NASA imesema imechelewa sana kuzuia Mawe makubwa yatakayotua Duniani

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240


Taarifa ya kuogopesha kuhusu Jiwe kubwa aina ya Asteroid kuweza kutua Duniani na kuhalibu Jiji kwa Ukubwa wake imetolewa na mwanasayansi akisema Nasa imechelewa kuzuia jiwe Hilo.

Inawezakana ukafikiria labda ni movie za Hollywood kuhusu Scifi Filamu kuhusu Jiwe kuhalibu maeneo ya watu ila hii ni Uwalisia Kuna jiwe kubwa linashuka Duniani na litaweza kusababisha Uharibifu mkubwa kwenye eneo litakalo tua.



Jiwe Hilo kubwa limepewa jina la 2024 YR4 liko njiani kushuka Duniani, likiwa na ukubwa sawa na sanamu la statue library, yenye ukubwa wa futi 130 mpaka 300 sawa na Mita 40 na 90 kulingana na ripoti ya Daily Mails.

mwandishi na mtaalamu wa volkano anayeishi London Dakt. Robin George Andrews. Alisema huenda tusiweze kuzuia kabisa jiwe kubwa hili kuweza kushuka Duniani kwani tuko chini ya miaka 8 ya kuweza kukabiliana nalo kupitia mtandao wa X aliweza kusema.



Aliongezea kwa kusema kupanga na kuthibiti hii asteroid 2024 YR4 ni zaidi ya miaka 10 lakini sasa linakaribia kushuka Duniani tuna chini ya miaka 8 hivyo tumeshindwa kulipoteza Tuombe tu Madhara yasiwe makubwa.
 
Hapo wanataka kuongezewa BAJETI tu wapige mpunga hawana lolote ,kama vimondo vilidondoka duniani sembuse hilo JIWE? Haliwezi kufika duniani bila kusambaratika.

Kama wanataka fedha waombe tu na si kutishia watoa PESA.
 
Kama ukubwa wa hilo jiwe anga ni sawa na statue of liberty, then kwa mtazamo wangu sioni haja ya kuwa na shaka maana ni dogo ukijumlisha hata likiweza kuingia kwenye gravity ya dunia litaishia kusambaratika kiasi...
 
Tusitishane maisha
 
Nina hakika Jumamosi lazima litatua
 
Wewe mbona umepitwa na wakati hivi, hili jiwe limeshaonekana kuwa halitaipiga dunia 2032.

Fuatikia habari za sasa, usiweke habari za zamani.

Na ukiweka habari za NASA, weka link ya source.

Ama sivyo tutakuona muongo unataka kutisha watu tu.

Soma hapa.

"Latest Calculations Conclude Asteroid 2024 YR4 Now Poses No Significant Threat to Earth in 2032 and Beyond"

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…