Napinga wazo la Muziki wa Singeli kusambazwa duniani

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Habari,

Wiki kadhaa zilizopita alisikika Waziri wa Utamaduni na michezo Profesa Kabudi akisema kwamba serikali kupitia wizara yake ina mpango wa kuupeleka muziki wa singeli Kimataifa.

Mimi binafsi napinga na ninakataa wazo hili kwa sababu zifuatazo;

1.Ni muziki unaotumia lugha chafu na unatoa ujumbe wa kuhamasisha tabia mbaya katika jamii nitatoa mifano ya nyimbo hizo
✅Hainaga ushemeji-Manfongo
Huu wimbo ukisikiliza ujumbe uliomo ndani ni kwamba hata ukiwa na mke/mchumba ni ruksa marafiki au ndugu wa kiume kumtongoza na kulala na mkeo kwa zamu.
✅Nakupenda wewe na huyo bwanako-Meja Kunta ft Mabantu
Ujumbe ndani ya wimbo huu ni kwamba kuna mtu ana mke wake halafu kuna kijana anampenda huyo mwanamke na huyo bwanake(anawapenda wote) sasa najiuliza hapa tunapewa ujumbe gani kama jamii?mapenzi ya jinsia moja,mapenzi mchanganyiko?huyu anayewapenda wote anataka nini?au ni bisexual?
✅Uchezaji usiozingatia maadili
Nyimbo tajwa hapo juu na nyingine za singeli ukiangalia video zake wanawake humo ndani wanacheza aidha na kanga moja iliyomwangiwa maji(hapa wanachaguliwa wenye makalio makubwa) au wanatikisa makalio na matiti kwa namna ya kushawaishi ngono au mwanamke kuinama na kushikwa kiuno huku akitikisa makalio,sasa najiuliza ni nchi gani wameomba kupelekewa huu uhuni?

Tuchukulie Leo timu ya Wizara na wasanii chini ya Kabudi wanakutana na Trump wamekaa kisha wakaweka hio video kwenye screen kubwa ili kuutambulisha wimbo wa hainaga ushemeji Je ni kweli utatazamika?Haya Bwana Trump akaomba kujua ujumbe uliomo utamwambia nini?
Trump; Mr Minister can you tell us the message from the song you've just played?
Kabudi;Yaa,of course Mr president it means your friends and brothers can eat your wife at any time(no barriers)hata nashindwa kutafsiri rasmi hapa
Au ule wimbo wa pili utasema tafsiri yake nini sasa 'Mr President it means I love you and your husband😀

Hivi kweli Mzee kabudi anaweza kutazama hizi nyimbo ndani ya familia yake?
Ndugu zangu hata kama tunatafuta kuwaridhisha hawa wasanii ili kujinufaisha kisiasa tuangalie kesho yetu itakuaje?

Ushauri wangu ni kwamba huu muziki lazima tuusafishe kwanza uwe ni muziki wa maadili na ukubalike kwanza hapa ndani ya nchi kabla ya kuupeleka huko nje.
Tuupe muda na hawa wasanii wa Singeli waelimishwe kwanza lengo la muziki ni kuelimisha na kuburudisha jamii na sio kuhamasisha uchafu.
Kwahio tuuzuie kwanza kwenda nje usije kutuaibisha na kutufanya tuonekane Tanzania ni watu wa hovyo.
Ahsante.

View: https://youtu.be/I590Q-MH0vQ?si=KfdfoB8UepfPbqpB

Pia soma:Thread 'Profesa Kabudi atangaza kusambaza Singeli Dunia Nzima. Atatumia njia gani? Anajua mwenyewe' Profesa Kabudi atangaza kusambaza Singeli Dunia Nzima. Atatumia njia gani? Anajua mwenyewe
 
Unamsagia mzee kunguni unataka atokeje kwa mama? Mwenzio kaona wizara yake itamtoaje kaamua liwalo na liwe
 
Kama tunaona kupanda kisiasa ni muhimu kuliko ustawi wa jamii sawa
 
Ccm ndio mtaji wa wajinga kwa vile wimbi kubwa la vichaa,wavuta bangi,vijana wengi wa uswahilini walikosa maisha na ajira ni wasikiliza singeri wengi.
Ili kutumia fursa hii lazima watumie ili sio kusambaza maparachichi au matunda dunia ili vijana waongeze nguvu za kulima.
 
Habari,

Wiki kadhaa zilizopita alisikika Waziri wa Utamaduni na michezo Profesa Kabudi akisema kwamba serikali kupitia wizara yake ina mpango wa kuupeleka muziki wa singeli Kimataifa.

Mimi binafsi napinga na ninakataa wazo hili kwa sababu zifuatazo;

1.Ni muziki unaotumia lugha chafu na unatoa ujumbe wa kuhamasisha tabia mbaya katika jamii nitatoa mifano ya nyimbo hizo
✅Hainaga ushemeji-Manfongo
Huu wimbo ukisikiliza ujumbe uliomo ndani ni kwamba hata ukiwa na mke/mchumba ni ruksa marafiki au ndugu wa kiume kumtongoza na kulala na mkeo kwa zamu.
✅Nakupenda wewe na huyo bwanako-Meja Kunta ft Mabantu
Ujumbe ndani ya wimbo huu ni kwamba kuna mtu ana mke wake halafu kuna kijana anampenda huyo mwanamke na huyo bwanake(anawapenda wote) sasa najiuliza hapa tunapewa ujumbe gani kama jamii?mapenzi ya jinsia moja,mapenzi mchanganyiko?huyu anayewapenda wote anataka nini?au ni bisexual?
✅Uchezaji usiozingatia maadili
Nyimbo tajwa hapo juu na nyingine za singeli ukiangalia video zake wanawake humo ndani wanacheza aidha na kanga moja iliyomwangiwa maji(hapa wanachaguliwa wenye makalio makubwa) au wanatikisa makalio na matiti kwa namna ya kushawaishi ngono au mwanamke kuinama na kushikwa kiuno huku akitikisa makalio,sasa najiuliza ni nchi gani wameomba kupelekewa huu uhuni?

Tuchukulie Leo timu ya Wizara na wasanii chini ya Kabudi wanakutana na Trump wamekaa kisha wakaweka hio video kwenye screen kubwa ili kuutambulisha wimbo wa hainaga ushemeji Je ni kweli utatazamika?Haya Bwana Trump akaomba kujua ujumbe uliomo utamwambia nini?
Trump; Mr Minister can you tell us the message from the song you've just played?
Kabudi;Yaa,of course Mr president it means your friends and brothers can eat your wife at any time(no barriers)hata nashindwa kutafsiri rasmi hapa
Au ule wimbo wa pili utasema tafsiri yake nini sasa 'Mr President it means I love you and your husband😀

Hivi kweli Mzee kabudi anaweza kutazama hizi nyimbo ndani ya familia yake?
Ndugu zangu hata kama tunatafuta kuwaridhisha hawa wasanii ili kujinufaisha kisiasa tuangalie kesho yetu itakuaje?

Ushauri wangu ni kwamba huu muziki lazima tuusafishe kwanza uwe ni muziki wa maadili na ukubalike kwanza hapa ndani ya nchi kabla ya kuupeleka huko nje.
Tuupe muda na hawa wasanii wa Singeli waelimishwe kwanza lengo la muziki ni kuelimisha na kuburudisha jamii na sio kuhamasisha uchafu.
Kwahio tuuzuie kwanza kwenda nje usije kutuaibisha na kutufanya tuonekane Tanzania ni watu wa hovyo.
Ahsante.

View: https://youtu.be/I590Q-MH0vQ?si=KfdfoB8UepfPbqpB

Pia soma:Thread 'Profesa Kabudi atangaza kusambaza Singeli Dunia Nzima. Atatumia njia gani? Anajua mwenyewe' Profesa Kabudi atangaza kusambaza Singeli Dunia Nzima. Atatumia njia gani? Anajua mwenyewe

Naunga mkono hoja. Mziki unaotambulisha taifa hauwezi kuwa singeli.
 
Back
Top Bottom