Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nimeamua nikazeekee kijijini kwa sababu zifuatazo:-
- Kule kijijini nitapata hewa safi isiyokuwa na mchafuko
- Kule kijijini nitapata majirani wema wasiokuwa na choyo
- Kule kijijini tutakuwa tunatembeleana bila chuki
- Kule kijijini tutakuwa tunakunywa togwa pamoja
- Kule kijijini tutapunguza msongo wa mawazo
- Kule kijijini tutaingia shamba lolote kuchuma matunda na kula
- Kule kijijini tutakuwa tunasikia milio ya ndege na viumbe mbali mbali
- Kule kijijini tutafurahia uoto wa asili
- Kule kijijini tutakuwa tunaenda kuwinda kama sehemu ya michezo
- Kule kijijini tutapata marafiki wengi ambao sio wanafiki
- Kule kijijini tutakuwa tunatembeleana panapotokea mmoja wetu anaumwa.
- Kukaa kwenye nyumba ya nyasi yenye hewa safi na ya kuvutia
- Kula vyakula vilivyopikiwa kwenye vyungu na kuwa na ladha nzuri
- Kendwa kuogelea mitoni na kuvua samaki kama sehemu ya michezo na uwindaji
Kwa ujumla maisha ya kijijini yatakuwa ni mazuri sana
Kwa nyie mnaobaki mjini, nawaachia mpambane na:-
Kwa nyie mnaobaki mjini, nawaachia mpambane na:-
- Majungu na fitina zenu
- Mchafuko wa hali ya hewa
- Jua kali
- Msongamano wa watu
- Makelele ya baa na kumbi za starehe zinazoharibu utulivu wa ubongo
- Misongo ya mawazo kutokana na changamoto za kimazingira
- Kudharauliwa na vijana
- Kununua kila kitu; nyanya, yai ,mchicha n.k
- Kutokuwa na marafiki wa kweli
- Kila mmoja kumuona mwenzie fursa
- Kuzeeka kabla ya umri wako
- Kupata magonjwa ya moyo na presha n.k
- Kula vyakula vyenye kemikali katika kukuzia au usindikaji
Fanya maamuzi mapema; njoo kijijini tukawinde kanga pori, sungura, n.k pamoja na kuongeza miaka mingi ya kuishi.