Nashauri kila basi la masafa marefu liwe na mtaalam wa afya

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,013
Reaction score
1,183
Habari Tanzania !

Napenda kutoa wazo kwa Serikali kuhusu kuzilinda afya za abiria wa masafa marefu ikiwapendaza iwekwe amri kwa kuyataka Mabasi yote yanayofanya safari za masafa marefu yawe na mtaalamu aidha 1 au 2 kwa kila gari kwa ajili ya huduma ndogo ya afya.

Hii itachochea kulindwa kwa afya za abiria, dereva na wasaidizi wake panapotokea changamoto katikati ya safari au hata kivyovyote kati hali yoyote pawepo msaada wa kiafya.

1. Kila basi la abiria liamuliwe liwe na "Huduma ndogo ya matibabu kwa abiria, dereva na wasaidizi wake"

2. Pawe na vifaa vya huduma na madawa kwa ajili ya huduma ya kwanza kwa kila basi.

3. Pawe na utoaji elimu kuhusu afya wakati wa safari.

NB

Hii iende sambamba na usafiri mwingine mfano, Ndege za abiria, meli au vivuko vya majini.

Karibuni.
 
Itapendeza, tutaongeza ufanisi na kuboresha huduma za usafiri hapa nchini.
 
Kitaifa kila muuguzi mmoja anahudumia watu 5000, kuna mikoa mhudumu mmoja anahudumia hadi watu 30,000 utawapata wapi wahudumu kila gari?

Wazo lako halitekelezeki sababu ya gharama,haya mambo ya huduma ya kwanza na personal hygiene yanafundishwa kuanzia shule ya msingi,sekondari mpaka vyuoni.Tatizo tunachukulia mzaha huko yanapofundishwa.Leo hii ukiwasha TV yako ukaona kipindi kuhusu huduma ya kwanza unatoa unaweza Music Wasafi. Ni msisitizo wa mambo madogo tu unaepusha mengi,kunawa mikono,kula chakula cha moto,kunywa maji safi na salama n.k. Kama una mgonjwa anasafiri hakikisha yupo na ndugu anayejua hali yake vizuri,usiwape abiria wengine heka heka. Mabus mengi yanakuwa na first aid kit,kwa dharura ndogo ndogo za kuharisha inatosha sana,labda sasa wahudumu wapewe mafunzo ya mara kwa mara.
 
Lakm, kwa uelewa wangu wa darasa LA 3c naona Tz kuna vyuo vingi sana vya afya na wahitimu kuanzia ngazi ya cheti wapo wengi sana kulinganisha. Na idadi ya mabasi ya Masafa marefu
 
Ndo hawatoshi, kama average ni mhudumu mmoja kila watu 5000 mpaka 30,000 ina maana wahudumu ni 2000 mpaka 12,000
 
Habari Tanzania !

Napenda kutoa wazo kwa Serikali kuhusu kuzilinda afya za abiria wa masafa marefu ikiwapendaza iwekwe amri kwa kuyataka Mabasi yote yanayofanya safari za masafa marefu yawe na mtaalamu aidha 1 au 2 kwa kila gari kwa ajili ya huduma ndogo ya afya.

Hii itachochea kulindwa kwa afya za abiria, dereva na wasaidizi wake panapotokea changamoto katikati ya safari au hata kivyovyote kati hali yoyote pawepo msaada wa kiafya.

1. Kila basi la abiria liamuliwe liwe na "Huduma ndogo ya matibabu kwa abiria, dereva na wasaidizi wake"

2. Pawe na vifaa vya huduma na madawa kwa ajili ya huduma ya kwanza kwa kila basi.

3. Pawe na utoaji elimu kuhusu afya wakati wa safari.

NB

Hii iende sambamba na usafiri mwingine mfano, Ndege za abiria, meli au vivuko vya majini.

Karibuni.
Kinachohitajika hapo ni sanduku la huduma ya kwanza.. Kusafiri na mtaalam wa afya ni jambo lisilowezekana kwakuwa hata ikitokea dharura hataweza kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa ukosefu wa vifaa
 
Una maanisha nan atawalipa hao wauguzi watakaoajiriwa kweny mabasi?mwenye KAMPUNI au Government
 
Ndo hawatoshi, kama average ni mhudumu mmoja kila watu 5000 mpaka 30,000 ina maana wahudumu ni 2000 mpaka 12,000
Mkuu,mm naona wewe unatumia uwiano kwa idadi ya wanajamii wanaohitaji huduma na wataalamu walioajiriwa ,lakn safari za masafa marefu nafikiri basi zake ni chache pia (sna uhakika) hivyo wangetafuta wale graduates wa afya hata cheti ndo wawaajiri kwenye mabasi kama hostess.
 
Mikoa 31, kama kila mkoa una basi 50 tu tayari ni mabasi zaidi 1000, kuna mabasi kwa maelfu mkuu hayo masafa marefu. Kuna
 
Kwani kimekukuta Nini mkuu ukiwa katika Basi?
Watu wengi sana wameshapata shuhuda na wanauzoefu wa kupata changamoto za kiafya kabla, wakati na baada ya safari. Kwao au kwa abiria wenzao.
 
Utakua unawalipa wewe?
Bro jaribu kufikiri mara mbili na kama hufahamu kuna aina nyingi za malipo. Mfano, malipo kwa masaa, malipo kwa siku, wiki au mwezi. Nina imani hakuna mfumo wa malipo usiowezekana hapa duniani.

NB

Katika hili tutachochea sana hizi biashara kwenda kwa uzuri na ufanisi.

Karibu.
 
Wazo lako halitekelezeki sababu ya gharama,haya mambo ya huduma ya kwanza na personal hygiene yanafundishwa kuanzia shule ya msingi,sekondari mpaka vyuoni.Tatizo tunachukulia mzaha huko yanapofundishwa.Leo hii ukiwasha TV yako ukaona kipindi kuhusu huduma ya kwanza unatoa unaweza Music Wasafi. Ni msisitizo wa mambo madogo tu unaepusha mengi,kunawa mikono,kula chakula cha moto,kunywa maji safi na salama n.k. Kama una mgonjwa anasafiri hakikisha yupo na ndugu anayejua hali yake vizuri,usiwape abiria wengine heka heka. Mabus mengi yanakuwa na first aid kit,kwa dharura ndogo ndogo za kuharisha inatosha sana,labda sasa wahudumu wapewe mafunzo ya mara kwa mara.
Utajisikiaje ukikutana na mtoa huduma wakati wa safari ya masafa marefu? Nina imani utapata ustahimilivu na utosherevu wa safari yako.
 
Kinachohitajika hapo ni sanduku la huduma ya kwanza.. Kusafiri na mtaalam wa afya ni jambo lisilowezekana kwakuwa hata ikitokea dharura hataweza kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa ukosefu wa vifaa
Tafiti Usafiri wa Treni ya TRC miaka nyuma, ilikuwa na watoa huduma ambao ni manesi na madaktari wakati wa safari. Abiria anasafiri kwa uhakika, amani na usalama.

Hii itapendeza.
 
Back
Top Bottom