Naseeb Abdul maarufu kama 'Diamond' ashikiliwa na Polisi kwa muda

Naseeb Abdul maarufu kama 'Diamond' ashikiliwa na Polisi kwa muda

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,015
Reaction score
2,680
MSANII Naseeb Abdul (Diamond) leo anashikiliwa na polisi, siku moja tu baada Meneja wake Babu Tale kuhojiwa na kulala mahabusu kuhusiana na matumizi ya mavazi ya kijeshi katika onyesho la Fiesta mwishoni wiki.

Habari zaidi zitafuata.

diamond3.jpg


=======================================================================================


Diamond akabidhi ‘kombati'


Kwa ufupi
Ni baada ya kuzua mzozo na vyombo vya dola kuhusu mavazi yake wakati wa maonyesho mwishoni mwa wiki.

Dar es Salaam
Mwanamuziki Nassib Abdul, ‘Diamond Platnumz' amesalimisha nguo zake za kijeshi kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Diamond alisema kuwa juzi alipokea wito uliomtaka afike kituoni hapo (Oysterbay) akiwa na madansa wake pamoja na nguo hizo. Alisema haikuwa rahisi kwake kutii amri ya vyombo vya dola kwani alikuwa na woga kutokana na kutokuwa na rekodi ya yoyote ya matukio ya uhalifu.

"Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana na ya jeshi na hayakuwa sare rasmi za jeshi hilo, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo," alisema nyota huyo aliyetajwa kuwania tuzo za MTV EMA zinazotarajiwa kufanyika Novemba 9 mjini Glasgow, Scotland.

Diamond alisema si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na Chifu Kiumbe, ila ukweli ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa nchini kama kaka yake kutokana na woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa dhamana yoyote.

"Awali, meneja wangu (Hamis Tale) alishikiliwa kwa muda na mimi nikatakiwa kufika na zile nguo nikiwa na dansa wangu ambao na wao walivaa pia, nilifanya hivyo na nikafika pale na kuziacha nguo baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika," alisema.

Diamond alijikuta akiingia kwenye matatizo na Jeshi la Wananchi (JWTZ) baada ya kupanda jukwaani Jumamosi katika onyesho la Fiesta akiwa amevalia nguo zinazofanana na sare za jeshi hilo.

Hata hivyo, Diamond alisema mavazi yale aliyoyavaa siku ile katika tamasha la Fiesta, hayakuwa ya JWTZ kama inavyodaiwa, bali aliyanunua alipokuwa kwenye ziara yake nchini Ujerumani mwezi uliopita.

Wakati huohuo, Diamond ni miongoni mwa wasanii waliopangwa kutoa burudani katika Siku ya Msanii itakayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, kesho.

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Siku ya Msanii 2014 inayoandaa sherehe hiyo, Peter Mwendapole alisema Diamond ataungana na Yamoto Band katika kutoa burudani siku hiyo.

"Maandalizi yote yameshakamilika na leo hii namtambulisha kwenu msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Diamond kuwa ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza katika sherehe hizo pale Mlimani City akiwa sambamba na kundi la Yamoto," alisema Mwendapole.

Kwa upande wake, Diamond amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na tasnia ya sanaa hapa nchini na pia kuwaenzi wasanii wao.

CHANZO: Mwananchi
 
MSANII Naseeb Abdul (Diamond) leo anashikiliwa na polisi, siku moja tu baada Meneja wake Babu Tale kuhojiwa na kulala mahabusu kuhusiana na matumizi ya mavazi ya kijeshi katika onyesho la Fiesta mwishoni wiki.

Ukicheka na mbwa atakufuata msikitini! hawa kina Diamondo and the so called No school billioneas; mamlaka zikicheka cheka nao sana haya ndio matokeo; kanafikiri nchi iko mfukoni mwake. kama CDM kuandamana ni kuvunja sheria basi kuvaa sare za jeshi ni kuvunja sheria pia tumeambiwa hivyo, sasa hebu tuone kama PoliCCM watamgwaya "prezida" wa bongo flava!
 
Wanafanya nae maongezi tuu watamuachia muda si mrefu!
 
ila sheria znaruhusu endapo alikuwa na kibari nothng to judge kuhusu ilo
 
watamwachia tu , yeye ndiye aliyemfanyia kampeni jk mwaka 2010 kwani ccm walimlipa . nawashauri jwtz wampe kwanza virungu
 
acheni uongo nyie... alipewa kibali... kumchafua tuu ndo mjuavyo
 
Back
Top Bottom