Habari wadau!
Ushauri wangu kuna watu wanaweza kuupuuza! Lakini itakuwa na maana tukijadili humu kwa pamoja!
Hakuna aliyesalama hata ukijihesabia haki kwa utajili/cheo na Mali ulizo Nazo.
Huko barabarani hata viongozi hupatwa ajali, hata matajili hupatwa ajali, wachungaji hupatwa ajali n.k
HIVYO KUPEWA MSAADA NA JAMII NI LAZIMA
usalama wetu upo mikononi kwa wenzetu!
Jeshi la polisi kitengo cha trafiki kwa kushauriana na wizara ya afya!
Waweke ulazima wa kila chombo cha moto kitumiacho barabara kuwa na kiboksi kidogo chenye GLOVES na nylon nyembamba!
Hili litasaidia sana wananchi kutoa msaada wa haraka kwa majeruhi punde ajali inapotokea kwa kutokuogopa damu za majeruhi.
Majeruhi wa ajali wamekua wakikosa misaada kwa wakati kutokana na watu kuogopa kushika damu!
Hata wenye magari ya kujitolea wengi huhofia magari yao kuchafuka kwa kuwa hakuna kapeti laini la kutanguliza ili kumlaza majeruhi
Haya ndiyo mambo ya msingi sana kwa trafiki kukagua kila chombo kuliko hata stika ya nenda kwa usalama!
Viwembe, spirit I au painkiller vinaweza kuhitaji muda lakini majeruhi hahitaji muda kupelekwa hospital!
Wizara ya afya pia inaweza kuliboresha zaidi hili kwa kuwatambua watu waliojitolea vyombo vyao vya moto kubeba majeruhi!.
Wanaweza kutoa hata motisha hati ya utambuzi ili mtu huyo imfae kupewa punguzo la bei endapo siku akihitaji huduma kwenye hospital!
Hospital iondoe dalili za usumbufu wowote unaoweza kukatisha moyo wa kujitolea n.k
Kila mtumia barabara ni mhanga! Hili linatakiwa lisimamiwe kikamilifu na jeshi la polisi barabarani ili kurahisisha wahanga kupata huduma!
Ajali inapotokea pikipiki, magari wakitoa gloves na kapeti msaada utapatikana haraka kuliko sasa watu hutegeana! Au mpaka wamjue kwanza majeruhi ndipo hujitolea!
Pia traffic wa eneo au njia husika wawe wa kwanza kufika kwenye tukio na wakichelewa wawajibishwe! Haiwezekani penye dili wawahi lakini kwenye tukio wachelewe! Mali za majeruhi zikipotea walipishwe trafiki wa eneo hilo ili kuwawajibisha!