Napingana na wanaosema Usiweke pesa yote kwenye biashara mpya

MendeOLD

Senior Member
Joined
Feb 13, 2023
Posts
196
Reaction score
405
Watu wanao anza kufanya biashara kuna maneno wanakutana nayo utakuta mtu anomba ushauri vizuri ana million zake 20 mtu ana shauri tumia million 10 kumi iweke kwanza, au una million 5 utaskia tumia 3 mbili skilizia kwanza.

Ukiona unapewa ushauri wa namna iyo ujue unapewa na mtu maskini au bado ana fikra fupi yaani ana ndoto za Kawaida tu za kupata ela ya kula na sio kua tajiri, business is about risk kikubwa usikimbilie biashara ambayo ipo nje ya mtaji wako.

Mfano utakuta mtu ana million zake 90 anakimbilia kununua Eicher haijui iyo biashara ipoje ajui spear zake ikiaribika na Hana akiba hapo sawa, ila kama utafuta biashara ambayo ipo ndani ya uwezo wa mtaji wako kwa mfano una ten million unataka kufanya biashara ya vipodozi nakushauri weka mzigo wote usikilize wale wa weka tano kwanza tano skilizia.

Watu wa karba iyo wana low minded na hawana ndoto kubwa. Epuka kuomba ushauri kwa watu hao.


Mkulima wa kahawa misenyi mkoani Kagera, kwa sasa Kuala Lumpur Malaysia.
 
Maneno mengi Lakin Kuna kitu yamemiss....
Yan una akili timamu uweze kupata 20m au 90m Ila anahitqji ushauri ili kuongeza kipato..?? Kwamba hio Hela ameiokota..?? Kwanini asitumie mbinu hizo hizo alizopata 20m au 90m? Kama kumshauri awekeze sehemu ya fedha kwa kusikilizia Ni umasikini Basi mwenye hizo Hela ndio masikini wa kutupwa
 
Mtoa mada umeongea pumba ya kiwango cha SGR.
Kwani wewe unadhani kwenye biashara ukinunua stock ya bidhaa kisha ukaziweka store ndio ushamaliza?
Hujui kwamba kutakuwa na mzigo wa kulipa kodi ya ofisi/store/fremu?
Hujui kwamba kutakuwa na mzigo wa kulipa mishahara wafanyakazi/wasaidizi wako?
Hujui kwamba kutakuwa na mzigo wa nauli za kila siku au pesa ya fuel ya gari lako kwenda ofisini na kurudi kila siku?pesa ya fuel kwenda kutembelea wateja mahali wanakopatikana?Pesa ya gharama za matangazo?
Kwa akili hiyo ukianzisha biashara haiwezi kudumu hata miezi 3
 
Usisahau kutuletea japo pakti za BOH TEA 🍵 utajapo rejea Huku nyumbani Tz
 
Weka Hela upate Hela mkuu, pesa haitaki ujanja ujanja
 
Money laundering
 
Mishahara unalipa kabla ya kufanya kazi?
 
Mishahara inalipwa baada ya mahudhurio ya kazi,kumbuka ya kwamba wateja wakija ama wasipokuja kununua wafanyakazi wako hiyp haiwahusu tarehe zikifika ni lazima uwalipe mishahara yao.
Sasa ikitokea hujaingiza pesa za kutosha na hela zote umemaliza kwenye akaunti yako utawalipaje mwisho wa mwezi?
Mishahara unalipa kabla ya kufanya kazi?
 
Mkuu tunaongelea mtu anayeanza biashara
 
Inawezekana kapata kwa kustaafu ajira!
 
Mtoa mada kwa biashara mpya hutakiwi kumaliza hela zote kwasababu stock ya kwanza utanunua kwamujibu wa mahewabu yako lakini stock zinazofuata utanunua kwamujubu wa oda,
Kwa mfano unauza vocha za jumla ukawanya sawasawa lakini katika mauzo ukagundua vocha za yas na voda ndio zinatoka zaidi manake utaongeza zaidi hizohizo zinazotoka usishangae kariakoo mti anaagiza contena nne za mzigo contena mbili ni mzigo mmoja mbili zingine ndio mizigo ya kuchanganyia kwamfano sokoni huwez kununua kreti za pepsi na coca kwa kiwango sawa kwasababu za pepsi zinanunulika sawa au maji makubwa na madogo lita moja inanunuliwa sana,
Unaweza kujilaumu umetumia gharama kubwa kwenye mzigo wenye mzunguko mdogo wakati mzigo wenye mzunfuko mkubwa umetumia pesa chache mfano.
Muuza mqji mtaani hawezi kununua mqji makubwa lita 5 mengi zaidi ya mqji mafogo lita moja au 1.5
Samahani kwa typing error
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…