Napingana na Dunia nzima, Kenya inaangamia!


Unayohaki ya kusema hayo uliyosema lakini unakumbuka mkurugenzi wa ICT wa tume hiyo ya uchaguzi alichokisema na unajua kilichompata?

Je waliofanya walikua wanamfurahisha mzungu?

Je hao walioingilia mfumo pasipokuwa na ridhaa hawawezi kuwa ni wale waliomuua Mkurugenzi yule na kuondoka na kiganja chake?

Je haiwezekaniki hao ndio walioingia kuvuruga matokeo? Je hao walikua wanamfurahisha mzungu yupi?

Shida unarukia matokeo bila kuangalia njia iliyopitiwa kufikia matokeo?

Kuna msemo wa wahenga: the mpre you grow the more you expose your butt.
 
Kwanza mkuu Kenya ni miongoni mwa nchi za Africa ambayo sio Maskini naomba nikusahihishe katika hilo mengine nakuunga mkono na kwa mkwara alio chimba jana Uhuru, haina shaka Uhuru lazima arudi tena madarakani by hook or crook

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee,hebu ficha ujinga wako basi.
Miezi 3? Nani kakwambia hivo? Inamaana kila mwezi unasiku ishirini?

Nani ka kwambia Kenya hawana pesa ya kurudia uchaguzi?

Nani ka kwambia kenya kuna njaa na hawajiwezi?

We unafikirikia mavitu yako akilini mwako,unatakakutuhamishia huo ujinga sio??
 


Nimeshaliongela hilo kwenye post yangu, nimesema kwamba kwenye nchi Masikini kama hizi zetu hauwezi kuwa na 100% free and fair elections kwanza hata nchi zilizoendelea pia hakuna kitu kama hicho na kilichopo wanacompromise tu ili maisha yaendelee, ndo maana mpaka leo hii hata USA Trump anasema illegal immigrants walipiga kura, kwanza kuna maeneo USA watu waliokufa walipigishwa kura na liko documented, hivyo kama utaruhusu kwenye masikini kila mtu akashitaki Mahakamani kwa kila hitilafu basi utakuwa hakuna kingine unafanya miaka yote isipokuwa kusikiliza kesi na kurudia chaguzi tu!
 


Kila kitu kipo wazi, Kenya ni nchi masikini third world country yenye kila aina ya umaskini wa third world country, hivyo kukana kwamba Kenya haina shida ya chakula ni kuwa mjinga!
 
Hizo ni vijisababu vya mtu mvivu, kunazo nchi za kisocialist ambazo ni tajiri au zina uwezo mkubwa duniani,
Alfu isitoshe, Tz iliachq mambo yaki socialist kitambo sana, tena nyinyi ni nchi ya pili au tatu africa kwa madini
 

Unaitaja Lumumba unasahau
Kikundi chenu cha kibendera mlipongeza uchaguzi wa kenya kuwa ulikuwa huru na haki
nakumpongeza uhuru kwa kushinda kihalali leo mnageuka!!
Kweli Aliye Waroga kisha kufa
 
Hizo ni vijisababu vya mtu mvivu, kunazo nchi za kisocialist ambazo ni tajiri au zina uwezo mkubwa duniani,
Alfu isitoshe, Tz iliachq mambo yaki socialist kitambo sana, tena nyinyi ni nchi ya pili au tatu africa kwa madini
Umekalia Ncha kali!!
Ulicho kijibu hapo nini!
Umekatikia njia kama unachomwa na mwiba!
 
Kila kitu kipo wazi, Kenya ni nchi masikini third world country yenye kila aina ya umaskini wa third world country, hivyo kukana kwamba Kenya haina shida ya chakula ni kuwa mjinga!
Kwa hiyo kama ni 3rd world country,inamaana kuwa watashindwa kugharamikia uchaguzi tena?

Hata kama ni 3rd world,umaskin wao huwezi kuufananisha na huu wa kwenu.

Kama huku munaweza kuwafuta wabunge 8 wa Cuf bila sababu ya msingi,huoni ni kama mnatafuta kurudia uchanguzi ikiwa wabunge wa Cuf wataamua kuachia wote?

Sasa kama ninyi mmejiamini kuwa hata wakiachia mtarudi kwenye uchaguzi,kenya watashindwa nini,na wao uchumi kwao ni mara 22 ya kwenu?

Jiongeze mkuu,ushabikie kila jambo la srikali hii.UKUKU
 
akili ndogo muda wote huwa na mawzo hasi ndio kama akili ya mtoa mada!!sikukusikia ukikanusha ya ccm iliyoyafanya zanzibar kwa upumbavu tu kufuta uchaguzi kisa hawa kushinda sasa wenzetu kenya maamuzi yametolewa na mhimili mwingine kati ya mihimili inayounda serikali unaita katiba ya kenya mzigo je hii katiba chakavu ya mpito ya kikoloni tulionayo kwetu tuiteje sasa
 
Umekalia Ncha kali!!
Ulicho kijibu hapo nini!
Umekatikia njia kama unachomwa na mwiba!
shindana kwa hoja sio kejeli alichosema kina eleweka wewe tu kwa akili ya ccm huwezi kuelewa maana kwenu ukweli ni uchochezi
 
Umekalia Ncha kali!!
Ulicho kijibu hapo nini!
Umekatikia njia kama unachomwa na mwiba!
Hayo unayojaribu kusema ni vijisababu tu.eti sijui socialist, capitalist ... Madini mnayo kupindukia lakini bado mko nyuma ya kenya kiuchumi kenya hii ambayo 70% ni ukame! Asilimia 80% ya nchi inaishi ndani ya asilimia 30% ya nchi manake huko kwengine hakuishiki!
 
Usitake kubishana na sheria, kama huna uelewa wa sheria utakesha ukitokwa povu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wewe ni typical Mwafrika, unataka kuprove kitu kwa Muzungu hkn kingine, kama ungewajali Wakenya hivyo angalau ungeguswa na gharama na fedha wanazopoteza kwa ujinga tu, fedha ambayo wangewekeza kwenye ustawi wa jamii yao!

Hili la gharama sikulisikia likiongelewa uchaguzi wa Zanzibar ulipofutwa na kurudiwa upya.
 
mimi naona unaongea pumba tu, ni haki yako kutoa povu. hivi Africa kuna nchi ndogo kama zanzibar? Zanzibar sio km inauchumi mdogo bali haijimudu kabisa na wamerejea uchaguzi na hakuna hata mmoja aliewahi kukemea leo ije iwe kenya ambayo sarafu yake ipo juu kuliko Tanzania. unaongea pumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sielewi chochote kuhusu huko unakokuuita kununuliwa kwa Lipumba, kama ingekuwa ni kweli na ningethibitisha hilo ingeniuma tena sana tu!

Unaongeleaje mabilioni ya pesa yaliyopotea wakati wa mchakato wa katiba na hakuna tulichoambulia cha maana? Huwezi kuwa na huruma na uchungu zaidi kwa pesa za jirani wakati unafuja za kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…