Narudi kijijini kulima, maisha ya kwenye jiji la Dar nimeshindwa, nimekubalii🙌🏽

Narudi kijijini kulima, maisha ya kwenye jiji la Dar nimeshindwa, nimekubalii🙌🏽

Kila kitu kina gharama zake.

Hata huko kijijini kwenye kilimo hakuna urahisi kama watu wa mjini ambao hawakuwahi kuishi kijijini hufikiria,hususani mtu mwenye mtazamo kama wako ..kwamba umeshindwa maisha ya mjini umeamua urudi kijijini kulima.

Ukifika kijijini inakubidi ukubali kupokea matokeo yoyote shambani. Mwanzo wa kilimo Huwa mgumu,miezi Sita ya mwanzo inabidi upambane kweli kweli ,kuna muda unaishi kijijini unakosa hata buku mbili,full ukata. Lakini pia hata baada ya kuvuna masoko muda mwingine yanazingua.

Kuna muda mazao ya Biashara kama nyanya,matikiti na vitunguu mnapoamua kuleta mjini kwa mauzo hukutana kutoka mikoa mbalimbali.mfano unakutannyanya ya morogoro,nyanya ya Lindi,nyanya ya Arusha nk,jambo ambako hupelekea bei kushuka sana. Hapa ndipo unakuta mkulima anakimbia mzigo wake maana mzigo auhuziki na mwenye gari uliyemkodi anasubiri chake kama mliambizana mtapeana Hela baada ya mzigo kuuza.

Wakati mwingine madalali wanazingua sokoni. Mzigo unao,ila dalali pale stereo anataka kukulalia.

Ila kwenye kilimo ukikutana msimu mzuri wa hayo mazao unatoboa,maana Kuna kipindi nyanya Moja mjini huuzwa hadi mia 2,kitunguu pia kinauzwa hadi mia mbili,alafu kidogo. Hapa ndiyo unakuta dalali anakupokea na mzigo kama Rais wa nchi na anakupangia gesti Kali Huku akiuza mzigo wako.

Mkuu hii ni nyeupe na nyeusi nakupa maana haya ndiyo maisha ya kilimo unayokwenda kuyachagua.

Nakushauri ukifika huko kijijini,kwa kuanzia wakati unajiandaa na kilimo cha muda mrefu,hakikisha unatafuta eneo la kukodi kandokando na chanzo cha maji kisha unalima bustani za mbogamboga kama mchicha,bamia,nyanya chungu,matembele na majani ya maboga ambazo ndani ya mwezi na nusu unakuwa imeshaanza kutengeneza vihela vya sabuni na kubadilisha dagaa siku ukichoka majani. ( Mfano mchicha kuanza kuandaa matuta hadi kumwaga mbegu na kuvuna hazizidi wiki sita). Uzuri wa mbogamboga hautegemei kupelekea mjini maana hata watu wa eneo lako hapo kijijini watakuungisha mchicha,au matembele au bamia nk.

Mimi nimewahi kuitumia hii mbinu ya kulima bustani za mbogamboga na ilinisaidia sana vihela vidogo vidogo. Vi 10k,20k vilikuwa haviniaumbui. Namwagilia zangu nyanyaau vitunguu unakuta kaja mama anataka umuuzie biringanya au mchicha wa buku. Masisha yanasonga.

Ila kumbuka hii :

"stress is the gape between expectations and reality. The more the gape,the more the stress".

Katika maisha Fanya kazi kwa bidii zote lakini punguza matarajio. Hii point ndiyo imekufanya umepaona mjini jau na hapakufai,umeamua upakimbie. Kuwa makini uendako usije ukapakimbia pia na huko,ukaishia kuyachukia maisha jumlajumla.

Mwenyezi Mungu akubariki sana katika safari yako ya kutafuta uhuru.
Ushauri mzuri sana ndugu, Mungu akamtangulie 🙏
 
Tatizo mnachukulia kuwa kilimo ni chaguo la mwisho baada ya kufeli, kilimo cha hivyo ni kile tu cha kulisha familia.
 
Nenda kalime vitunguu, hata apo ruvu tu unaona wenzako wanajipigia mahela tu
Screenshot_20240327-181243.jpg
 
Kuna uzi wa jamaa wa wilaya ya Tanganyika, Mwese namba 4 humu utafute ukaungane naye. Lakini huko uende na adabu zote kuna akina ngosha ukileta ujinga wa mjini wanakugawana! Kilimo chenyewe kule kinakubali! Ni wewe tu na nguvu yako ya kufyeka mapori!
Unaitwaje huo uzi mkuu?
 
Wakuu natumai mko poa kabisa
Mimi ni kijana ambaye nimeamua kuwa muwazi kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.

Jiji la Dar es Salaam limenishinda, Nimekubali na sitaki tena maisha ya jiji lolote. Sina degree, diploma wala cheti chochote, pesa yote niliyokuwa najichanga mwisho wa siku inaishia kwenye Kodi, umeme, maji, usafi, ulinzi, taka, chakula, na kulipa madeni. Sasa huu mchezo nimeuchoka. Maana hii ni mark-time, hakuna chenye nna fanya, hata zile raha za jiji wanazozisema sizifaidi maana nikisema nitenge 30k au 50k nikale Bata, ohoo nimeishaa...siioni future kabisa.

Hivyo wakuu nimeamua kwenda kijijini kushika jembe kulima kwa bidii na uaminifu, na kuishi maisha ya chini kabisaa...maisha yangu ikibidi niyamalizie huko huko kabisa. Kusali, kulima, kula, kulala ivyo yaan.

Kwahiyo wanajukwaa naombeni kwa ambaye ni mkulima au anamashamba huko vijijini, au ni mwenyeji wa mikoa ya kilimo sana na ameelewa hali yangu naomba anipokee , hata kama hakuna umeme, au nyumba ya kulala...nipo tayari kulala hata kwenye mahema nje humo humo mashambani endapo hakuna wanyama wakali lakini.

Hata kama sitalipwa pesa yoyote, ilimradi nipate chakula na niwe na amani ya moyo inatosha kabisa. Maana jiji limeninyoosha.

NB: Sijayakatia tamaa maisha, nimelikatia tamaa jiji.

Asanteni sana kwa maoni na michango yenu mnayoenda kuitoa.

Mungu azidi kutupa Amani na Upendo na Mshikamano.
View attachment 2945601
Wakati we unatoka wenzio wanaingia! Ni sawa bye bye
 
stress is the gape between expectations and reality. The more the gape,the more the stress".
Kabisa mkuu.
Kuna muda unafika inabidi upange mipango kulingana na kipato, ustarehe kulingana na kipato pia.

Jamaa anadhani kula bata ni mpaka awe na 50k wakati 15k anaweza kuifurahia vizuri tu.

Tatizo vijana wengi wanaiga, wanapenda kufake mpaka furaha ili watu waone anaishi vizuri, sijui hii hua inawafaidisha nini nafsini mwao.
 
Back
Top Bottom