipofikia haina cha kuomba Mungu wala kuvumilia, You need to live for your kids maana atakuja kukuua na wanao wakabaki hawana mzazi maana yeye akishaoa tena ndo kwisha habari yao. pole.
Mhh Carmel, mbona kama unataka ajilipue... naona kama kuna muda hapo wamekubaliana mpaka miezi kumi mtoto akue, kwanini asiangalie namna ya kutatua huu mgogoro kwa kipindi hiki, kabla ya kuagiza fuso na kuiba hati? hatari sana ushauri wako...
<br />hana hati wala nyumba na mie sitaki chochote nanyanyasika sana leo ya tatu tena haongei na mimi mtoto akikosa adabu mama lazima ampige je hilo kosa?<br />
Basi leo nimempiga mtoto hataki kwenda shule hataki kuvaa ukaidi ujeuri nikampiga kibao baba mtu kanisukuma kataka kunipiga hivi haki?