Nakuomba uanze kuwepo shamba kuanzia siku ya kuweka mbegu kwenye kitalu na siku za kupandikiza, na kila siku kukagua afya ya mimea kwenye magonjwa na mahitaji ya mbolea.
Kwenda shamba kwa wiki mara moja au mbili tu utarudi hapa kuniambia nilikuwa sahihi.
Hakikisha unajua vipimo vyote vya matuta au vitalu, kati ya shina na shina, aina bora za mbegu na ukanunue mwenyewe, pia uhakikishe zinamwagwa zile ulizonunua, kifupi uwepo kila hatua.
Siwezi kuandika mambo unayoweza kutendewa kwa uzembe wa msimamizi, shamba boy, mshirika wako au kupigwa ni mengi sana kwa namna tofauti, siwezi kuandika hapa nitakuchosha.
Hao watu wa shamba wote wanafanana mizengwe yao karibu mikoa yote Tanzania, trust me.