Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Heshima kwako pia Lizarazu!Keyon.
Nakupa salute kwa udadavuzi wa mambo haya, sio wote wanayajua hivi hata kwa wale wanaofuatilia.
Nadhani hata mashabiki wengi nao pia wamechangia kuwaharibu/kuwabadirisha wasanii wa hip hop bongo... Hip hop ya mwanzoni mwa 2000 ilikuwa imesimama kuliko hata bongo fleva na hata bongo fleva wenyewe walikuwa wanakaaa kwa wasanii wa hip hop.
Sababu ni nini!!! Msanii aliangalia ni jinsi gani kitakubalika katika jamii kwa watu wa aina zote, lakini Leo hii msanii anatoa kitu huku akilenga nyimbo itamuingizia shingapi haijalishi hata kama kuna watu wataona ni ya kipuuzi.
Na ndio maana hata watu kama Joh, Chege,Jaffarah sio wale wa kipindi kile tena...!! wamechange.
Hip hop siku hizi ni burudani na sio sehemu ya kufikirisha ubongo.
Si unaona hata huu Uzi ulivyokosa wachangiaji lakini ingekuwa ni nyimbo ya weusi imetoka ungefika hata page 20+.
Hehe jioni ya saa ngapi!!manJioni nitakuja na uchambuzi wangu.
Umeharibu Kiswahili katika kichwa cha habari yako - ni KUUSIKILIZA WIMBO WA na sio KUISIKILIZA NYIMBO YA....Habari zenu wanajukwaa
Binafsi kila nikisikiliza wimbo wa Nash Emcee uitwao Shujaa.
Namuona Dk.slaa.
wewe unamuona nani ?
noma ili dude ninalo simuniAsiyehusika na hipHop, atokeee !
-Kaveli-
Heshima kwako pia Lizarazu!
Kipindi cha nyuma kweli hip hop ilifanya vyema Tofauti kidogo na sasa!
Jambo la kutia matumaini tuna Mwanaume(Nash) Mimi napenda kumuita "The black scorpion"-West war...anafanya jitihada ya kuwaweka watu katika mistari ulionyooka!
Ukumbuke kabisa 99% hip hop haitaki Unafiki kama rangi nyeusi inakubidi useme ni nyeusi na sivinginevyo! Jamii kubwa Duniani huwa hawapendi kuambiwa ukweli mtazame Yesu mnazaleti (Biblia) alivyopata taabu sana kwa watu enzi zile kisa kusimamia ukweli na aliupinga na kuukemea unafiki!
Labda naweza nikasema Dunia imebadilika au kizazi hiki cha leo kimebadilika-kipaumbele starehe/fake life!
Katika swala la soko naona wengi Ndio wanateteleka na kukosa msimamo hapo ndipo heshima zote nazipeleka kwa Zuzu!
Nimalizie ni hii katika nyanja zote za Maisha-No matter how good your you can be replaced!!!!
Mkuu Keyon mambo niaje...!?
Hip hop ya kipindi cha nyuma ilikuwa ni mwiko kuskia ikichezwa disco labda hakuna kulala ya Juma nature, muziki wa kipindi kile ulikuwa ni muziki fikirishi na ndio maana hadi wakaleta shindano la mfalme wa rhymes ambalo kwa bahati mbaya sana halikudumu.
Nash mcee, incredible,Kadugo na Mbishi hawa kwangu ndio wasanii wa bongo wanaoutendea haki genre ya hi hop na kuifanya iendelee kuwa hai...Fid nae siku hizi namuona ameanza kufuata nyayo za weusi! Yaani anafanya nyimbo ambayo itakaa kwenye top 20 kwa muda mrefu na sio ambayo itawafikirisha watu kwa muda mrefu na radha isiyoisha.
Tuko katika zama ambazo anasa imeshika kasi kuliko kawaida na ndio maana hata maudhui ya kazi nyingi za kisanaa yameelekea huko. Ndio maana mimi muda mwingi huwa napenda kuskiliza old school tracks tu sababu zina radha isiyoisha tofauti na hizi za kuota mapembe na kuongezana mkia.