Napingana na barua ya Wizara. Sababu 5 kwanini video ya mochwari ni halisi na sio AI

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
472
Reaction score
581
20251116_155327.jpg

Wadau,

Nimeona tamko la leo, Novemba 16, 2025, kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Afya likikana vikali uhalisia wa video inayosambaa inayoonyesha idadi kubwa ya miili ya watu. Wizara imedai video hiyo "imetengenezwa na wahalifu wenye nia ovu" na "siyo ya uhalisia."

Nimepitia kwa makini ile video ya kutisha yenye urefu wa karibu dakika moja.

Hizi hapa hoja 5 kwanini napingana na tamko la Wizara:

1. Wizara Imejichanganya: Picha Kwenye Tamko ni ya Kwenye Video!

Hili ndilo kosa kubwa la kimantiki walilofanya. Picha waliyoitumia kwenye barua yao ya kukanusha (ile Shuka ya MSD) ni 'screenshot' iliyotolewa moja kwa moja kutoka kwenye hiyo video wanayodai ni feki!

-Ushahidi: Angalia video yenyewe kuanzia sekunde ya 9 hadi 10 (00:09 - 00:10). Utakiona miili imefunikwa na Shuka hizo nyeupe.
Swali: Ikiwa video "imetengenezwa" na "siyo ya uhalisia," Wizara ilipataje 'screenshot' halisi kutoka ndani ya video hiyo na kuitumia kwenye tamko lao rasmi? Huu ni ushahidi tosha kwamba wanajua video ipo na ni halisi, lakini wanakana tu muktadha wake.

2.Mwendo wa Kamera (Shaky Cam)

Video yote imerekodiwa kwa mkono unaotetemeka, kwa kutumia kile kinachoonekana ni simu ya mkononi. Mwendo huu (shaky cam) unaonyesha wazi mtu anayerekodi anafanya hivyo kwa haraka, pengine kwa siri na hofu, huku akitembea. Hii ni alama ya "citizen journalism" au kurekodi kwa siri.

Video za AI au CGI huwa na mwendo laini (smooth render) au makosa ya kimuundo unaweza kuta Meza ipo mdomoni kwa mtu kichwa kipo kwenye mguu n.k ambayo hapa hayaonekani..

3.Mazingira Halisi Yanathibitisha Eneo

Video haionyeshi miili pekee; inaonyesha mazingira halisi ya jengo.
-Ushahidi Muhimu: Kuanzia sekunde 00:22 hadi 00:27, kamera inapanda na kuonyesha waziwazi milango ya chuma ya majokofu ya kuhifadhia maiti (morgue freezers). Hii inathibitisha bila shaka kuwa eneo la kurekodia ni mochwari au kituo cha afya chenye chumba cha kuhifadhia maiti.
-Muundo wa Jengo: Korido ndefu na ngazi zinazoonekana ni sehemu halisi za jengo, si kitu cha "kutengeneza" kirahisi.

4.Maelezo Mahususi (Specific Details)

Video za AI zinashindwa vibaya sana inapokuja kwenye maelezo madogo na mahususi. Kwenye video hii, kuna maelezo mahususi yanayothibitisha uhalisia

Shuka na T-shirt Maalum: Kwenye sekunde 00:09 hadi 00:10, kamera inasimama kidogo na kuonyesha mwili uliofunikwa na Shuka nyeupe yenye maandishi yanayosomeka kama "MSD". Hii ni "specific identifier" (alama mahususi) ambayo ni vigumu sana kwa AI kutengeneza kwa usahihi huu na inaonyesha ni tukio halisi.

5.Uhalisia wa Picha (Physics & Lighting)

Jinsi miili ilivyolala, jinsi nguo zilivyokaa mwilini, na jinsi mwanga (kutoka madirishani) unavyoakisi kwenye sakafu na kuta, vyote vinaendana kikamilifu na sheria za fizikia (physics) za ulimwengu halisi.

Hakuna "glitches", "artifacts" (makosa ya picha), au mwingiliano wa ajabu wa vivuli (shadows) ambao huwa ushahidi mkuu wa video feki. Ni picha halisi inayoonyesha hali ya kutisha ya mochwari iliyozidiwa uwezo.

Hitimisho

Video hii ni halisi. Hoja ya kuwa "imetengenezwa" au ni "AI" haina mashiko kiufundi. Mjadala sasa usihusu kama video ni feki, bali ujikite kwenye maswali ya msingi: Video hii imerekodiwa lini? (Wanasema ni ya kati ya tar 1-3).. Wapi? (Inaelezwa ni Mwananyamala RRH, Sijui maana sijawahi kufika nimeona waliofika wanakubali kusema ni ya pale)

Na nini hasa kimesababisha mkusanyiko huu wa kutisha wa miili ya binadamu katika eneo moja? (Huenda nafahamu lakini labda kuna namna nyingine ilikuwa 🤦)
 
Wajinga sana hao jamaa. Wanajua kuna namna ya kufanya ukajua picha ni ya AI au hapana. Yaani hawa ndo hopeless hasa. Wangekaa kimya tu. Sasa jamaa wakiongeza zingine itakuwaje
😃😃Watasema ni AI tena ...kuna zile za arusha 🙌🙌
 
View attachment 3502763

Wamekiri wahalifu
 
Wakiinama nchale wakiinuka nchale🤣🤣🤣
 
AI video due to technological improvement make their video in 4k quality. From the video i saw that was a mobile perhaps chines made like tecno or the person was hurry and shaking.
Siku hizi hata ukiandika essay kwa Ai ipo program inakagua inasema .essay hii ni AI.
I remember TARIK AZIZ. HIS DEMISE WAS TRAGICALLY. Wonder that spoke person thinking capacity
 
CCM Wana miaka 70 Toka wamezaliwa ni ngumu Sana kuwa na Akili za kisasa
Kuna watu tulishasema miaka mingi iliyopita. Ili Taifa lipone, hili kundi linaloitwa ccm linatakiwa liondolewe madarakani. Tena kwa kutumia nguvu ya umma. Maana kwenye idara zote wamejaa wao. Hivyo huwezi kuwaondoa kwa kutumia jeshi au sanduku la kura. Isipokuwa kwa kutumia nguvu ya umma.
 
‎THE CLEAR MESSAGE FROM TRUMP
‎
‎God has blessed your country. Go back and hold your corrupt leaders accountable. Stop loitering the streets of America.
‎
‎If Americans were docile and refused to initiate Revolution, then you would never see such an amazing nation like USA.
‎
‎If France kept mum in 1775, you wouldn't see a developed nation like France.
‎
‎If you like, keep playing tribal politics in suffering while your ruling class loot with reckless abandon.
‎
‎Stop depending on WHO for subsidized drugs. At your age, you ought to have home-made drugs for common ailments. On that ground, America has left WHO.
‎
‎Why must your country depend on the goodwill from WHO? Has God not blessed your country with professors of medicine, pharmacy, etc who could develop your nations hospitals?
‎
‎Go and hold your ruling class accountable for rots in health care delivery. When they are sick, they run to USA for treatment with your national resources.
‎
‎Keep playing tribal politics but get out of USA. If you're ready, you will take over your country from destiny destroying ruling class as they did in France.
‎
‎All decent nations have accurate population index. Even in hell fire, God has a record of those in it. America belongs to Americans not indians, Nigerians, Chinese, Mexicans, and other nationals who want good life and escaped to USA.
‎
‎We fought for liberty and advancement. Keep quiet and wait for angels to repair your bad roads. Remain dumb as ministers, Governors, commissioners, etc loot in trillions.
‎
‎Return to your country and change the narratives. No more running to America with your heavily pregnant wives. You want them to give birth in America and automatically become citizens of America. That is revoked immediately.
‎
‎Are you praying for God to fix your bad roads? Keep praying. Was it God that fix the roads you see in USA, France, UK, Canada, Saudi, etc? Remain in your country and face the rots. If you like allow electoral umpire to be under your corrupt Politicians. Allow them to keep rigging while your religious leaders sing to your ears that those rigged into power are "God's will for your country"!
‎
‎If truly you are tired of your country, arise and face the rulling class squarely. The french people in their millions didn't fear the military. They all involved in the Revolution that gave birth to a New France.
‎
‎Ohhhh, are you fasting to have stable electricity? Just continue. If you don't want to pay the price, why do you run to USA, France, Canada, etc for a better life? Remain in your country and enjoy the consequences of being docile.
‎
‎
‎The message is clear. Let it sink into the skulls of all those who desire a new Africa
‎
 
Usije shangaa baada ya mda wanakuja kijibu hoja yako.Maana siku hizi nilichokiona mange kimambi akieleza kwenye mitandao iliyofungiwa wahuni wanakuja kukanusha
 
Back
Top Bottom