Akili 09 Nguvu 01
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 695
- 1,377
Mnamo mwezi wa 12/2018 na Januari 2019 niliingia kwenye kilimo cha Nyanya. Nikiri kua nilikua sina maarifa wala uzoefu wowote kweny kilimo cha nyanya. Kuna rafiki yangu mmoja ndo alinishauri na kunishawishi kuingia kwenye kilimo cha nyanya(alinichukua na kunitembeza kweny mashamba ya nyanya na niliona jinsi watu walivyofanikiwa kupitia kilimo cha nyanya) hivyo nilishawishika vilivyo
Tulikubaliana tulime shamba la pamoja kwa kushirikiana na kushare gharama sawa kwa sawa. Tulikodi shamba na tukalima kwa trekta, baada ya wiki moja tu tangu kulima uyu rafiki yangu akapata kazi nyingne mkoa mwingine. Hivyo nikabaki peke yangu nikilisimamia shamba.
Nilienda vijijini nikatafuta vijana wa kazi nikawapeleka shamba shughuli iliendelea. Hapa nikiri kua gharama zote za shamba nilitoa mim uyu rafiki yangu ni kama alinisusia shamba(kumbuka tulilima shamba kubwa kama hekari 1.25 ivi kwa minajili ya kushare gharama)
Kufupisha stori
Katika kilimo hiki nyanya zilipofikia hatua ya kukomaa ziliingiliwa na ugonjwa wa wadudu na mnyauko hivyo mwisho wa siku sikuvuna hata ndoo moja ya nyanya. Pia vijana waliokua wanahudumia shamba wamenifelisha kwa kiasi kikubwa
Nilivopiga hesabu nilikua nimetumia zaidi ya Milioni 2 lakini sikuvuna kitu
Sijakata tamaa
Mwaka huu 2020 nimerudi tena kweny kilimo cha nyanya, saizi nna maarifa na uzoefu kidgo pia nmemtafuta mwenyej mzoefu nashirikiana nae, mim natoa gajarama yeye katoa shamba na nguvukazi yake. Kama mambo yakienda vizuri nategemea mwezi wa 4 nyanya zitakua tayari
Tukutane mwezi wa 4 kwa ajili ya mrejesho wa mavuno