Naanza kuamini nchi hii imejaa vidikteta. Yaani kama tunadhani ni rahisi kukomesha udikteta nchi hii tunajidanganya. Kuna watu udikteta unawafaidisha hadi wako tayari kufanya lolote kuutetea. Kwa taarifa yako;
1. Kuwa mkuu wa mkoa hakumaanishi wewe ni mwamuzi wa mwisho kwa kila kitu ndani ya mkoa. Mfano, Mkuu wa mkoa hana maamuzi juu ya mgonjwa achomwe sindano au apewe vidonge. Vivyo hivyo hana maamuzi ya mwisho ya kubadilisha ramani ya jengo la serikali kwa sababu ya matakwa binafsi, hapo akijitokeza mtu akagoma kubadilisha ramani na akatoa sababu za kitaalamu mtaona anadharauliwa lakini mtaalamu atakuwa sahihi.
2. Kila mtumishi kwenye nafasi yake ana mamlaka kamili. DED ana mamlaka kamili katika nafasi yake mfano, matumizi ya fedha za Halmashauri yaliyopitishwa na Baraza la Madiwani hayawezi kutenguliwa kiboya na Mkuu wa mkoa kisa tu yeye ni msemaji wa mwisho mkoani kwake.
3. Mkuu wa mkoa ana maamuzi kamili katika nafasi yake kwa kufuata Job description ya nafasi yake lakini maamuzi yake yapaswa kufuata ushauri bora wa wataalamu alionao na siyo matakwa binafsi. Ndo maana unaona Wakuu wa mikoa wenye kujua mipaka yao huoni wakigombana na wataalamu wao. Hata wanapochukua hatua husikii mtu alisema Mkuu wa mkoa kamwonea mtu.
4. Kuna msemo siku hizi vijana wanasema "SIMAMA KWENYE JINSIA YAKO". Mkuu wa mkoa anayejitambua anatakiwa kujua mipaka ya madaraka yake. Lakini ukikuta mkuu wa mkoa anataka kukagua ghala la silaha za Polisi au kuamuru mtuhumiwa fulani aachiwe kwa vile tu yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama (KUU) mkoa, ujue huyo ni Bomu na muda wowote atalipua mkoa.
5. Mkuu wa mkoa au mkuu yeyote wa Idara hana hiari ya kudharau wa chini yake na kuwadhalilisha hadharani kwa vile tu yeye ni Mkuu. Kuheshimu walio chini yake ni miongoni mwa masharti ya uteuzi wake. Asipofanya hivyo sheria ya Mahusiano kazini inamtaka aidha ajiondoe au aondolewe.
6. Mkuu wa mkoa hapaswi kuwa mtu wa majungu na kufanyia kazi taarifa za kuokoteza. Ukiwa mkubwa kazini fanya maamuzi ambayo kila anayeona ajue una taarifa sahihi, majungu na umbea isiwe sehemu ya maamuzi yako kama Mkuu.
Kwa hayo hapo juu, Gambo kutumbuliwa pamoja na DED na DC Arusha ni kumheshimu tu, lakini alitakiwa aondoke peke yake ili liwe fundisho kwa wakuu wa mikoa na wilaya wanaofanya kazi kinyume cha miongozo ya nafasi zao.