NASA watangaza kampeni ya kumuapisha kiongozi wao Raila Odinga na Kalonzo Musyoka tarehe 30 Januari 2018

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Viongozi wa Muungano wa Upinzani nchini Kenya (NASA) wametangaza kampeni ya kitaifa kuhamasisha wafuasi wao kujitokeza kwenye sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka tarehe 30 ya mwezi huu.
 
Kuna hatari inakuja maana serikali itawakamata kwa uhaini, then what next? Jeshi linaweza kugawanyika, what next likigawanyika? Raila anaungwa mkono na Jeshi? if yes, what next? Kenyatta anaungwa mkono na jeshi, if yes, what next?
 
vita
 
Kuna watu wanaamini kuwa Odinga kuna siku atajiapisha kuwa rais hewa wa Kenya.....!

Hilo jambo halipo,Odinga mwenyewe anajua urais ambao angeweza kuupata ni wa chuo,kampuni au taasisi nyingine na si nchi.

Odinga anajijua fika kuwa yeye ni ngazi ya kupandia wanaoutaka urais,hata Kalonzo analijua hilo ndo maana amemganda Odinga.
 
Kuna hatari inakuja maana serikali itawakamata kwa uhaini, then what next? Jeshi linaweza kugawanyika, what next likigawanyika? Raila anaungwa mkono na Jeshi? if yes, what next? Kenyatta anaungwa mkono na jeshi, if yes, what next?
Hakuna hata mwanajeshi mmoja anayemuunga mkono Raila. Hata kurutu! Mi naona wangeacha tu ajiapishe, afu tuone kioja kitakachofata. Ataenda wapi baada ya hapo? Labda kwa mkewe akale sima kwa mchuzi wa dagaa.
 
Kenya bado kunatatizo
kuna bomu lina subiria kupasuka
Pwaaaaaaa
 
Wanao kufa ni watoto wa maskini wao wanakuwa nyuma mara hii nadhani wao watatangulia mbele yetu macho
 
Hatimaye Kenya itakua na marais wawili

Tubadilishe kwa miezi sita tu Rais Magufuli awe Rais wa Kenya na Rais Uhuru awe Rais wa Tanzania!!!!!![emoji1][emoji1][emoji1] Magufuli angewanyoosha wale ambao wanatamba eti wanaapisha Rais bandia wa Kenya na wakati huohuo Rais Uhuru angekuwa kana kwamba yupo likizo Tanzania. Pawe na MOU au Kagame Aende Kenya kuwa Rais kwa kipindi hicho na Uhuru awe Rais wa Rwanda!!!!
 
Magufuli hawezani na Uchumi wa Kenya atazubaia maendeleo yaliyomo asahau kilichomleta Kisha angatuliwe upesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…