Nashauri kila mwana JF asome vitabu vya Neuroscience

Nashauri kila mwana JF asome vitabu vya Neuroscience

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Habari wakuu,

Kuna wakati nilihitaji kujua lwanini kampuni ya cocacola inawatumia watu maarufu duniani kutangaza bidhaa zao tena inawalipa mabilioni ya pesa, nkatamani kujua hayo matangazo yanamshawishi vipi binadamu anunue cocacola, nkajiuliza kwanini wakati Cristian Ronaldo anaongea na wanahabari kwanini chupa za cocacola huwekwa mezani ? Je kuna mechanism gani inayomshawishi mimi niliyeko huku bongo ninunue cocacola?
Jibu ni kwamba IF YOU LIKE CHRISTIAN RONALDO, AND CHRISTIAN RONALDO LIKE COCACOLA, YOUR BRAIN WILL UNCOUNSCIOUS LIKE COCACOLA THAT TIME YOU THINK ABOUT CHRISTIAN RONALDO,

wakuu mtanisamehe kwa kuchanganya lugha, Basi nikaanza kusoma vitabu mbali mbali ni jinsi gani matangazo humshawishi binadamu, nikajikuta naangukia kwenye kutaka kujua what is mind? Where is it located in the human body? baada ya kusoma sana vitabu nkajikuta naangukia kwenye kutaka kujua WHAT IS MEMORY? how is it stored in thehuman brain, and by which mechanism? Why we remember and forget other things? Baada ya kuingia kwenye hilo swali nkasoma sana vitabu nkajikuta naangukia kwenye somo linaloitwa NEUROSCIENCE.

Kiufupi nmejifunza mambo mengi sana, nimepata majibu ya maswali yafuatayo,
  1. Kwanini mashabiki wa simba au Yanga hufurahia na kuruka ruka kama watoto pindi timu zao zinapo funga goli, mechanism inayoperekea wao kuwa hivo ni ipi?
  2. Kwanini mtu mwingine hawezi hata kuangalia kidonda cha binadamu ila kuna mwingine anamuua mtu kwa kumkata kata na mapanga, mwingine anamchoma mpenzi wake na moto wa petrol kisa wivu what is the mechanism behind?
  3. Kwanini unaposikia mziki mzuri unajikuta unakata mauno na kifurahia kama mtoto what is the mechanism behind?
  4. Kwanini watu wengi wanapokuwa na mawazo hukimbilia kunywa pombe na pombe zikiisha kichwani mawazo huanza upya what is the mechanism behind?
  5. Kwanini mtu akasirike mpaka kufikia hatua ya kupigana kisa umemtankia tusi ambalo ni neno tu moja what is the mechanism behind?
  6. Kwanini wanaume wakiona kiungo cha mwanamke kama vile mapaja, makalio n.k hujikuta wanapata hisia za mapenzi hata kama wana akili timamu what is the mechanism behind?
KWa wasio jua majibu ya hayo maswali watasema Mungu ndio anajua, lakini wenzetu hawakuwa wavivu walifanya tafiti usiku na mchana wakapata majibu ndio maana wanatucontrol kwa kutumia maarifa waliyonayo
HIVI SASA WATU WANAUZIWA MIDOLI YA KUFANYA NAYO MAPENZI kwa sababu mtengenezaji anajua how the human brain works!

Ninawawekea baadhi ya vitabu msome nanyi mfunguke akili

1. Meet your happy chemicals
Screenshot_20210808-131048_Adobe Acrobat.jpg

2. Cognitive neuroscience
Screenshot_20210808-131714_Chrome.jpg

3. Neuroscience of sleep and dreams
Screenshot_20210808-131631_Adobe Acrobat.jpg


Vingine mtaongezea
 
Natamani kila mtu ajifunze Neuroscoence nitaambatanisha pdf kwa wanaohitaji
 

Attachments

Wakati mwingine hatujui sababu bali tunajua matokeo tu.

Lonardo akipenda kokakola na wewe ukapenda lonardo ukajikuta unapenda kokakola hayo ni matokeo lakini kujua kwa nini inakuwa hivyo hapo sasa ndio yanapokuja mawazo ya wanasayansi.

Ila wanastahkli pongezi wana sayansi
 
Wakati mwingine hatujui sababu bali tunajua matokeo tu.

Lonardo akipenda kokakola na wewe ukapenda lonardo ukajikuta unapenda kokakola hayo ni matokeo lakini kujua kwa nini inakuwa hivyo hapo sasa ndio yanapokuja mawazo ya wanasayansi.

Ila wanastahkli pongezi wana sayansi
Kuna umuhimu mkubwa wa kujua sababu, vinginevyo utakuwa mtu wa kuchezeshwa sindimba
 
Mkuu weka walau kwa muhtasari sababu zake ili utufungue akili kidogo,halafu tutasoma kujazilia.
 
Unatuwekea ma cover ya vitabu unasema vitabu, wee jamaa sikuelewi kabisa yaani.....
 
Kuna umuhimu mkubwa wa kujua sababu, vinginevyo utakuwa mtu wa kuchezeshwa sindimba
Hakuna mwisho wa sababu.

Na pengine ikawa ni ngumu kujua sababu kuliko tunavyofikiria mkuu.

Na kujua sababu inaweza kuwa kubeti maana hakuna marejeo ambayo wanadunia wsmekubaliana kwamba warejee hapo
 
Hakuna mwisho wa sababu.

Na pengine ikawa ni ngumu kujua sababu kuliko tunavyofikiria mkuu.

Na kujua sababu inaweza kuwa kubeti maana hakuna marejeo ambayo wanadunia wsmekubaliana kwamba warejee hapo
Point yako ni ipi hasa?
 
Hicho cha pili kinapatikana Z LIBRARY
Google
b-ok.org
Kisha kisearch na udownload kina MB nyingi kinagoma kuki upload
 
Nataka nitengeneze my own cult.

"Hatari zaidi ya Freemasonry"

Stay tuned

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
Freemason msingi wake ni George Mason ambaye alikuwa anatatizo la psychopathy, yeye hakuona shida kuua mtu.

Tafuta kitabu chochote kinachohusu psychopathy usome.
 
Back
Top Bottom