Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Huyo makalla kama ameamua hivyo basi ajue kwamba tunaoteseka ni sisi abiria....siku zote mtu kama hajapitia shida hapo nyuma, basi hawezi fikiria ya wengine...


Nashauri afanye hivi;
1 Uwepo usafiri wa bure wa kututoa mbezi hadi mjini/Urafiki
2 Viwepo vituo ama ofisi za mabasi mfano; Temeke, kariakoo, mbagala, kinondoni, kigamboni n.k ili iwe rahisi kupandia hayo maeneo na kutufikisha stand.....
 
Ni mjinga yule he will never think of solutions to people's problems as he has never been part of it before, mtatuzi mzuri wa changamoto ni yule aliyezipitia
 
Kuna waliowahi kugoma kuhamishwa iliyokuwa stendi ya Kisutu.

Kila mtu ni mjuaji kama wewe! Hebu tuliza...
 
Sisi wenzenu tulilia sana taratibu kama hiyo huku SONGEA lakini hadi leo kimya
 
huyu MAKALA atakuwa mkuu wa mkoa alietumikia muda mfupi sana Dar es Salaam.

yaani naishi Tabata kuna option ya kushushiwa Ubungo unanilazimisha nishushiwe huko porini Mbezi ili iweje?
 
Kuna vitu lazma serikali iache kuwekeza na ibaki kuwa mwangalizi tu na kudai mapato. Masoko na stand za mabasi iachwe kwa private.
Alichofanya RC ni ujinga wa kutotafiti uhalisia. Hakuna faida yoyote kulazimisha mabasi kupita au kushusha na kupakia tu Mbezi. Kiu jumla ni mateso.
 
Huyu alikaa bench muda mrefu sana. Amesha sahau kazi zina fanyikaje. Hapo amekurupuka 100%. Asipo angalia ana rudishwa bench faster.
 
Hili lipo kwa maslahi yake binafsi
 
Huyu alikaa bench muda mrefu sana. Amesha sahau kazi zina fanyikaje. Hapo amekurupuka 100%. Asipo angalia ana rudishwa bench faster.
Vyombo vya habari vinatakiwa kusaidia wananchi kupaza sauti kulipigania hili, ni unyanyasaji mbaya sana kuwahi kutokea, vinginenyo hatutamuelewa Rais akilifumbia masikio jambo hili
 
Mimi naona RC yupo sawa tu kwa maana halisi ya kuwa na stand ya mkoa. Haitakuwa na maana kama kila mmiliki wa mabasi awe na stand yake, hata hivyo ikumbukwe ile investment iliyowekwa pale na serikali inahitaji return japo kuwa ni huduma kwa wananchi. Sasa return itarudi vipi ikiwa lengo halifikiwi kwa sababu ya uchache wa abiria
 
Yaani stend ya ndege ilifaa iwe nje ya mji huko, hata kibaha kabisa alafu stend ya abiria iwe kipawa,nasema uongo ndg zangu?
Makalla agizo lake halitkelezeki naona anaanza kukurupuka kidogokigo km bashite.
 
Ipo siku mtataka abiria wa ndege wanaoishi Bagamoyo ndege ziwe na kituo
 
There must be rule of the game...
 
Sasa return itarudi vipi ikiwa lengo halifikiwi kwa sababu ya uchache wa abiria
Huwezi kufanya return kwa kuwaumiza wananchi tena kwa kuwabaka, think outside the box, na ndiyo tafsiri ya kiongozi, waondolee watu kero ili kuwaongezea ufanisi na siyo kuwajengea mazingira magumu ili waumie nawe unufaike kupitia maumivu yao, kiongozi ni problem solver siyo problem creator
 
Huyu mkuu wa mkoa amecopy upuuzi wa Dodoma,
Dodoma Kuna amri basi lolote hata lifike saa 8 usiku Dodoma,lazima lishushe abiria wote stand kuu,hakuna kuwapa msaada abiria wanaoenda mjini Kati Kati,basi lishushe,harafu liende tupu mjini kupaki,
Kisa wanataka abiria wanaoenda mjini,watumie usafiri mwingine wa boda boda,teksi,lengo ilikuwa ni kulazimisha abiria wapande boda boda,teksi kwenda mjini
Dodoma daladala mwisho saa nne usiku,unafika Dodoma saa Saba usiku,uchukue boda boda mpaka mjini,ulipe Tena 15000!akili za hovyo kabisa
 
Mkuu ameumiza watu kwa namna gani hapo? hebu nieleweshe kidogo.
 
Waondoe machinga na wapiga debe

Watu wanafata huduma nzuri ndo maana mabasi yanatengeneza stend zao ili abiria wakwepe usumbufu waupatao mbezi
 
Hapo kwenye FM Academia umegusa penyewe, namshauri awalete ngwasuma kiupya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…