Napitia kipindi kigumu nilivamiwa na vibaka na kunipora pesa zangu za mtaji, napitia kipindi kigumu sana wakuu msaada

Napitia kipindi kigumu nilivamiwa na vibaka na kunipora pesa zangu za mtaji, napitia kipindi kigumu sana wakuu msaada

kijana mpambanaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2026
Posts
200
Reaction score
509
Ilikua siku ya ijumaa, majira ya saa sita mchana nikiwa maeneo ya kilimahewa bondeni, kuna mteja wangu wa sabuni aliniagiza nimpelekee kwake nikiwa getini alitoka nikampatia mzigo wake akanipa pesa kisha akanambia nisiondoke kuna mtu mwingine ana taka.

Kweli alitoka dada mmoja nae akachukua mzigo, mara wakatokea vijana wawili kichochoroni wakapita, mmoja akamwambia mwenzake huyu hapa, wakageuza kunifata sikuwa na wasi, walipo fika wakaniamuru niwape pesa, sikuwa nashida niiitoa buku nikawapatia, mmoja akadai Yani sisi unatupa buku, wakatoa visu yule dada akanivutia ndani, nikaanguka nataka simama jamaa hawa hapa.

Wakanikandamiza ukutani wakinielekezea kisu, mmoja akachukua pesa zangu mfukoni, wakaanza kuondoka, NILIPO taka kiwafata Kuna dada akanishauri usiende huko watakudhuru, basi nika ghaili, nilirudi nyumbani na mawazo sana.kesho yake nikarudi kupeleleza ndipo nikatajiwa jina la kijana anaitwa jini mweupe, nikaanza kurudi home nimefika mahala nikaingia msikitini kupata Ibada.

Kipindi natoka nikamuona trafic, nilimfuata nikamueleza akanielekeza kituoni cha polisi jirani tu hapo, nilienda nilipo fika nashukuru mwenyezi mungu nilipokelewa vizuri nikajieleza nikamtaja mhusika, basi bhana mara paap nikapewa mpelelezi, tukaanza kumtafuta huyo kibaka na mwenzake, baadae nikapewa taarifa kuwa jini mweupe kashikwa nilipo letewa kumtambua hata wala hafanani na yule jamaa walio nikaba nikakata kuwa sio huyu basi ikabidi niambiwe niwe na subra taitwa.

Nilitoka huku najiuliza Sasa taishije hapa mjini sina hata ndugu na pesa zote kibaka kabeba, nikasema no acha nipande huko juu kumsakua, nikaanza ruti hapa na pale kule na huku mara paap yule kibaka huyu hapa, hakunitambua nikamfatilia mpaka huku juu kituo cha Banda maiti, nikarudi kwa bibi mmoja huwa ni mteja wangu na hiki kisa anakijua nikamueleza yule kibaka nimemuona akasema aha Sasa beba hawa watoto kawaoneshe watakuja kutuambia ninani hao basi bhana nikaenda na hao watoto nika waonesha walivo muona wakaja kuwambia ni Fulani wao wakamtambua, basi bhana nikapiga simu kwa mpelelezi nae akadai ana dharura hivo niwe na subra, basi bhana ndo hivo Sasa NIKO nasubiri kuona hatma, kwa kweli hawa vibaka wamenilostisha sana napitia kipindi kigumu sana ndugu zangu basi tu, maisha haya. Yani Kila kitu kwangu cha shida Sasa nateseka kwa sababu ya watu Fulani tu. Natamani walau nipate member mmoja tu kipindi hiki anishike mkono kwa kweli napitia kipindi kigumu sana,
 
Umeibiwa ijumaa, jumamosi ukaamua ujiunge jf.

anyway kwanza hueleweki stori yako inataka nini, mwanzo umeanza kwa huzuni, mara dada akakuvutia ndani, mara ukaja kipande cha kuchanganyikiwa ukaenda kwa trafiki badala ya polisi

umefuata kipande cha userious ukaenda polisi ukapewa mpelelezi, ukafuata sehemu ya comedy ulipoingia kumsaka jini na kumpeleka kwa bibi, yaani hueleweki kiujumla.

anyway mzunguko wa srori yako yote shortcut yake ni mistari mitatu ya mwisho uliyoiandika
 
Pole. Aina gani ya msada unahitaji?? Eleza matajiri wa jf wanaweza kukusaidia.
Kwanza nipate mtu anaefahamiana, na polisi hapo kituo cha ng'ambo ili yule kibaka akamatwe haraka.


Pengine labda pesa kidogo, kwani Kuna jamaa zangu wanafanya fikra kunikwamua shida sijui ni lini watani bless mana nao mpaka waitane wakae kikao dah
 
Umeibiwa ijumaa, jumamosi ukaamua ujiunge jf.

anyway kwanza hueleweki stori yako inataka nini, mwanzo umeanza kwa huzuni, mara dada akakuvutia ndani, mara ukaja kipande cha kuchanganyikiwa ukaenda kwa trafiki badala ya polisi

umefuata kipande cha userious ukaenda polisi ukapewa mpelelezi, ukafuata sehemu ya comedy ulipoingia kumsaka jini na kumpeleka kwa bibi, yaani hueleweki kiujumla.

anyway mzunguko wa srori yako yote shortcut yake ni mistari mitatu ya mwisho uliyoiandika
Shukran kaka, nime summarize nilihofu maswali ya waja ikabidi nijitahidi kutoa short story ili maswali yasiwe mengi
 
Umeibiwa ijumaa, jumamosi ukaamua ujiunge jf.

anyway kwanza hueleweki stori yako inataka nini, mwanzo umeanza kwa huzuni, mara dada akakuvutia ndani, mara ukaja kipande cha kuchanganyikiwa ukaenda kwa trafiki badala ya polisi

umefuata kipande cha userious ukaenda polisi ukapewa mpelelezi, ukafuata sehemu ya comedy ulipoingia kumsaka jini na kumpeleka kwa bibi, yaani hueleweki kiujumla.

anyway mzunguko wa srori yako yote shortcut yake ni mistari mitatu ya mwisho uliyoiandika
Kama Kuna sehemu hujaelewa sema nikueleweshe mkuu feel free
 
-Tukio limetokea ijumaa iliyopota.
-Mlolongo wa matukio sio wa siku moja ni siku tofauti za kufatana hadi leo.
-Dada alie nivutia ndani ye anadai lengo lilikua kunilinda mana alihisi vibaka wangeogopa kuingia ndani ya fensi ila ikawa tofauti waliingia.
-Jini mweupe ni nck name ya kibaka mmoja hapo bondeni.
 
Yes hii ni I'd mpya ila mi ni wa zamani, sababu kutumia I'd mpya ni kujikinga na mengi Kuna watu wataanza fukua makuburi nikitumia I'd ya zamani, jambo moja likaanzisha jingine, hivo busara nikaona nije na I'd mpya wakuu samahani sana
 
Mkuu fanya faster Log in kwa I'd yako ya zamani😁
Manaake hii I'd mpya unatuchanganya utachelewa sana kupata msaada, manaake inaonekana unahitahi misaada mingi kwenye nyuzi moja
Vizuri kaka, lakini sababu ya kutumia I'd mpya, nikuepuka matatizo zaidi, Kuna watu kazi Yao kufukua makaburi mi Niko tayari nisisaidiwe ila kutumia I'd ya zamani hapana, hapo Kuna rb nineweka Niko tayari kuonana uso kwa uso na mtu ataetaka tusaidizane hili jambo nipo unguja mkuu
 
Back
Top Bottom