Nashauri Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula ang'atuke na akabidhi mikoba kwa Abdulrahman Kinana

Nashauri Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Philip Mangula ang'atuke na akabidhi mikoba kwa Abdulrahman Kinana

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wazalendo Wote Nchini

Natoa ushauri ufuatao kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi yetu.

Sio Siri Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM upande wa Bara amekuwa na Utumishi wa muda mrefu uliotukuka akihudumu kwenye nafasi mbalimbali ndani na nje ya Chama

Hata hivyo pamoja na ukweli huo naona kuwa huu ni upepo muda muafaka kwake wa kung'atuka na kukabidhi mikoba kwa mrithi wake

Kwa Maslahi Mapana ya nchi yetu nashauri Kamarada ABDULAHAMAN Kinana Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM achukue mikoba yake

Kamarada Kinana ana uwezo mkubwa wa kuimarisha & kuunganisha & kukijenga Chama kikamilifu kulingana na mazingira ya sasa ya kisiasa

Kamarada Kinana anakubalika WanaCCM na atakuwa msaada mkubwa kwa Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani na CCM kwa ujumla Kuelekea uchaguzi wa 2022 na 2025.

Twende na Mama
Twende na Kamarada Kinana.
KaziIendelee
Watetezi wa Mama

UPDATES: March 31,2022

Kamarada Abdulhaman Kinama amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kuchukua nafasi ya Philip Mangula
 
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM Makamu Mwenyekiti wa Chama ndiye Mnadhimu! Nawaza Kinana sasa kuna Mnadhimu mmmhh!
 
Tunaenda mbele, au tunarudi tulikotoka? Vijana maelfu wanaohitimu vyuo kila mwaka hamwaoni!?
 
Hicho chama kimepoteza kila kitu. Kimepoteza wanachama wale wenye kukifia toka moyoni. Kimebaki na wanachama matumbo, wanachama kulinda maslahi.

Kimepoteza ushawishi, hata waliopo kwenye nafasi iwe serikalini au kwenye chama, imefika mahala hawajielewi wawe na muelekeo gani.

Kimebaki chama ambacho ambacho hata kikishindanishwa na jiwe kwenye uchaguzi wowote,jiwe litachaguliwa na wananchi ili mradi uwe wa haki. Kimebaki chama kutisha watu, kutumia mabavu, polisi kwenye kila inapotaka kupenya.
 
Unataka CHADEMA warudishe mambo ya pembe za ndovu wakati tulishasahau mambo hayo?

Kazi ya kutetea wahalifu tunachoka.
 
Aaah hawa wazee wakae pembeni, wawe washauri tu sasa
 
Mnataka Ajiuzulu ili mrasimishe ufisadi?
Hatoki ng'oo mpeni sumu tu
 
Hapo ni hila tu ya fisadi kumtosa mzee Mangula kwa kuwawekea kiwingu project yao ya kujenga bandari Bagamoyo. Mzee mangula kawaambia ilani ya CCM ni kujenga gati Bagamoyo sio bandari. Hapo tayari washakuja na mpango kumuweka mtu wao mzee Kinana. Huyu aliyesikikika akimnanga Magufuli na vijana wake Nape na Januari Makamba.
 
Vijana s ndo nyie tukiwapa madaraka mnaanza kupora mali za watu
Wewe acha upuuzi huyo mnaemtetea si ndiye mwenye genge la wavunaji wa pembe za ndovu? Unakumbuka meli inayomilikiwa na familia ya huyo msomali ilikamatwa Vietnam ikiwa imebeba magunia ya choroko kumbe chini kuna magunia ya unga wa pembe za ndovu? Alipoulizwa alikubali kuwa hiyo meli ni yake lakini hautambui huo mzigo,
 
Acheni ujinga, mna utoto mwingi toka lini vijiji Kijiji kikakosa wazee mzee...mipango yenu ya wizi inabuma Mangula yupo kwa kazi maalum
 
Ile sumu aliyolishwa imepoa?

Wahusika wameonywa? Kwakuwa hawagusiki!
Hapo hamukuona mashitaka ya kuwadhuru viongozi wa kitaifa?
Waliokusudia kukata matawi ya miti sheria ikaonyesha ugaidi.
Tunapata aibu kimataifa kwa unyanyasaji kisiasa.
 
Wadau wa JamiiForums

Wazalendo Wote Nchini

Natoa ushauri ufuatao kwa kuzingatia maslahi mapana ya Nchi yetu.

Sio Siri Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM upande wa Bara amekuwa na Utumishi wa muda mrefu uliotukuka akihudumu kwenye nafasi mbalimbali ndani na nje ya Chama

Hata hivyo pamoja na ukweli huo naona kuwa huu ni upepo muda muafaka kwake wa kung'atuka na kukabidhi mikoba kwa mrithi wake

Kwa Maslahi Mapana ya nchi yetu nashauri Kamarada ABDULAHAMAN Kinana Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM achukue mikoba yake

Kamarada Kinana ana uwezo mkubwa wa kuimarisha & kuunganisha & kukijenga Chama kikamilifu kulingana na mazingira ya sasa ya kisiasa

Kamarada Kinana anakubalika WanaCCM na atakuwa msaada mkubwa kwa Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani na CCM kwa ujumla Kuelekea uchaguzi wa 2022 na 2025.

Twende na Mama
Twende na Kamarada Kinana.
KaziIendelee
Watetezi wa Mama
Njama zenu za kurudisha utawala fulani tunazijua. Mkifanya hivyo mtakuwa wahuni wakubwa
 
Back
Top Bottom