Narudi kijijini kulima, maisha ya kwenye jiji la Dar nimeshindwa, nimekubalii🙌🏽

Shukrani kwa ushauri mujaraabu mkuu, umeongea kama vile unanijua, kama best friend dah Shukrani mkuu
 
Robo 3 ya wakazi wa dar kipato chao kinaishia kwenye kodi usafiri na kula tu
 
KURUDISHA MPIRA KWA KIPA SIO MBAYA
BORA UMEKUWA MKWELI NA MUWAZI
KUANZA UPYA SIO UJINGA

DAR USUMBUFU
 
Jitahidi uwahi msimu,bado mbegu na mbolea za ruzuku zinatolewa, Kila lakheri katika maisha mapya
 
Hiì ndio real fasihi uandishi, hakika ujumbe umeifikia hadhira kubwa, intelijensia inaonyesha fanani sio mhusika mkuu kwenye hili bali ujumbe umefika, big up great thinker
 
Majiji yote Duniani yana hitaji uwe na Mzunguko mzuri wa kipato kuweza kuishi maisha ya standard

Ndiyo maana huko Ulaya mtu mmoja unakuta anafanya vibarua hata Ofisi 3 Kwa Siku kuweza kujikimu na maisha ya Mijini.

Kibongo Bongo kuishi Mjini kunahitaji uwe na kipato kizuri pamoja na uwekezaji vinginevyo utaishi Mijini miaka hata 50 lakini ukaishia kupanga na kupata hela ya kula tu 🙌
 
Una Kijiji ? Sababu hata kama kijiji hauna basi utakosa pia hizo basic needs..., kulima haulimi tu unahitaji ardhi na kilimo kingine kinachohitaji mvua na huu ukame unaweza usiambulie hata mbegu..., ingawa kama utakuwa na kijisehemu cha kulima na angalau unapokwenda kuna mvua hata za mara mbili kwa mwaka basi huenda maisha yako yakawa ya furaha.....

 
Jaribu kuishi maisha yako, usiige watu, angalia uwezo wako wa kuzalisha kipato upo wapi halafu komaa, ni vizuri kujijua asili na tabia zako unaweza kufanya nini kikakusaidia wewe na jamii inayokuzunguka.
 

Kikubwa umeshatambua kwamba unapoteza Muda Anza upya kwani kwenye Nia njia hufunguka kikubwa usikate tamaa njia bado ipo ya kifikia malengo mm ni Mmoja ya waliorudi kijijin sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…