Napinga Tulia Ackson kuwa Mgeni Rasmi kwenye mechi ya Simba na Wydad Cassablanca

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Asalaam Aleykhum , Eid Mbarakha .

Baada ya Salamu hiyo na baraka hizo za Eid el Fitri naingia moja kwa moja kwenye hoja .

Nimepata taarifa kwamba Timu yangu ya Simba imemteua ndugu Tulia Ackson kuwa mgeni rasmi kwenye mechi yake ya Klabu bingwa Africa dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco , Wala haijafahamika vigezo wala sababu zozote zile zilizopelekea Ndugu Tulia kuteuliwa kuwa mgeni Rasmi kwenye game muhimu kama hii .

Nachukua nafasi hii kupinga jambo hilo kwa nguvu zote , Tulia hafai kuwa Mgeni Rasmi kwenye mechi kama hii kwa vile ataleta mgawanyiko kutokana na siasa zake za chuki na Ubabe , uchunguzi unaonyesha kwamba huyu ndio Spika anayechukiwa zaidi na wananchi tangu kuanza kwa utaratibu wa Bunge nchini Tanzania akifuatiwa na Job Ndugai , hajawahi kuwa mwanamichezo zaidi ya kushabikia ngoma za asili za huko kwao ambako nako alijiingiza ili apate umaarufu wa kisiasa tu .

Mechi hii inataka Mshikamano wa wadau wote , kuingiza Uwanjani mtu aliyevuruga bunge hadi kuwa kama muhuri wa kupitisha kila kitu na asiyekubalika kwenye jamii ni sawa na kujitafutia matatizo ya bure tu , kwanza Tulia Ackson hana Bahati kwenye soka , ndio maana tangu awe mbunge wa Mbeya timu za soka za huko zinaporomoka utadhani zinauza mechi kama inavyosuasua Mbeya City , mnataka na Simba ifike huku ?

Hata hivyo bado muda ungalipo na ili kuondoa nuksi tunaamini viongozi wa Simba watatubadilishia Mgeni Rasmi .
 
Asalaam Aleykhum , Eid Mbarakha .

Baada ya Salamu hiyo na baraka hizo za Eid el Fitri naingia moja kwa moja kwenye hoja .

Nimepata taarifa kwamba Timu yangu ya Simba imemteua ndugu Tulia Ackson kuwa mgeni rasmi kwenye mechi yake ya
uchunguzi unaonyesha kwamba huyu ndio Spika anayechukiwa zaidi na wananchi tangu kuanza kwa utaratibu wa Bunge nchini Tanzania

Mh!!!!! Naomba utuonyeshe chapisho kuonyesha huo uchunguzi!!!!!

Chuki zako binafsi usitulazimshe wote tukubaliane nazo!!!!!!!!!!!
 
Tafiti hupingwa kwa Tafiti mpya
 
mmh! we Jomba una bifu na dada yako kisa tu mnatofautiana chama... (gwe ilumbugo ujo)..... mnapoenda likizo Mbeya mkae myamalize maana sio kwa chuki hiii.....!!
 
Kwanza mpe heshima yake ni dk tulia
Halafu kila mgeni ni lazma viwekwe vigezo acha upuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…