Napinga Tulia Ackson kuwa Mgeni Rasmi kwenye mechi ya Simba na Wydad Cassablanca

Napinga Tulia Ackson kuwa Mgeni Rasmi kwenye mechi ya Simba na Wydad Cassablanca

Asalaam Aleykhum , Eid Mbarakha .

Baada ya Salamu hiyo na baraka hizo za Eid el Fitri naingia moja kwa moja kwenye hoja .

Nimepata taarifa kwamba Timu yangu ya Simba imemteua ndugu Tulia Ackson kuwa mgeni rasmi kwenye mechi yake ya Klabu bingwa Africa dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco , Wala haijafahamika vigezo wala sababu zozote zile zilizopelekea Ndugu Tulia kuteuliwa kuwa mgeni Rasmi kwenye game muhimu kama hii .

Nachukua nafasi hii kupinga jambo hilo kwa nguvu zote , Tulia hafai kuwa Mgeni Rasmi kwenye mechi kama hii kwa vile ataleta mgawanyiko kutokana na siasa zake za chuki na Ubabe , uchunguzi unaonyesha kwamba huyu ndio Spika anayechukiwa zaidi na wananchi tangu kuanza kwa utaratibu wa Bunge nchini Tanzania akifuatiwa na Job Ndugai , hajawahi kuwa mwanamichezo zaidi ya kushabikia ngoma za asili za huko kwao ambako nako alijiingiza ili apate umaarufu wa kisiasa tu .

Mechi hii inataka Mshikamano wa wadau wote , kuingiza Uwanjani mtu aliyevuruga bunge hadi kuwa kama muhuri wa kupitisha kila kitu na asiyekubalika kwenye jamii ni sawa na kujitafutia matatizo ya bure tu , kwanza Tulia Ackson hana Bahati kwenye soka , ndio maana tangu awe mbunge wa Mbeya timu za soka za huko zinaporomoka utadhani zinauza mechi kama inavyosuasua Mbeya City , mnataka na Simba ifike huku ?

Hata hivyo bado muda ungalipo na ili kuondoa nuksi tunaamini viongozi wa Simba watatubadilishia Mgeni Rasmi .
Unamuonea wivu mwanamke?
 
Back
Top Bottom