Hamna kitu nafurahia zaidi katika OP hii kama nikisoma kua ghala za silaha kutoka Magharibi zimelipuliwa na makombora ya Urusi.
Nafurahi sana kwa kweli.
Furaha yangu ni kwamba,silaha hizo ndio zinaleta mateso kwa Wananchi wa Ukraine maana zingefika field zinasababisha vita iwe ndefu TU.
Pili furaha yangu ni kuwatia hasara wa NATO TU.
Tatu. Ni kwadhalilisha USA na NATO.
Nne kwa vile maghala hayo huweka silaha zote za west kwa ajili ya kuzipeleka front basi nafurahi Kisha ikibtu kua pengine kombora moja au mbili au tatu TU za Urusi zimeteketeza masilaha kibao ya west. Yaani ni Raha Fulani TU hivi.
Kwa kifupi katika maisha ya NATO,NATO haikuwahi kukutana na mtihani Mgumu kama huu amabao imeshindwa hata ku attempt hata swali moja.
NATO inapitia katika kipindi kigumu mno.
NATO inadhalilishwa na inadhalilika.
NATO inateswa na inateseka.
NATO inasimangwa na inasimangika.
Iko wapi Ile NATO iliyoipiga mabumu Yugoslavia,
Iko wapi NATO iliyoipiga Iraq ya Sadam Husein na operation Desert storm?
Iko wapi NATO iliyowasaidia waasi kumtoa Muamar Gaddafi?
Iko wapi NATO iliyoenda Afghanistan kuwapiga watalaban walioongizwa na Mullah Omar Mohamed na Rafiki yake Osam bin laden?.
Leo hii Nchi ya Ukraine kipenzi Cha west na NATO amabyo,Rais wake anapewa nafasi ya kuhutubia mabunge ya nchi zote za west, na Blocks zote za west anapigwa na Urusi mchana na usiku,miundombinu inaharibiwa lakini west wako madirishani wanachungulia TU.wanaishia kukaa vikao Kila kukicha kuchangishana vijisilaha na fedha, lakini kuingia moja kwa moja kama walivyo fanya kwa mataifa mengine hawaingii.mafano Kuwait,Iraq, Afghanistan, Yugoslavia na Libya.
Iko wapi NATO hiyo?