Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Mtu anatoa kauli hii bila kutoa takwimu za vifo au ajali za miezi mingine huku akilinganisha na Desemba.
Kwakuwa watu wengi wako likizo basi habari husambaa haraka na kwa wingi. Tukio moja likitokea hupambwa kwenye media zote.
Pia ili upige hesabu sawia ya takwimu ya ajali barabarani usisahau kupiga hesabu ya magari yanayofanya movement katika hiyo barabara.
Kama mwezi April barabara ya Dar - Arusha kwa siku hupita magari 1000, ajali 4-7 . December kama yanapita magari 2500 kwa siku ajali zikiwa 7- 13 hapo ukimwona mtu anakesha kanisani kufunga roho ya ajali basi akili yake si timamu.
Hii ni sawa na kusema shule hii siku hizi inafaulisha sana. Ukiangalia waliofaulu kwenda kidato cha 5 ni 40, huku waliohitimu kidato cha 4 ni 200.
Zamani walikuwa wakifaulu 15-20, huku waliohitimu kidato cha 4 ni 60.
Pia lazima tufahamu kuwa watu wengi ambao hawajazoea masafa marefu ndipo hujifunza kushika usukani kwa muda mwingi kwenda kwao kuringishia harrier zao.
Hamna cha roho za ajali mwezi Desemba. Kama zipo rohi za ajali basi hazihusiani na mwisho wa mwaka.
Hakuna cha sijui roho ya ajali, mara roho ya umwagaji damu kwaajili ya kafara . No.
Kama wapo watu hutoa kafara basi hawawezi kusubiria Desemba. Watafanya muda wowote kwa kadri ya uhitaji wao.