Omary Sameer
Member
- Oct 17, 2018
- 6
- 9
Ni muda mrefu tangu niameanza kusikiliza kipindi cha Ushauri wako cha Redio Free Africa ambacho maudhui yake ni kama vipindi vingine vingi ambavyo lengo lake ni kuwasaidia watu wenye matatizo na uhitaji wa hali na mali.
Lakini licha ya kusikiliza pia hivyo vipindi vingine, kuna kitu cha utofauti nakiona kwenye kipindi anachokisimamia mwanamama huyo.
Akiwa amejikita zaidi kwa wanawake ambao wamekuwa na matatizo mengi ya kiafya kwa wanawake ambao kwa bahati mbaya ama wanakuwa wajane ama hata kukimbiwa na waume/wazazi wenzao;
Pia wapo waliopata matatizo hayo kutokana na ukatili wa kijinsia waliofanyiwa na wanajamii wenzao ama hata waume zao.
Wengine wamejikuta wakipitia magumu kutokana na ama kuzaliwa na ulemavu, kupata ulemavu ukubwani ama hata kujifungua watoto wenye tatizo fulani la kiafya ama ulemavu.
Nimejaribu kukaa katika nafasi yake huyo mtangazaji nahisi ni mtu ambaye huenda hata kipato chake huishia kuwapa msaada wa awali watu ambao anawaalika kwenye kipindi chake kwani ni wengine nahisi bila msaada wa awali hata kipindi hakiwezi kikaenda sawa.
Nashauri kama jamii tumpe tunzo huyu mwanamama ama hata kumfungulia mfuko ambao utahusisha kuwasaidia watu hao wenye uhitaji au hata kutoa bima ya afya kwa watu wanaopitia katika kipindi chake na vingine vingi vinavyofanana na hicho......
Naomba kuwasilisha