Nashauri Mawaziri kuchuja maneno na kauli kabla ya kuzungumza mbele ya Umma ili kutoleta taharuki

Tena ingekuwa mm ndio niko kwenye nafasi hiyo ya waziri wa michezo, watakaokuja na jezi za wapinzani kabla sijawarudisha makwao ningewachapa bakora 12 za moto.
 
Kamsikilize tena. Amesema hata kushangilia timu ngeni uwanjani hairuhusiwi. Pia hata hiyo ya kuvaa jezi, ulikuwa wapi kukemea wakati viongozi wako wanavaa jezi za Kaizer Chiefs?
 
Wazungu walisha acha upuuzi uo tangu miaka ya 1960, karibu miaka 60 iliyopita.
Na ao ndio walio tuletea mpira wa miguu.
 
Tena ingekuwa mm ndio niko kwenye nafasi hiyo ya waziri wa michezo, watakaokuja na jezi za wapinzani kabla sijawarudisha makwao ningewachapa bakora 12 za moto.
Kwa sheria ipi iliyo ndani ya nchi hii?
 
Mjinga mwingine huyu hapa, unaweza unaweza unaweza and all brah brah hayo unazungumza kwa base ipi?
 
Hilo ni sahihi!ni Bora ukavaa t shirts za watani was jadi kuliko za timu pinzani ya nje ya nchi!!
Kwa sheria kifungu namba ngapi kwenye katiba ya nchi?
Kila mtu ana uhuru wa kuvaa anacho taka ,ana uhuru wa kupenda anacho kipenda na sio kulazimishana.

Mpira ni mchezo wa furaha hivyo mtu anashangilia timu anayo ona inampa furaha na sio kurazimisha mtu ashabikie timu asiyo ipenda.

Huyu waziri wenu naona analazimisha Tz ije kupigwa rungu na FIFA.
 
Mpaka waje kumtukana mwenza wake ndio atawambia wanakosea raisi amekusanya kundi la wahuni mwenyewe anasema ndio wasaidizi matokeo yake kila mmoja anajisemea bila kupima kauli!
Tangu nilipomsikia akisema ukizingua nakupumzisha, ukinifurahisha nakurejesha nikagundua hatuna Rais. Kwamba timu yake ni ileile kama usajili wa Mtibwa yenye Wachezaji 30. Hairuhusiwi kuchukua nje ya wigo wa wapendwa wake. Kama Rais angekuwa makini Molel na Ndumbaro wasingekuwa sehemu ya Baraza la Mawaziri.
 
Hili linafanyika duniani kote na Hakuna dhambi katika Hilo Acha ujinga na Waziri wako Mbumbumbu. Brazil ina mashabiki dunia nzima, siku inacheza pale Afrika Kusini Wazulu wengi walivaa jezi zào.
Uzalendo uchwara mnaohimiza kaeni nao Wezi wakubwa wa Mali za Umma. Hivi mashabiki wa Simba wakiingia na jezi zào nyekundu siku ya Yanga vs Mamelody wakashangilia Mamelody mwanzo mwisho mtawakamata?
 
Hana watoto wakuwapangia jinsi ya kuvaaa...??!
Anajisumbua tu.. yaani mtu atoke Songea huko anipangie jinsi ya kuvaa!
 
Hakuna popote uo upuuzi wenu, iyo Dunia unayo zungumzia Kijiji cha Tanzania.
Uko Argentina kwenye ushabiki wa ngumi unao tambulika Duniani hawana uo upuuzi.

Pale Cairo palipo tokea vifo vya mamia ya mashabiki hawana uo upuuzi wa kwenda na jezi ya timu pinzani kuishangilia uwanjani.
 
Kijana vipi uteuzi bado tu? Sasa usimponde mteule utaja ukosa hivi hivi....
 
Ona hii pumba tena
 
Anataka kutupa kazi tu 2025 wengine tulishaamua kujipumzikia kisiwani!
 
Mbona wewe uko Tabora na hushabikii Tabora united bali unashabikia utopolo? Utaunga mkono mkuu wa mkoa wa Tabora akiwakataza wananchi wa Tabora kuvaa jezi ya Utopolo siku ya mechi dhidi ya Tabora united?

Unatetea upuuzi bila kupima athari zake. Kama nyinyi ni wazalendo anzeni kuzipenda timu za mikoa yenu.
 
Kwenye playlist ya Ndumbaro wimbo #1 ni mwaka wa kufosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…