Nashauri Mawaziri kuchuja maneno na kauli kabla ya kuzungumza mbele ya Umma ili kutoleta taharuki

Nashauri Mawaziri kuchuja maneno na kauli kabla ya kuzungumza mbele ya Umma ili kutoleta taharuki

Tena ingekuwa mm ndio niko kwenye nafasi hiyo ya waziri wa michezo, watakaokuja na jezi za wapinzani kabla sijawarudisha makwao ningewachapa bakora 12 za moto.
 
Nchi hii baadhi ya watu wana mihemko ya kipuuzi, Waziri hakuna alicho kosea yuko sahihi.
Huna haja ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayo tokea nje ya nchi ukiwa uwanjani.

Unaweza kushangilia iyo timu pinzani bila kuvaa jezi, Jezi yako kavae mtaani au kwako ui burudishe nafsi yako.

Nenda uwanjani kashangilie timu uipendayo(pinzani) hakuna atakaye kusumbua.

Waziri katika nafasiyake angalau ameonyesha kutokubaliana na mambo ya kipumbavu na ame kemea na wapo Watanzania wengi wame muunga mkono kwa jambo ilo.
Kamsikilize tena. Amesema hata kushangilia timu ngeni uwanjani hairuhusiwi. Pia hata hiyo ya kuvaa jezi, ulikuwa wapi kukemea wakati viongozi wako wanavaa jezi za Kaizer Chiefs?
 
Wewe na wazir wote ni wapumbavu mnafanana akili.
Kwani mamelodi ni timu ya taifa? Kwani tunavyoshabikia Man U au Liverpool mbona akatazi?
Yaani Jezi ninunue kwa pesa yangu, nikate tiketi kwa pesa yangu Halafu uniletee upumbavu!
Naval Jezi ya Al ahly au mamelodi huwezi kunilazimisha nivae simba na yanga.
Kwa sheria gani ya mpira? Kwa sheria gani ya nchi nimevunja?
Acha CCM waendelee kutawala sababu si viongozi wala raia kama wewe wamejaa makamasi kichwani
Wazungu walisha acha upuuzi uo tangu miaka ya 1960, karibu miaka 60 iliyopita.
Na ao ndio walio tuletea mpira wa miguu.
 
Tena ingekuwa mm ndio niko kwenye nafasi hiyo ya waziri wa michezo, watakaokuja na jezi za wapinzani kabla sijawarudisha makwao ningewachapa bakora 12 za moto.
Kwa sheria ipi iliyo ndani ya nchi hii?
 
Nchi hii baadhi ya watu wana mihemko ya kipuuzi, Waziri hakuna alicho kosea yuko sahihi.
Huna haja ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayo tokea nje ya nchi ukiwa uwanjani.

Unaweza kushangilia iyo timu pinzani bila kuvaa jezi, Jezi yako kavae mtaani au kwako ui burudishe nafsi yako.

Nenda uwanjani kashangilie timu uipendayo(pinzani) hakuna atakaye kusumbua.

Waziri katika nafasiyake angalau ameonyesha kutokubaliana na mambo ya kipumbavu na ame kemea na wapo Watanzania wengi wame muunga mkono kwa jambo ilo.
Mjinga mwingine huyu hapa, unaweza unaweza unaweza and all brah brah hayo unazungumza kwa base ipi?
 
Hilo ni sahihi!ni Bora ukavaa t shirts za watani was jadi kuliko za timu pinzani ya nje ya nchi!!
Kwa sheria kifungu namba ngapi kwenye katiba ya nchi?
Kila mtu ana uhuru wa kuvaa anacho taka ,ana uhuru wa kupenda anacho kipenda na sio kulazimishana.

Mpira ni mchezo wa furaha hivyo mtu anashangilia timu anayo ona inampa furaha na sio kurazimisha mtu ashabikie timu asiyo ipenda.

Huyu waziri wenu naona analazimisha Tz ije kupigwa rungu na FIFA.
 
Mpaka waje kumtukana mwenza wake ndio atawambia wanakosea raisi amekusanya kundi la wahuni mwenyewe anasema ndio wasaidizi matokeo yake kila mmoja anajisemea bila kupima kauli!
Tangu nilipomsikia akisema ukizingua nakupumzisha, ukinifurahisha nakurejesha nikagundua hatuna Rais. Kwamba timu yake ni ileile kama usajili wa Mtibwa yenye Wachezaji 30. Hairuhusiwi kuchukua nje ya wigo wa wapendwa wake. Kama Rais angekuwa makini Molel na Ndumbaro wasingekuwa sehemu ya Baraza la Mawaziri.
 
Nchi hii baadhi ya watu wana mihemko ya kipuuzi, Waziri hakuna alicho kosea yuko sahihi.
Huna haja ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayo tokea nje ya nchi ukiwa uwanjani.

Unaweza kushangilia iyo timu pinzani bila kuvaa jezi, Jezi yako kavae mtaani au kwako ui burudishe nafsi yako.

Nenda uwanjani kashangilie timu uipendayo(pinzani) hakuna atakaye kusumbua.

Waziri katika nafasiyake angalau ameonyesha kutokubaliana na mambo ya kipumbavu na ame kemea na wapo Watanzania wengi wame muunga mkono kwa jambo ilo.
Hili linafanyika duniani kote na Hakuna dhambi katika Hilo Acha ujinga na Waziri wako Mbumbumbu. Brazil ina mashabiki dunia nzima, siku inacheza pale Afrika Kusini Wazulu wengi walivaa jezi zào.
Uzalendo uchwara mnaohimiza kaeni nao Wezi wakubwa wa Mali za Umma. Hivi mashabiki wa Simba wakiingia na jezi zào nyekundu siku ya Yanga vs Mamelody wakashangilia Mamelody mwanzo mwisho mtawakamata?
 
Hana watoto wakuwapangia jinsi ya kuvaaa...??!
Anajisumbua tu.. yaani mtu atoke Songea huko anipangie jinsi ya kuvaa!
 
Sasa Huyu ndiye Lucas Tunayemtaka..
Safi sana nakupongeza mwa hili!
Huu ndo uzalendo halisi..

Ila sio Huu uliokuwa ukiufanya 👇👇👇👇
Screenshot_20240319_221539_Facebook.jpg
 
Hili linafanyika duniani kote na Hakuna dhambi katika Hilo Acha ujinga na Waziri wako Mbumbumbu. Brazil ina mashabiki dunia nzima, siku inacheza pale Afrika Kusini Wazulu wengi walivaa jezi zào.
Uzalendo uchwara mnaohimiza kaeni nao Wezi wakubwa wa Mali za Umma. Hivi mashabiki wa Simba wakiingia na jezi zào nyekundu siku ya Yanga vs Mamelody wakashangilia Mamelody mwanzo mwisho mtawakamata?
Hakuna popote uo upuuzi wenu, iyo Dunia unayo zungumzia Kijiji cha Tanzania.
Uko Argentina kwenye ushabiki wa ngumi unao tambulika Duniani hawana uo upuuzi.

Pale Cairo palipo tokea vifo vya mamia ya mashabiki hawana uo upuuzi wa kwenda na jezi ya timu pinzani kuishangilia uwanjani.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hekima na unyenyekevu mkubwa sana,kwa upendo na heshima kubwa sana na uzalendo wa hali ya juu sana ningependa kutoa rai na ushauri wangu kwa viongozi wangu hasa Mawaziri kuchunga sana ndimi zao,vinywa vyao kabla ya kutoa maneno ,matamshi na kauli kwa umma au hadharani. Hii ni kwa kuwa Waziri ni kiongozi wa juu sana katika ngazi ya uongozi wa Taifa letu,ni mjumbe wa baraza la mawaziri chombo cha juu kabisa kiuongozi,ni sehemu ya chombo kinachomshauri Mheshimiwa Rais katika masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Hivyo wajumbe wake au mjumbe wake anatarajiwa kuwa mwenye hekima, busara, unyenyekevu, uzalendo, utulivu, uvumilivu, utii kwa Taifa lake na makini katika mambo yake.kwa sababu maneno ya waziri yana athari kubwa sana katika jamii tofauti yakitolewa na mtu wa chini yake ndani ya wizara kwa kuwa yanaweza kuleta taharuki, sintofahamu na Mjadala unaoweza chochea hata chuki kwa serikali yote na wakati mwingine mashambulizi yakaelekezwa kwa Rais mwenyewe ambaye ndiye mteuaji. Ndio maana ni muhimu sana waziri kama hana neno au taarifa za kutosha na rasmi juu ya jambo fulani ni bora aka kaa kimya kujipa muda kabla ya kutoa au kufanya maamuzi au kutoa maelekezo au kauli au maagizo.

Mfano nimeisikia kauli ya Mheshimiwa waziri mmoja akisema kuwa haitaruhusiwa kwa mtanzania kuingia na jezi ya timu pinzani uwanjani wakati timu mgeni ikija kucheza na club zetu za hapa nyumbani ,kwa kuwa utakuwa siyo uzalendo. Kwanza ningependa kusema kuwa uzalendo haupo na haukai katika jezi au rangi ya nguo au tisheti aliyovaa mtu.uzalendo upo katika moyo wa mtu ambao utajionesha nje kupitia matendo.hii ndio maana kuna watu wana kaa maofisini tena ofisi kubwa na za hadhi kubwa lakini wanafanya ufisadi,wanapokea rushwa na kuiba mali za umma ikiwepo pesa au kusaini vitu kwa maslahi binafsi huku ukutani mwa ofisi zao kukiwa na Picha ya Rais ikiwatizama.

Wapo wengine wanapokea rushwa kutoka kwa maskini bila hofu ya aina yoyote ile huku katika viuno vyao wakiwa wamevaa mkanda wenye rangi ya bendera ya Taifa. Kwa hiyo ni lazima tujifunze kupanda mbegu za uzalendo katika mioyo ya watu wetu na siyo kuupima uzalendo wa mtu kwa kuangalia mavazi aliyo yavaa.maana kama nimavazi ndio yangekuwa ni kipimo na tafsiri ya uzalendo basi tungekuwa tunaamua tu vazi fulani wavae viongozi wetu ili wafanye mambo yao kwa uzalendo.

Maana katika suala la jezi wapo watu mitaani utakuta anajezi ama tisheti ameinunua kama sehemu tu ya mavazi yake na wala siyo kwa kuwa ni mshabiki wa timu hiyo.mwingine anaweza ipenda mwonekano tu au rangi yake tu.ndio maana unaweza mkuta mtu amejivalia zake leo jezi ya man u au man city au Liverpool kutoka uingereza ,au Madrid au Barcelona kutoka Spain au Chelsea kutoka Uingereza au psg kutoka Ufaransa au Dortmund kutoka Ujerumani au ajax kutoka uholanzi au Maccab Tel Aviv au Maccab Haifa kutoka Israel au Porto kutoka ureno au juve au Roma au Intermilan kutoka italy. Mtu anavaa tu japo siyo Raia wa nchi mojawapo ya ulaya na wala hajawahi kufika ulaya.

Mimi mwenyewe japo ni mshabiki wa Dar Yanga Afrika lakini kuna wakati nimevaa sana jezi ya man u japo sikuwa mshabiki wa man u lakini nilinunua na niliivaa tu kama sehemu ya nguo yangu kama zilivyo zingine.kwa hiyo kumzuia mtu kwasababu amevaa jezi ya club nyingine mtu aliyelipia tiketi kutizama mchezo huo inakuwa siyo sawa na ni kumuonea sana na kujenga chuki na hasira kwa watu zisizo na sababu ya aina yoyote ile..kwa sababu hakuna mahali sheria inapokataza mtu kufanya hivyo. Lakini pia inakuwa ni kupoteza na kuondoa Radha ya mpira ambao siku zote ni burudani, furaha na utani na siyo amri amri tu. Utani na kuzodoana kwa simba na yanga ndiko kumefanya club zetu hizi kupata mafanikio yanaonekana leo hii ,maana kila mchezaji akiingia uwanjani anataka kupambana sana ili timu yake ipate ushindi na kuwapa raha mashabiki wake wanaokuwa wamefurika uwanjani dhidi ya wale wanaokuwa wapinzani wao bila kujali ni watanzania waliovaa jezi za timu pinzani kutoka nje au ni wa kutoka nje moja kwa moja.

Uzalendo ni lazima tuusisitize kwenye timu za Taifa maana huko tunaunganishwa na Utaifa wetu na utanzania wetu lakini siyo huku kwenye club.huku tuombeanage tu zote zisongage mbele ili sifa zijage sana Tanzania na kuipa nchi nafasi ya kujitangaza na hata serikali kuchukua nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii .kama ambavyo simba kwenye jezi zao waliandika kuwa Visit Tanzania.uzalendo tuusisitize lakini si katika namna hii ya kupangiana hadi aina ya nguo za kuvaa kwa ngazi za mashindano ya Club .sisi wenyewe huwa tukienda nje ya nchi wakati mwingine tunapata washabiki huko huko wa ugenini wanaokuwa nao wanataka wapinzani wao watoke.

Kikubwa ambacho kingesisitiizwa ni kuwa hawa watakao vaa jezi za timu pinzani basi wakae eneo lao na siyo kwenda kukaa kwenye mashabiki wa club nyingine ili kuepusha vurugu zinazoweza kutokea hasa kutoka kwa wale waliofungwa.na hivyo kufanya au kuchochea au kupelekea uharibifu wa miundombinu ya uwanjani kama vile kung'oa viti, kurushiana chupa za maji , kupigana ngumi na wakati mwingine kuharibu hata utulivu wa mchezo wenyewe na hata kupelekea vifo. Mpira ni uwekezaji kwa hiyo tuendelee kusisitiza na kujikita katika uwekezaji na kuvutia wawekezaji katika Secta ya michezo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Kijana vipi uteuzi bado tu? Sasa usimponde mteule utaja ukosa hivi hivi....
 
Nchi hii baadhi ya watu wana mihemko ya kipuuzi, Waziri hakuna alicho kosea yuko sahihi.
Huna haja ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayo tokea nje ya nchi ukiwa uwanjani.

Unaweza kushangilia iyo timu pinzani bila kuvaa jezi, Jezi yako kavae mtaani au kwako ui burudishe nafsi yako.

Nenda uwanjani kashangilie timu uipendayo(pinzani) hakuna atakaye kusumbua.

Waziri katika nafasiyake angalau ameonyesha kutokubaliana na mambo ya kipumbavu na ame kemea na wapo Watanzania wengi wame muunga mkono kwa jambo ilo.
Ona hii pumba tena
 
Tangu nilipomsikia akisema ukizingua nakupumzisha, ukinifurahisha nakurejesha nikagundua hatuna Rais. Kwamba timu yake ni ileile kama usajili wa Mtibwa yenye Wachezaji 30. Hairuhusiwi kuchukua nje ya wigo wa wapendwa wake. Kama Rais angekuwa makini Molel na Ndumbaro wasingekuwa sehemu ya Baraza la Mawaziri.
Anataka kutupa kazi tu 2025 wengine tulishaamua kujipumzikia kisiwani!
 
Nchi hii baadhi ya watu wana mihemko ya kipuuzi, Waziri hakuna alicho kosea yuko sahihi.
Huna haja ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayo tokea nje ya nchi ukiwa uwanjani.

Unaweza kushangilia iyo timu pinzani bila kuvaa jezi, Jezi yako kavae mtaani au kwako ui burudishe nafsi yako.

Nenda uwanjani kashangilie timu uipendayo(pinzani) hakuna atakaye kusumbua.

Waziri katika nafasiyake angalau ameonyesha kutokubaliana na mambo ya kipumbavu na ame kemea na wapo Watanzania wengi wame muunga mkono kwa jambo ilo.
Mbona wewe uko Tabora na hushabikii Tabora united bali unashabikia utopolo? Utaunga mkono mkuu wa mkoa wa Tabora akiwakataza wananchi wa Tabora kuvaa jezi ya Utopolo siku ya mechi dhidi ya Tabora united?

Unatetea upuuzi bila kupima athari zake. Kama nyinyi ni wazalendo anzeni kuzipenda timu za mikoa yenu.
 
Kwenye playlist ya Ndumbaro wimbo #1 ni mwaka wa kufosi
 
Back
Top Bottom