Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Pablo kaanza na mguu mbaya Simba. Mwanzoni tu kaikuta timu haina Chama wala Luis na hapo hapo kakutana na sapraizi ya mwaka ya Muzamiru, Boko, Mugalu na Kagere wote wameshuka viwango ghafla jumlisha majeruhi. Lakini kajitahidi kuifikisha Simba robo fainali japo inachechemea kwenye NBC ligi. Da Rosa hakuwa na jipya sana alisafiria nyota ya Kishingo mpaka viongozi waliposhtuka wakajikuta Simba haina timu bali ina wachezaji wenye majina makubwa tu.
Naamini huyu Pablo akipewa wachezaji wapya wa maana watano tu atafanya vizuri zaidi ya alipofika mwaka huu. Apate tu:-
1. Mafowadi wawili wakali wa kigeni wawe na uwezo wa zaidi ya Mugalu na Kagere
2. Fowadi mmoja mkali wa kibongo awe na uwezo sawa na Boko alivyokuwa kwenye "peak ". Kati ya mpole au Lusajo mmoja atawafaa sana
Simba
3. Viungo wawili wakali na wawe wote wanaweza kushambulia na kukaba kama alivyokuwa Fraga.
Na Simba sasa isirudie tena kuleta vijana wa kiume kama wakina Banda, Sakho, Mwanuke, Israel na Mhilu kama vile inatengeneza academy wakati under 20 na 17 tayari zipo Simba. Vijana waliopo wanatosha sana. Simba sasa isajili wanaume wa kuleta matokeo kama wakina Phiri, Adebayor, n.k. ili hao vijana wakina Banda, Sakho na wenzano wajifunze kutoka kwa hao wanaume. By the time hao wanaume wanastaafu utakuta hao wakina Banda na wenzake nao watakuwa "matured enough" kuachiwa timu na Simba itakuwa kwenye mikono salama.
Mwisho Simba ijitahidi kusajili wachezaji wapambanaji badala ya kuingalia tu kipaji. Kwa mfano ukimwangalia Bwalya ni bonge la mchezaji ana kipaji cha hali ya juu lakini sio mpambanaji kabisa. Lakini kuna wachezaji kama Inonga, Morison na Kapombe unawaona kabisa wanatumia mpaka pumzi yao ya mwisho kupambania timu. Kwangu mimi ni heri mara mia kuwa na mchezaji mpambanaji asiye na kipaji kikubwa sana kuliko kuwa na mchezaji mwenye kipaji kikubwa halafu hapambanii timu.