Kama ndio hvy zidane asingepaswa kuwa na ballon dor 3 ..kwa vigezo hivyo zidane ilipaswa awe na ballon dor moja tu
Kingine midfielders sio strikers hivyo huwezi kutoa kigezo cha magoli tu kwenye ballon dor basi iitwe strikers ballon dor maana defenders na midfielders itakuwa hawajatendewa haki
Kingine Modric alikuwa na perfomance bora uefa champions league na world cup pia alikuwa exceptional mpk kila mtu alisuuzika moyo wake baada ya kupewa tuzo ya mchezaji bora wa dunia
Na la mwisho wanaopiga kura ni makocha na makapteni wa timu za taifa na waandishi wa habari za michezo na kwa pamoja wameona Modric ndiye aliyestahili
Nimefurahi kuona tuzo ikirudi kwa midfielder hii tuzo haijaumbiwa kwa masteikers tu ..hongera Luca modric
Kumfananisha zidane na modric ni kutolitendea haki soka.
Mechi muhimu zaidi hasa za fainali ambapo mbinu zote zinashindikana yeye ndio unamuona kila sehemu,refer fainali ya brazili,italy, leverkusen etc
Zidane wenzake ni GOAT wengine kina maradona, pelle etc.
World cup sawa nakubali modric alikuwa bora ila UEFA ilikuwa nibebe nibebe naweza taja hata wachezaji 10 bora zaidi ya modric kwenye uefa iliopita. Japo mimi mshabiki wa man u ila salah, mane na firmino walikuwa bora zaidi Uefa kuliko modric.
Hebu niambie perfomance gani ya Modric Uefa kumzidi Mane? Au kumbukumbu yako hebu nitajie iconic perfomance yake inayo highlight huo uchezaji bora wake?.
Ukija kwenye ligi kacheza mechi 23 tu (15 hajacheza) nako pia alikuwa average.
Na ndio tusijudge midfield kwa magoli ila modric kama creative player tunatakiwa tumjudge kwa chance anazocreate na assist,ila vyote hivyo modric sio best duniani.
Watu kama Ronaldo, Varane, mbape, salah,de bruyne etc walikuwa bora zaidi kwa muono wangu.
Na hizo votes ndio zinazoharibu baloon d or, siku ukizidownload na kuangalia ndio utaona ambavyo sio fair, popularity na uwezo wa mpira ni vitu viwili tofauti kuna makapteni wa nchi za ajabu ajabu hawana hata interest na mpira wanavote tu randomly.